Brazil --- FranceBrazil --- France
  • Licha ya kumaliza mchezo wakiwa wachezaji 10 baada ya staa wao, Dayot Upamecano kuonyeshwa kadi nyekundu, France wamefanikiwa kupata ushindi muhimu wa mabao 2-1 vs Brazil.
  • Ni mabao ya, Mbappe & Ekitike ndiyo yaliyowapa ufaransa ushindi huo muhimu.
  • Kipigo hiko kiliwaacha mashabiki wa Brazili waliokusanyika katika Uwanja wa Gillette huko Massachusetts, Marekani wakiliimba jina la staa wao Neymar Jr aliyeachwa kikosini.

Licha ya kumaliza mchezo wakiwa wachezaji 10 baada ya staa wao, Dayot Upamecano kuonyeshwa kadi nyekundu, France wamefanikiwa kupata ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Brazil. Ni mabao ya, Kylian Mbappé & Hugo Ekitike ndiyo yaliyowapa ufaransa ushindi huo muhimu. Kipigo hiko kiliwaacha mashabiki wa Brazil waliokusanyika katika Uwanja wa Gillette huko Massachusetts, Marekani wakiliimba jina la staa wao Neymar Jr

SOMA HII PIA: Spain vs Brazil: Preview, Team News & Prediction 23/24

Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Mchezo ulikuwaje?

Kwa ujumla France ndio waliokuwa na udhibiti mkubwa wa umiliki wa mpira, wakimaliza mechi kwa asilimia 53.9 dhidi ya 46.1 ya Brazil licha ya kwamba Brazili walitengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga. Mpaka mchezo unakamilika Brazil walipiga mashuti 17 huku 4 yakilenga lango, huku Ufaransa wao wakipiga mashuti 7 tu, ambapo 3 yalilenga lango na kupata mabao 2. Hii inaonyesha namna gani safu ya ushambuliaji ya Brazil ilikuwa mbovu mbele ya langu kulinganisha na France.

Mbappe & Ekitike, Dembele, Olise waiteka shoo

Mbappe & Ekitike Olise Dembele
Mbappe & Ekitike Olise Dembele

Mastaa 4 wa Ufaransa, Kyliani Mbappe, Hugo Ekitike, Michael Olise na Ousmane Dembele walimaliza mechi hiyo na takwimu za juu. Mbappé alipokea pasi safi kutoka kwa Ousmane Dembélé dakika ya 32 na kupiga mpira kwa ustadi juu ya kipa wa Brazil Ederson aliyekuwa akimkabili, akiiandikia France bao la kuongoza. Hili linakuwa bao la 56 kwa Mbappé katika mechi yake ya 95 akiwa na timu ya taifa ya France na sasa anakaribia kuvunja rekodi ya Olivier Giroud mwenye mabao 57 ya mfungaji bora wa muda wote wa nchi hiyo.

Mbappe mwenye umri wa miaka 27 alitolewa katika dakika ya 66 na nafasi yake kuchukuliwa na Marcus Thuram. Mbappe alicheza mechi yake ya kwanza kwa Ufaransa akiwa na miaka 18 mwaka 2017, amerejea kutoka kwenye majeraha ya goti. Mara ya mwisho staa huyo kuanza kikosini ilikuwa Februari 22, akiwa na Real Madrid.

SOMA HII ZAIDI: Best Fifa Men’s 11 in 2025 – Mastaa wa PSG wateka tuzo nyingi za kikosi bora duniani mwaka huu

Upamecano apewa umeme

Ufaransa walilazimika kubaki na wachezaji 10 kipindi cha pili baada ya mchezaji, Dayot Upamecano kumfanyia faulo beki wa Brazil Wesley França karibu na eneo la hatari. Hata hivyo, licha ya kuwa pungufu ya mchezaji mmoja, timu ya kocha Didier Deschamps iliongeza bao la pili kupitia kwa staa wa Liverpool, Hugo Ekitiké dakika ya 65. Brazil, wakiongozwa na kocha wa zamani wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, walipata bao la kufutia machozi dakika 13 baadaye kupitia beki Bremer.

Mashabiki Brazil wanamtaka Neymar

Brazil walimkosa mfungaji wao bora wa muda wote, Neymar Jr, ambaye hakujumuishwa kwenye kikosi kutokana na matatizo ya utimamu wa mwili. Licha ya sababu hizo, mashabiki walionekana wakiimba jina la Neymar baada ya mchezo kuisha. Ikumbukwe timu hizo zilicheza katika Uwanja wa Gillette ambao utatumika kwa mechi ya mwisho ya makundi ya Kombe la Dunia ya Ufaransa dhidi ya Norway.

Brazil vs France rekodi ya h2h

Raphinha vs France
Raphinha vs France: credit 433

Timu hizi zilikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1958, ambapo toka wakati huo zimecheza mechi 16. Mpaka sasa France ndio wababe ambapo ushindi wa jana umewafanya kufikisha ushindi wa mechi 7, dhidi ya 6 za Brazil. Mechi 3 zikimalizika kwa matokeo ya sare, huku mabao 50 yakifungwa.

SOMA HII PIA: Yamal na Dembele watikisa listi mastaa 30 Tuzo ya Ballon d’Or 2025

Dondoo muhimu za timu

Katika mfululizo wa maandalizi ya kombe la Dunia, timu ya Taifa ya Brazil pia itakutana na Croatia wakati wa ziara yao fupi Marekani. Kikosi cha Didier Deschamps, kinaitarajia pia mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Colombia. Ikumbukwe Brazil ambao ni mabingwa mara 5 wa kombe la dunia walikuwa na nyakati ngumu kukata tiketi ya kushiriki mashindano hayo. Kikosi cha, Carlo Ancelotti kilimaliza nafasi ya tano katika hatua ya kufuzu kwa CONMEBOL, nyuma ya Argentina, Ecuador, Colombia na Uruguay.

Brazil wamekuwa wakisuasua kurejesha ubabe wake kimataifa, ikishinda mechi 2 tu, kati ya 6 zilizopita (za kirafiki na mashindano). Mwishoni mwa mwaka jana, walifungwa na Bolivia na Japan, lakini Novemba ilikuwa bora kidogo walipoifunga Senegal 2-0 na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Tunisia huko Lille. Ikumbukwe katika Kundi C la Kombe la Dunia, Brazil itavaana na Morocco, Haiti na Scotland, na kama wataongoza kundi hilo, wanaweza kukutana tena na France katika hatua za juu.

Kwa upande wa France, hawakupata shida kufuzu Kombe la Dunia, wakimaliza kileleni mwa Kundi D la UEFA kwa kupoteza pointi mbili tu. Kocha, Didier Deschamps, ambaye ni mmoja wa watu wachache kushinda Kombe la Dunia akiwa mchezaji na kocha (pamoja na Franz Beckenbauer na Mario Zagallo), ataiongoza France katika mashindano yake ya mwisho kabla ya kumpisha kocha, Zinedine Zidane. France haijapoteza mechi saba mfululizo, (ikishinda sita tangu ilipofungwa na Spain katika nusu fainali ya Nations League).

Hitimisho

Vinicius Jr
Vinicius Jr: Credit 433

Mchezo huu umeonyesha ni wapi kila kikosi kina ubora n ani maeneo gani yanapaswa kufanyiwa kazi. Mashindano ya Kombe la Dunia yamekaribia, hivyo ni wazi kila timu inapaswa haraka kuchukua funzo la mechi hii, ili kuunda vikosi vyenye ushindani zaidi. Mbappe & Ekitike wameonyesha uwezo wa kuibeba France hata katika nyakati ngumu.

Mbappe
Mbappe
Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.