- Kamishna mechi namba 7, Mussa Nyamandege afanua sababu ya mchezo kutochezwa
- TRA United vs Simba SC umeahirishwa rasmi Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
- TPLB kupanga tarehe mpya ya mchezo huo
- Timu zote mbili zaridhia, vikosi kazi viliwasili uwanjani kwa burudani ya NBC Premier League
Mchezo kati ya TRA United vs Simba SC umeahirishwa rasmi utapangiwa tarehe na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB). Kamishna wa mechi hiyo namba 7, Mussa Nyamandege amethibitisha kuahirishwa kwa mchezo. Akizungumza kupitia Azam TV amesema aliwaita viongozi wa timu zote mbili.
SOMA HII: TRA United vs Simba SC nani atashinda?/ H2H, Standings, live score
Je bado hujashinda mamilioni ya SportPesa?
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Mchezo wa TRA United vs Simba SC umeahirishwa, TPLB kuamua

Ule Mchezo wa TRA United vs Simba SC umeahirishwa kuchezwa leo Machi 14,2026 umeahirishwa. Sababu kubwa ni Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kujaa maji. Hiyo inatokana na mvua ambazo zinaendelea kunyesha Tanzania.
Kamishna wa mechi hiyo namba 7, Mussa Nyamandege amesema, pande zote mbili zimeridhia mchezo huo kuahirishwa leo Machi 14,2026.
“Kutokana na mvua kubwa ambayo imenyesha, sheria namba moja imegoma kuendesha mchezo wa leo kwa kuwa uwanja umejaa maji na mpira huwezi kudunda.
“Mimi nikiwa ni kamishna wa mchezo ninatangaza rasmi kuahirisha kwa mchezo mpaka tarehe mpya itakapotangazwa na bodi. Kabla ya kuahirisha nimeita viongozi wat imu zote mbili TRA United na Simba SC.
“Tulishauriana na wote wameridhia kwamba mchezo hautachezwa. Mchezo umeahirishwa hivyo hautachezwa kwa leo,”.
Msimamo TRA United vs Simba SC

| POS | MP | W | D | L | PTS |
| 4.Simba SC | 12 | 8 | 3 | 1 | 27 |
| 9. TRA United | 14 | 5 | 4 | 5 | 19 |
Kikosi cha TRA United kilichotarajiwa kuanza
Kabla ya TRA United vs Simba SC kuahirishwa tayari wenyeji waliwatambulisha wachezaji watakaoanza kikosi cha kwanza. Hii hapa orodha ilikuwa namna hii:-
Jean Noel atakuwa langoni.
Wachezaji wengine ni Nasry Kombo, Valentin Nouma, Amy Mapaka, Christopher Tebandeke, Ramadhan Ramadhan, John Lazarus, Chande Chewe, Omary Yusuph, Jamalia Dulaz na Denis Nkane.
Wachezaji wa akiba
Nassoro Kapama, Khasimuh Mugoya, Kaiza John, Ally Ng’anzi, Akandwanaho, Darius Kacou, Seleman Fikirini, Joe Makoye, Isaac Mtengwa na Juma Msati.
SOMA HII: TRA United vs Simba SC nani atashinda?/ H2H, Standings, live score

Kikosi cha Simba SC kilichotarajiwa kuanza
Mohamed Kassali
Mabeki
Mabeki ni Shomari Kapombe, Rushine De Reuck, Nickson Kibabage na Ismael Toure.
Viungo
Inno Loemba, Allasane Kante,Libasse Gueye, Anicent Oura, Yusuph Kagoma na Clatous Chama.
Wachezaji wa akiba
Bashir Salum, Mligo, Vedastus Masinde, Kameta, Hussen Abel, Naby Camara, Mpanzu, Hussen Mbegu, Semfuko na Morice Abraham.
SOMA HII: Azam FC vs Yanga SC: Jeshi la Yanga SC latua Dar leo Ijumaa, h2h, Ratiba, matokeo Ligi Kuu ya NBC
Hitimisho
TRA United vs Simba SC umeahirishwa baada ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kujaa maji. Mvua zinanyesha Tanzania. TPLB watapanga tarehe mpya.

