- Tanzania Prisons wakiri kuwa wanakwenda kukutana na timu bora uwanjani.
- Tanzania Prisons vs Simba SC NBC Premier League Februari 22,2026 saa 3:00 usiku.
- Steve Berkar Kocha Mkuu wa Simba SC akiri mchezo utakuwa mgumu, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Tanzania Prisons vs Simba SC ni ratiba inayofuata NBC Premier League. Mechi itapigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma saa 3:00 usiku. Benchi la ufundi la Wajelajela limekiri kuwa Simba SC nit imu nzuri na ina wachezaji bora. Licha ya kukiri huko limepania kuwazuia kwa mkakati mzito.
SOMA HII: Simba SC 3-0 Greenland FC CRDB Federation Cup/ Yanga SC vs Cosmopolitan FC, matokeo na ratiba
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Tanzania Prisons vs Simba SC nani anapewa nafasi kushinda?

Wakati Tanzania Prisons vs Simba SC wakitarajiwa kuchuana vikali uwanjani, mnyama anapewa nafasi kubwa kushinda. Hii inatokana na rekodi wanapokutana. Kwenye mechi 10, ushindi unyamani mara 6 huku Prisons ikipata ushindi mechi 3 na sare 1.
Prisons kwenye ligi haina mwendo mzuri ikipata ushindi mechi 3. Kwenye mechi 4 zilizopita ilipata ushindi mchezo mmoja. Lakini bado haiwaondoi kwenye ushindani dakika 90 zitaamua nani atatoboa pointi zote tatu.
Matokeo ya mechi za Tanzania Prisons NBC Premier
| 02/02/2026 | Mtibwa Sugar | 2 | 1 | Tanzania Prisons |
| 10/02/2026 | Tanzania Prisons | 1 | 4 | Coastal Union |
| 06/02/2026 | Mashujaa FC | 0 | 0 | Tanzania Prisons |
| 14/02/2026 | Tanzania Prisons | 3 | 2 | Namungo FC |
Matokeo ya Simba SC NBC Premier League

| 07/12/2025 | Simba SC | 0 | 2 | Azam FC |
| 18/01/2026 | Simba SC | 1 | 1 | Mtibwa Sugar |
| 29/01/2026 | Simba SC | 2 | 0 | Mashujaa FC |
| 11/02/2026 | KMC FC | 0 | 2 | Simba SC |
Tanzania Prisons vs Simba SC msimamo NBC Premier
| MP | W | D | L | PTS | |
| 7. Simba SC | 8 | 6 | 1 | 1 | 19 |
| 14.T. Prisons | 13 | 3 | 3 | 7 | 12 |
Maoni ya Kocha wa Tanzania Prisons
Kocha wa Tanzania Prisons, Zedekiah Otieno kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Simba SC, amesema wapo tayari kimbinu na kimwili.
“Simba ni timu nzuri na ina wachezaji wenye ubora hilo tunalitambua. Tumejiandaa kimwili na kimbinu kuwakabili wapinzani wetu,”.

Maoni ya Sabiyanka mchezaji wa Tanzania Prisons
Mchezaji wa Tanzania Prisons, Lambert Sabiyanka amesema wanaiheshimu Simba SC kama timu kubwa kwao hivyo mchezo wao ambao ni kutumia zaidi akili na nafasi.
“Tunatambua tunakutana na timu ya aina gani kwenye mchezo wetu. Wachezaji tumejiandaa vizuri kisaikolojia. Kikubwa ni kuhakikisha tunatumia kwa umakini nafasi,”.
Steve Berkar Kocha Mkuu wa Simba SC maoni yake
Kocha Mkuu wa Simba SC Steve Barker akizungumzia maandalizi ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alibainisha kwamba wanatambua watapata ushindani.
“Tunafahamu wapinzani watatupa ushindani licha ya kwamba hawapo kwenye nafasi nzuri kwenye ligi. Sisi tumefanya maandalizi mazuri ya kimbinu na kiakili wachezaji wangu waende kufanya vizuri kwenye mchezo huu,”.
SOMA HII: Usajili wa Simba SC dirisha dogo balaa! Gueye, Kibabage, Loemba

Masinde kwa niaba ya wachezaji Simba SC
Vedastus Masinde akielezea namna wachezaji wamejiandaa kuwakabili wapinzani Tanzania Prisons alibainisha kwamba wapo tayari.
“Wachezaji tumejiandaa vizuri ili kupata pointi tatu katika mchezo wetu na tupo tayari kuipambania Simba SC kufikia malengo yake na tunaamini kwamba itakuwa hivyo,”.
Hitimisho
Tanzania Prisons vs Simba SC haujawahi kuwa mchezo mwepesi. Timu zote mbili zimetoka kupata ushindi mechi zilizopita nyumbani. Tanzania Prisons ilipindua meza mbele ya Namungo FC huku mnyama akivuna pointi tatu dhidi ya KMC FC. Je nani ataibuka na ushindi kesho? Dakika 90 zitaamua.

