- Yanga SC vs JS Kabylie, CAF Champions League saa 1:00 usiku Uwanja wa New Amaan Complex
- Al Ahly vs AS FAR Rabat, CAF Champions League saa 1:00 usiku, Misri
- Msimamo wa kundi B na matokeo tumekusogezea hapa
Yanga SC vs JS Kabylie, CAF Champions League ni Februari 15 2026. Mchezo huu wa makundi unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku Uwanja wa New Amaan Complex. Yanga SC ili kufuzu hatua ya robo fainali anahitaji ushindi angalau kuanzia magoli 3. Kundi B bado timu iliyo nafasi ya pili haina uhakika kufuzu mpaka dakika 90 zitakapokamilika.
SOMA HII: Yanga inapanga kuwachafua JS Kabylie kwenye CAF Champions League mnamo Novemba 28, 2025
Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.


Yanga SC vs JS Kabylie, CAF Champions League hesabu za kufuzu zipoje?
Yanga SC vs JS Kabylie, CAF Champions League hesabu za kufuzu bado ni moto. Kwenye kila kundi timu mbili zinazonga mbele ambapo Al Ahly tayari ana uhakika. Nafasi ya pili ni AS Far Rabat pointi 8, Yanga SC nafasi ya 3 pointi 5.
Ikitokea Yanga SC akashinda kuanzia magoli 3 atafikisha pointi 8. Ikitokea AS Far Rabat akapoteza atabakiwa na pointi 8. Hapo itatizamwa idadi ya magoli waliyofungana Yanga SC vs AS Far Rabat kumpata mshindi wa pili.
Ikitokea AS Far Rabat akapata sare ama akashinda, basi atafikisha pointi 9. Hivyo tiketi ya mshindi wa pili itakuwa mikononi mwa AS Far Rabat. Kundi B ni moto katika kusaka tiketi ya robo fainali.
Chaguo la Yanga SC ni kushinda mchezo wa mwisho huku AS Far Rabat ushindi ama sare kwake ni faida. Hivyo dakika 90 za maamuzi zitatoa mshindi ambaye atatinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
SOMA HII: Yanga SC yaibana mbavu JS Kabylie CAF Champions League, Azam FC yapoteza / Highlights, magoli

Msimamo wa kundi B

| MP | W | D | L | PTS | |
| 1. Al Ahly | 5 | 2 | 3 | 0 | 9 |
| 2. AS Far | 5 | 2 | 2 | 1 | 8 |
| 3. Yanga SC | 5 | 1 | 2 | 2 | 5 |
| 4.Kabylie | 5 | 0 | 3 | 2 | 3 |
Matokeo ya Yanga SC CAF Champions League
22/11/2025 Yanga SC 1 0 AS Far Rabat
28/11/2025 JS Kabylie 0 0 Yanga SC
23/01/2026 Al Ahly 2 0 Yanga SC
31/01/2026 Yanga SC 1 1 Al Ahly
07/02/2026 AS Far Rabat 1 0 Yanga SC
Hitimisho
Yanga SC vs JS Kabylie, CAF Champions League ni mchezo muhimu kwa timu za kundi B hasa Yanga SC na AS Far Rabat. Yanga SC anahitaji ushindi, AS Far Rabat anahitaji sare. Dakika 90 zitakuwa na majibu nani atasonga hatua inayofuata.

