- Mechi za mzunguko wa tano za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika zitaendelea tena wikiendi hii.
- Wawakilishi pekee wa Tanzania ambao wana nafasi kubwa ya kufuzu Robo Fainali Young Africans nao watakua nchini Morocco.
- AS FAR vs Young Africans ni mchezo unaotajwa kuwa kama fainali, ambao utapigwa siku ya Jumamosi.
- Je, ni kwa matokeo gani yatakayo patikana huko Morocco yataipeleka Yanga Robo Fainali?
Mzunguko wa tano wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utaendelea tena wikiendi hii. Wawakilishi pekee wa Tanzania ambao wana nafasi kubwa ya kufuzu Robo Fainali, Young Africans nao watakua nchini Morocco. Wananchi watavaana katika mechi ya AS FAR vs Young Africans, mchezo unaotajwa kuwa kama fainali ya kusaka tiketi ya kwenda hatua ya Robo Fainali. Je, ni kwa matokeo gani kuipeleka Yanga Robo Fainali? Makala hii inakuletea dondoo muhimu kuhusu mahesabu hayo.
SOMA HII PIA: Matokeo ya Yanga SC CAF Champions League 2025/26/ Standings, fixture
Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Hali ilivyo Kundi la Yanga SC mpaka sasa

Katika droo ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/26, ambayo ilipangwa nchini Afrika Kusini Novemba 3, mwaka huu. Yanga SC walipangwa kwenye Kundi B, pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, AS FAR ya Morocco na JS Kabylie ya Algeria.
Mpaka sasa katika msimamo wa Kundi hilo Yanga SC wanakamatia nafasi ya 2, wakiwa na pointi 5 walizokusanya katika michezo 4 ya kwanza. Al Ahly anaongoza na pointi zake 8, AS FAR wanakamatia nafasi ya 3 na pointi zao 5 sawa na Yanga SC. JS kabylie wao wanabuluza mkia wakiwa na pointi 2 pekee.
Kwa msimamo huo, Je matokeo gani AS FAR vs Young Africans Morocco, kuipeleka Yanga Robo Fainali?
Kuna namna 3 za matokeo ambayo Yanga SC akiyapata basi anaweza kufuzu robo fainali, 1. Yanga SC wanapaswa kushinda mchezo huu vs AS FAR na watakuwa wamefuzu moja kwa moja. 2. Yanga SC wapate sare mchezo huu vs AS FAR kisha washinde dhidi ya JS Kabylie kwenye mchezo wa mwisho. 3. Yanga SC wanapaswa kuhakikisha hata kama watafungwa basi wafugwe kwa tofauti ya bao 1 tu, na ikiwezekana apate goli la ugenini kisha na ashinde mchezo wake vs JS Kabylie wa mwisho.
SOMA HII ZAIDI: Yanga SC vs AS FAR Rabat CAF Champions League ni leo Novemba 22 2025/ Matokeo, ratiba
AS FAR vs Yanga SC historia ya H2H inasemaje?

Hii ni mara ya 2 katika historia kwa timu hizi kukutana, katika mashindano rasmi ya kimataifa. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa New Amaan Complex, Zanzibar Yanga SC waliibuka na ushindi wa bao 1-0. Hivyo kila timu inatarajiwa kuuendea mchezo huu, kama Daraja la kuandika historia mpya kimataifa.
Yanga SC kutua rasmi Morocco leo Jumatano
Tayari kikosi cha Wananchi kimeondoka Tanzania kupitia Dubai, ambapo leo Jumatano rasmi wanatarajia kuwasili nchini Morocco. Uongozi wa Yanga SC kupitia kwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Ali Kamwe umeweka wazi kuwa kikosi chao kitaanza mazoezi ya mwisho mara moja baada ya kutua. Kikosi cha timu hiyo kinatarajiwa kuwa na mastaa wote, isipokuwa baadhi ambao wana sababu binafsi.
Kikosi tarajiwa cha Yanga SC vs AS FAR

Kipa: Djigui Diarra
Walinzi: Israel Mwenda, Mohammed Hussein, Dickson Job, Ibrahim Bacca.
Viungo: Zouzoua Pacome, Allan Okello, Maxi Nzengeli, Damaro, Duke Abuya
Washambuliaji: Depu
SOMA HII PIA: Yanga SC vs AS FAR CAF 22/11/2025: Live Score, H2H, vikosi, takwimu, Habari za timu
Ratiba kamili ya Yanga SC hatua ya makundi CAF Champions League
Yanga SC 1-0 AS FAR Novemba 22, 2025
JS Kabylie 0-0 Yanga SC Novemba 28, 2025
Al Ahly 2-0 Yanga SC inatarajiwa kuchezwa Januari 23, 2026
Yanga SC 1-1 Al Ahly inatarajiwa kuchezwa Januari 30, 2026.
AS FAR vs Yanga SC inatarajiwa kuchezwa 6, Februari 2026.
Yanga SC vs JS Kabylie inatarajiwa kuchezwa Februari 13,2026.
Hitimisho

AS FAR vs Young Africans ni mechi ya kufa na kupona. Licha ya ubora wa AS FAR ambao wanauonyesha katika ligi ya Morocco, bado umadhubuti wa Yanga SC kimataifa umezidi kuimarika. Misimu miwili iliyopita walicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mashabiki wao wanatamani kuona timu inaandika rekodi nyingine kubwa zaidi msimu huu, hasa baada ya kuishia makundi msimu uliopita.

