Allan OkeloAllan
  • Mtambue Allan Okelo timu ambazo amecheza, takwimu zake na mkataba wake.
  • Allan Okelo Star Boy aliyetikisa katika usajili na anachokifanya Yanga SC.
  • Goli la kwanza alifunga katika mechi ya 10 dhidi ya Singida Black Stars.

Allan Okelo maarufu kama Star Boy kijana mwenye kipaji kutoka Uganda sasa ni sehemu ya kikosi cha Yanga SC. Alijiunga na timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo 2025/26. Ana umri wa miaka 25 tayari amecheza mechi kwenye NBC Premeir League na CAF Champions League.

SOMA HII: Deal done Allan Okelo asaini miaka miwili Yanga SC/ Orodha ya wanaofuata

Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Allan Okelo usajili wake ulitikisa

Allan Okelo
Allan Okello utambulisho wake Yanga SC. Source: Yanga SC

Januari 10, Allan Okelo alisaini miaka miwili Yanga SC kwenye dirisha dogo la usajili. Ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa timu ya taifa ya Uganda AFCON 2025 hatua ya makundi nchini Morocco. Maisha yake ya soka la ushindani yanaendelea ndani ya kikosi cha mabingwa watetezi.

Inadaiwa Yanga SC ililazimika kutoa dola 300,000 sawa na shilingi milioni 740 akitokea Vipers United ya Uganda. Sababu kubwa ya gharama kuwa kubwa inatajwa Wydad Casablanca walikuwa wanahitaji huduma yake. Wananchi wakafanikisha mpango huo kwenye dirisha dogo.

Huu ni usajili uliotikisa Afrika Mashariki. Ikumbukwe kwamba wakati anasajiliwa alikuwa katika mashindano ya AFCON alipocheza mechi 3 za ushindani na alitoa pasi moja ya goli. Okelo mwenye miaka 25 ni kiungo anayecheza nafasi zaidi ya mbili uwanjani.

SOMA HII: Yanga SC 6-0 Mashujaa FC NBC Premier League/ Highligts, stats, standigs

image

Rekodi za Okelo AFCON 2025

Allan Okelo
Okello Allan akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa.
MechiMagoliAsistiKadi ya njano
3010

Goli la kwanza Allan Okelo Yanga SC

Mchezaji Allan Okelo goli lake la kwanza kwenye ligi alifunga dhidi ya Singida Black Stars kwa mkwaju wa penati. Katika mchezo huo ubao wa Uwanja wa Airtel ulisoma Singida Black Stars 0-3 Yanga SC. Ilikuwa ni 05/03/2026 Uwanja wa Airtel.

CAF Champion League alitoa pasi

Yanga SC 3-0 Kabylie CAF Champions League. Alitoa pasi ya goli dakika ya 63 alimpa Depu. Ilikuwa 15/02/2026. Depu alifunga magoli mawili dakika ya 36 kwa mkwaju wa penati na dakika ya 63. Goli la tatu lilifungwa na Chadrack Boka kwa pasi ya Prince Dube dakika ya 66.

Jedwali la timu alizocheza Okelo

Zitambue timu ambazo amecheza Okelo. Raia huyu wa Uganda katika wakati wa tetesi alikuwa akitajwa Simba SC. Kwa sasa ni mali ya Yanga SC mpaka mkataba wake utakapofika tamati.

Okelo Allan
Okelo Allan kiungo wa Yanga SC. Source: Yanga SC.
TareheTimu
10 Jan 2026Yanga SC
21 Sept 2023Vipers SC
30 Jan 2023Paradou AC
20 Sept 2022Kampala City
21 Januari 2020Paradou AC
1 Julai 2016Kampala City

SOMA HII: Depu mtambo wa mabao: Ataziba pengo la Mayele? Takwimu, rekodi zake hizi hapa, zatikisa bongo

image

Hitimisho

Allan Okelo bado yupo sana ndani ya kikosi cha Yanga SC kwa miaka miwili. Mkataba wake unatarajiwa kufika tamati 31/12/2028. Kwa timu ambayo inahitaji huduma yake itapaswa kuvunja mkataba na Yanga SC.

Share this: