Petro de Luanda vs Simba SCSemaji Ahmed kwenye mkutano mkuu
  • Kikosi cha Simba SC kimetua rasmi nchini Angola, tayari kwa ajili ya kuwavaa Petro de Luanda katika mchezo wa CAF Champions league.
  • Petro de Luanda vs Simba SC ni mchezo wa Kundi D ambao unatarajiwa kupigwa siku ya Jumamosi.
  • Mpaka sasa Simba SC wana nafasi finyu kufuzu Robo Fainali na wakielekea katika mchezo huu, huku Meneja Habari na mawasiliano, Ahmed Ally akitumia ujumbe mzito kwa mashabiki wao.

Jeshi la Simba SC limetua rasmi nchini Angola, tayari kwa ajili ya kuwavaa Petro de Luanda katika mchezo wa CAF Champions league. Petro de Luanda vs Simba SC ni mchezo wa Kundi D ambao unatarajiwa kupigwa siku ya Jumamosi. Mpaka sasa Simba SC wana nafasi finyu kufuzu Robo Fainali na wakielekea katika mchezo huu, Meneja wa Habari na mawasiliano wat imu hiyo, Ahmed Ally amewatumia ujumbe mzito mashabiki wao.

SOMA HII PIA: Simba SC vs Petro de Luanda nani atachukua pointi tatu CAF Champions League? Stats, prediction

Shinda na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Msimamo wa Kundi la Simba SC baada ya mechi 4

MSIMAMO - Kundi D
MSIMAMO – Kundi D #CAFCL #LigiYaMabingwaAfrika #CAFChampionsLeague

Kwa mara ya kwanza baada ya misimu 7, Simba imeshuhudia msimu mbaya zaidi katika mashindano ya klabu bingwa Afrika. Hii ni baada ya kujikuta wamekusanya pointi 1 tu, katika michezo 4 ambayo wamecheza mpaka sasa. Pointi hiyo moja Simba SC waliipata katika mchezo wa sare ya mabao 2-2, dhidi ya ES Tunis siku ya Jumapili iliyopita. Kabla ya mchezo huo, Simba ilishuhudia vipigo 3 mfululizo ya kwanza hatua ya makundi.

Kwa mwenendo huo Simba mpaka sasa wanabuluza mkia wakikusanya pointi 1, Kundi D la mashindano hayo linaongozwa na Stade Malien ambao wamekusanya pointi 8. Nafasi ya pili inakamatiwa na ES Tunis wenye pointi 6, Petro de Luanda wao wanakamatia nafasi ya 3 na pointi zao 5. Hivyo nafasi ya Simba kwenda Robo Fainali inahitaji miujiza.

Alichosema Ahmed kwa mashabiki wa Simba SC

Petro de Luanda vs Simba SC
Semaji Ahmed kwenye mkutano mkuu

Kufuatia mwenendo huo uliowapa hasira na machungu mashabiki wa Simba SC, meneja Habari na mawasiliano wa timu hiyo, Ahmed amesema: “Umekua msimu mbaya kwetu kwenye michuano ya kimataifa, inauma lakini hatuna budi kukubali kuwa msimu huu umekua mgumu kwetu. Kama ambavyo misimu mingine tunafuzu kwenda Robo Fainali na wengine wanashindwa, basi msimu huu imekua zamu yetu kuanguka.

“Hatuna sababu ya kuvurugana wala kutafuta mchawi, itoshe kusema msimu huu haukuwa wetu au haikua rizki yetu. Tumalizie mechi mbili zilizobaki, baada ya hapo tuwekeze nguvu kwenye mashindano ya ndani huku bado tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri. Poleni ndugu zangu Wanasimba, Tulichozea kufanya tumeshindwa kufanya safari hii, Tukubali kuwa huu ni msimu mbaya kwetu na hutokea kwa timu yeyote Duniani.

SOMA HII ZAIDI:  Simba SC kuwakosa wachezaji muhimu watatu wakiikabili Petro de Luanda CAF Champions League Novemba 23,2025

Kuhusu tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wao Mangungu

Ahmed ameendelea kusema: “Najua tunahasira kufuatia mwenendo wetu katika michuano ya Afrika msimu huu, Lakini hasira zetu zisitufanye tuvunje misingi yetu ya utu na heshima kwa viongozi wetu na sisi wenyewe kwa wenyewe. Hatuna budi kukubali kuwa msimu huu haukua mzuri kwetu, na hilo hutokea kwa kila timu Duniani, hivyo tusijione sisi ni wakosefu sana.

“Rai yangu tusipoteze muda kufarakana wala kubagazana mitandaoni, au kwenye vyombo vya Habari. Tukumbuke kuwa wabaya wetu wananufaika zaidi na marumbano yetu na wanachochea tuvurugane. Muhimu tukumbuke kuwa bado tuna mashindano mengine mbele yetu, ambayo tunapaswa kuwekeze nguvu, akili na maarifa. Ligi Kuu ya NBC na CRDB Cup ni tumaini letu pekee lililobaki, hivyo badala ya kucharurana na kupoteza muelekeo ni vema tukawekeza nguvu huko tupate mafanikio”

Hakuna kukata tamaa

Matokeo ya Simba SC CAF
Kapombe na Gueye

“Tusivunjike Moyo ndugu zangu Wanasimba, tujipange kwa ligi za ndani na tujipange kurejea kwa kishindo msimu ujao katika mashindano kimataifa. Mechi zilizobaki tusimalize kinyonge, kushindwa kufanya vizuri kimataifa msimu huu isitunyong’onyeshe bali itupe nguvu ya kujipanga msimu ujao. Wakati mwingine ili ufike juu lazima uanzie chini, msimu huu tumeteleza lakini tusiivunjie adabu timu yetu ambayo imetupa heshima kubwa Afrika.

“Wakati huu na tuchague cha kusikiliza na tuchague cha kuongea wengi wanaonekana kama wanaipigania klabu, au wanatutetea lakini uhalisia wanachochea vurugu. Tuilinde nembo ya klabu yetu, mnyama atarejea tuu kwenye ufalme wake tena hivi punde tuu

SOMA HII ZAIDI: Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League 2025/26/ Live score, H2H

Hitimisho

Kuhusu mechi ya Petro de Luanda vs Simba SC, Ahmed amesema: “Kikosi chetu kimewasili Angola, pamoja na matumaini yetu kufuzu Robo Fainali kuwa finyu, lakini mchezo dhidi ya Petro ni muhimu sana kwetu. Kupata matokeo chanya itakuwa heshima ya Mnyama.” Kila la kheri Simba SC.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.