- CAF Champions League 2025/26 group stage leo inaendelea kuwaka moto
- MC Alger vs Al Hilal CAF Champions League 2025/26 wababe kutoka kundi C watakuwa kazini
- Rhulan Mokwena Kocha Mkuu wa MC Alger na Simone Inzaghi wa Al Hilal kupimana ubavu wa mbinu uwanjani
- Ratiba kamili na msimamo tumekuwekea kwenye makala hii yenye takwimu
MC Alger vs Al Hilal CAF Champions League 2025/26 ni mchezo unaofuata kwenye ratiba leo usiku. Uwanja wa Al Amar wababe hawa watakuwa kazini kutafuta pointi tatu muhimu. Huu ni mchezo wa hatua ya makundi ukiwa ni watano kwa kundi C vinara ni Al Hilal.
SOMA HII: MC Alger ya Mokwena yaanza kwa kipigo 2-1 Al Hilal Omdurman CAF Champions League

MC Alger vs Al Hilal CAF Champions League utabiri unasemaje?
MC Alger vs Al Hilal CAF Champions League utabiri unampa nafasi kubwa mwenyeji kushinda. Faida ya kuwa nyumbani na rekodi yake kushinda mechi 10 kati ya 11 zilizopita akiwa mwenyeji. Licha ya kupewa nafasi hiyo bado Al Hilal sio hawana mwendo mbaya katika matokeo yao. Katika mechi 3 walizokutana, Al Hilal alipata ushindi 2 na sare 1 hivyo anatambua namna ya kumbana mpinzani wake.
Rhulan Mokwena, Kocha Mkuu wa MC Alger anakibarua kizito kulipa kisasi cha mchezo uliopita. Walipokutana kwenye hatua ya makundi mchezo wa kwanza walipoteza ugenini kwa kufungwa magoli 2-1 ilikuwa Novemba 2`,2025.
Ni mwaka mpya na mambo mapya yameanza. Kuna matumaini yakupata matokeo nyumbani na wageni wanajiamini kutokana na mwendo wao kutokuwa mbaya. Ni dakika 90 za burudani ambazo zinasubiriwa kwa shauku kubwa. Mbinu za kocha yupi zitakuwa na majibu, kilakitu kitakuwa wazi.
| 06/02/2026 | MC Alger | vs | Al Hilal/ Saa 4:00 usiku |

Petro de Luanda vs Simba SC
| 7/02/2026 | Power Dynamo | vs | RS Berkane / Saa 10:00 jioni |
| 7/02/2026 | Petro de Luanda | vs | Simba SC/ Saa 1:00 usiku |
| 7/02/2026 | AS Far Rabat | vs | Yanga SC/ Saa 4:00 usiku |
| 7/02/2026 | Kabylie | vs | Al Ahly/ Saa 4:00 usiku |
SOMA HII: CAF Champions League matokeo mechi zote hatua ya makundi 2025/26

FC Lupopo vs Mamelodi Sundowns
| 8/02/2026 | FC Lupopo | vs | Mamelodi Sundowns/ Saa 10:00 jioni |
| 8/02/2026 | Stade Malien | vs | Es Tunis/ Saa 1:00 usiku |
Msimamo wa kundi C

| MP | W | D | L | PTS | |
| 1. Al Hilal | 4 | 2 | 2 | 0 | 8 |
| 2. Mamelodi Sundowns | 4 | 1 | 2 | 1 | 5 |
| 3. MC Alger | 4 | 1 | 1 | 1 | 4 |
| 4. Saint Eloi Lupopo | 4 | 1 | 1 | 2 | 4 |
Msimamo wa kundi A
| MP | W | D | L | PTS | |
| 1. Pyramids | 4 | 3 | 1 | 0 | 10 |
| 2. RS Berkane | 4 | 2 | 1 | 1 | 7 |
| 3. P.Dynamos | 4 | 1 | 1 | 2 | 4 |
| 4.Rivers Utd | 4 | 0 | 1 | 3 | 1 |
Msimamo wa kundi B
| MP | W | D | L | PTS | |
| 1. Al Ahly | 4 | 2 | 2 | 0 | 8 |
| 2. Yanga SC | 4 | 1 | 2 | 1 | 5 |
| 3. AS Far | 3 | 0 | 2 | 1 | 2 |
| 4.Kabylie | 3 | 0 | 2 | 1 | 2 |
Msimamo wa kundi D

| MP | W | D | L | PTS | |
| 1. Stade Malien | 4 | 2 | 2 | 0 | 8 |
| 2. Esperance de Tunis | 4 | 1 | 3 | 0 | 6 |
| 3. Petro de Luanda | 4 | 1 | 2 | 1 | 5 |
| 4.Simba SC | 4 | 0 | 1 | 3 | 1 |
SOMA HII: AS FAR Rabat vs Yanga SC CAF Champions League/ H2H, standings, key player

Hitimisho
MC Alger vs Al Hilal CAF Champions League 2025/26 wanasaka tiketi kutinga hatua ya robo fainali. Timu mbili kila kundi zinasonga mbele. Ikitokea timu mbili au tatu zikalingana pointi kuna kanuni ambazo zinatumika kumpata mshindi, mechi timu ilizocheza, idadi ya magoli yakufunga na kufungwa, idadi ya magoli yaliyofungwa kwa timu husika zilipokutana.

