Singida Black Stars kuikabili Azam FC leoKhalid
  • NBC Premier League leo mchezo mmoja mkubwa kuchezwa Singida, saa 10:00 jioni, Uwanja wa Airtel
  • Singida Black Stars kuikabili Azam FC leo Aprili Mosi 2026.
  • Ni mbinu za Kocha Mkuu Othmen Najjar wa Tunisia vs Florent Ibenge raia wa Dr Congo.

Singida Black Stars kuikabili Azam FC leo NBC Premier League. Wenyeji ngome yao ni Singida wanatumia Uwanja wa Airtel kwa mechi za nyumbani. Ipo chini ya Kocha Mkuu Othmen Najjar raia wa Tunisia mwenye miaka 41. Atapambana na Florent Ibenge wa Azam FC, raia wa DR Congo mwenye miaka 64.

SOMA HII:Singida Black Stars vs Azam FC NBC Premier League | H2H, msimamo, takwimu, utabiri

Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Singida Black Stars kuikabili Azam FC leo kazi ipo

Singida Black Stars kuikabili Azam FC leo
Wachezaji wa Singida Black Stars kwenye moja ya mchezo wa ushindani.

Singida Black Stars kuikabili Azam FC leo kazi ipo kutokana na uimara wat imu zote mbili. Wenyeji kwenye mechi 5 Machi, wamepoteza mbili zote wakiwa nyumbani. Je leo watakubali kupoteza mchezo wa 3?

Timu hiyo kwenye mechi kubwa mbili ilipoteza dhidi ya Yanga SC na Simba SC. Mechi 2 za ugenini ilipata ushindi na kuvuna pointi 6. Ikiwa nyumbani imeshinda mchezo mmoja kati ya mechi 3.

Maoni ya Kocha Mkuu Othmen Najjar

Singida Black Stars kuikabili Azam FC leo
Najjar, Kocha Mkuu wa Singida Black Stars

Kocha Mkuu Othmen Najjar amesema kuwa wachezaji wanazidi kuimarika. Kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Azam FC anaamini watafanya vizuri. Ameongeza kuwa wanawaheshimu wapinzani lakini wanahitaji matokeo.

“Sio Azam FC peke yake hapana ila timu nyingi hapa Tanzania zinaonyesha viwango bora. Muda mwingine huja na matokeo ambayo hujatarajia. Kwa maana hiyo ni wazi mpira wa Tanzania umepiga hatua nzuri.

“Hakuna timu ndogo wala timu kubwa. Muhimu kwetu kufanya kile ambacho tumekifanya mazoezini ili kupata matokeo. Tumeanza kurudi hatua kwa hatua. Kipindi nilichokabidhiwa timu tulikuwa nafasi ya 13. Na sasa tunazidi kuwa bora tuna wachezaji wazuri ambao wanaweza kutupeleka katika hatua nzuri zaidi,”.

SOMA HII: Mtibwa Sugar 1-3 Singida Black Stars, KMC FC yapigwa na Azam FC/ Namungo FC vs Yanga SC lineups

image

Maoni ya Ibenge wa Azam FC

Singida Black Stars kuikabili Azam FC leo
Florent Ibenge Kocha Mkuu wa Azam FC. Source: Azam FC.

Kocha wa Azam FC, Florent Ibenge amesema mchezo wa leoni muhimu kupata pointi tatu. Kocha huyo mchezo uliopita ugenini alivuna pointi moja dhidi ya Mashujaa FC. Amebainisha kwamba wachezaji wanahitaji ushindi.

“Akili zetu kwa sasa kuelekea mchezo dhidi ya Singida Black Stars zinawaza ushindi. Tunajua itakuwa ni ngumu, tunataka kucheza soka safi dakika zote 90. Ni bahati kwa wachezaji na soka la Tanzania kuwa na aina hii ya mechi,”.

Msimamo wa NBC Premier League 2025/26

POSMPWDLPTS
1.Yanga SC16115038
2.Simba SC1494131
3. Azam FC1578029
4. JKT Tanzania1777328
5.Pamba Jiji FC1667325
6.S. Black Stars1574425
7.M. Sugar1757522
8.Namungo FC1756621
9.Dodoma Jiji FC1756621
10.TRA United 1655620
11.Mashujaa FC1747619
12.Fountain 1644816
13.Coastal Union1636715
14.Mbeya City1634913
15.T. Prisons17341013
16. KMC FC1622128

SOMA HII: Singida Black Stars 1-2 Simba SC NBC Premier League/ Highlights, goal, standings

image

Hitimisho

Singida Black Stars kuikabili Azam FC leo NBC Premier League. Huu ni mchezo mkubwa ndani ya ligi namba 6 kwa ubora Afrika. Azam FC haijapoteza mchezo msimu huu je wenyeji wataivunja rekodi?

Share this: