Azam FC vs Yanga SCAzam FC vs Yanga SC
  • Wakijiandaa kuvaana na Tanzania Prisons kesho Alhamisi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League). Wananchi wamepokea taarifa mpya.
  • Taarifa hii ni ya mabadiliko ya Uwanja kuelekea mchezo wao wa Azam FC vs Yanga SC.
  • Mchezo huu unaojulikana zaidi kama Dar es Salaam Dabi umepangwa kupigwa Machi 15, 2026 kuendana na ratiba.

Huku wakijiandaa kuvaana na Tanzania Prisons kesho Alhamisi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara (Premier League). Wananchi wamepokea taarifa mpya ya mabadiliko ya Uwanja kuelekea mchezo wao wa Azam FC vs Yanga SC, ambao umepangwa kupigwa Machi 15, 2026 kuendana na ratiba. Uongozi wa Azam FC umeenda mbali na kutoa sababu ya maamuzi hayo.

SOMA HII PIA: Yanga SC yatambulisha mashine mpya nne 2025/26 | Benchi la ufundi balaa zito

Je, bado hujashinda mamilioni? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune pesa sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Aviator

Kuhusu ratiba ya Yanga SC mwezi Machi, 2026

Azam yawabadilishia Uwanja Yanga Sc
Kocha Yanga

Kocha wa Yanga SC, Pedro Goncalves ameonekana kutoridhishwa na mpangilio wa ratiba waliyopangiwa. Kwa maelezo yake mechi zao zinaonekana kufuatana, angalau kla baada ya siku mbili. Ratiba ya Yanga SC katika mwezi Machi ilianza na moto wa mchezo wa Kariakoo Dabi, ambapo katika mchezo huo dhidi ya watani zao walitoa Suluhu.

Mechi nyingine zilizo katika ratiba ya Yanga ya mwezi huu ni kama ifuatavyo;

Machi 5, 2026 Singida Black Stars   vs Yanga SC     

Machi 12, 2026 Tanzania Prisons    vs Yanga SC     

Machi 15, 2026 Azam FC vs Yanga SC

Machi 18, 2026 TRA United vs Yanga SC        

Machi 21, 2026 Mtibwa Sugar vs Yanga SC   

SOMA HII PIA: Yanga SC 4-1 KMC FC NBC Premier League 2025/26/ Highligts, magoli, msimamo

Msimamo unasemaje?

Msimamo wa NBC
Msimamo wa NBC

Mpaka sasa Wananchi wanakamatia usukani wa ligi na pointi zao 32 walizokusanya katika mechi 12 walizocheza. ‘Top Four’ na JKT Tanzania walio nafasi ya pili na Azam FC wanaokamatia nafasi ya 3. Simba wanasalia katika nafasi ya 4 na pointi zao 27 walizokusanya katika michezo 12.

SOMA HII PIA: Timu bora zilizofunga ndani ya boksi la 18 Ligi kuu ya NBC Tanzania 2024/2025- Azam FC, Simba SC na Yanga Sc ni balaa

Tamko la kubadili uwanja kuelekea mechi ya Azam FC vs Yanga SC

Uwanja wa Benjamin Mkapa
Uwanja wa Benjamin Mkapa

Uongozi wat imu ya Azam umenukuliwa kuthibitisha kuwa mchezo wake dhidi ya Yanga, utakaopigwa Jumapili ya Machi 15, 2026 utachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Mabadiliko haya ni kutoka Uwanja wa Azam Complex, ambao ulipagwa awali Dar es Salaam. Azam pia wametoa sababu ya maamuzi hayo.

Akizungumzia hilo kupitia Chombo kimoja cha Habari, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Kabla ya msimu kuanza, Azam FC tulichagua kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mechi zetu mbili za nyumbani. Mechi hizi ni dhidi ya Yanga na ile dhidi ya Simba SC badala ya Azam Complex. Tulivyoona taarifa kuwa Uwanja utafungwa kwa ukarabati, tukawa tunaangalia uwezekano wa mchezo huo kuchezwa katika Uwanja wa Azam Complex.

“Lakini wamiliki wa Uwanja wa Benjamin Mkapa wakatuelekeza kuwa, hautotumika pale maboresho yake yatakapoanza na sio kwa sasa hivyo tunaweza kuutumia. Uwanja wa Benjamin Mkapa tunaamini tutakuwa na faida zaidi kucheza dhidi ya Yanga, kwa sababu tumeshakutana nao pale mara nyingi na tumewafunga sana katika Uwanja ule. Hivyo tuwaondoea wasiwasi mashabiki wa Azam na wapenda soka kiujumla.

“Hatuna hofu ya kukutana na Yanga katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, tunaamini tutapata matokeo mazuri.”

Ikumbukwe mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ambao Azam ilicheza katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ulikuwa ni wa mzunguko wa kwanza msimu huu dhidi ya Simba ambao Azam waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

SOMA HII PIA: Dodoma Jiji FC vs Azam FC NBC Premier League/ H2H, Lives core

Matokeo ya mechi 6 zilizopita Yanga SC

Azam FC vs Yanga SC
Libese G

Februari 7, 2026/CAF AS FAR Rabat 1-0 Yanga SC

Februari 15, 2026/CAF Yanga SC 3-0 JS Kabylie     

Februari 22, 2026/NBC Namungo FC 0-1 Yanga SC        

Februari 25, 2026/NBC JKT Tanzania 0-5 Yanga SC        

Machi 1, 2026/NBC Yanga SC 0-0 Simba SC   

Machi 5, 2026 NBC Singida Black Stars 0-3 Yanga

Hitimisho

Azam FC vs Yanga SC mchezo uliopewa jina la Dar es Salaam Dabi, unasubiriwa kwa hamu kutokana na ubora wa timu zote mbili. Sakata la mabadiliko ya kila mara ya viwanja linatoa ujumbe kuwa bado uwekezaji juu ya miundombinu ya viwanja, linasalia kuwa tatizo linalokwamisha ligi yetu. Ni wazi kila timu inawajibika kuhakikisha inamiliki kiwanja chake bora.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.