- Baada ya vipigo vitatu mfululizo vya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatimaye Mnyama Simba SC amefufuka.
- Hii ni baada ya leo Alhamisi kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa FC.
- Simba SC 2-0 Mashujaa FC ndivyo ubao wa Uwanja wa Meja Generali Isamuhyo ulivyoonesha baada ya dakika 90 za mchezo huu wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League) kumalizika.
- Makala hii inachambua kwa ufupi matukio muhimu ‘highlights’ za mchezo huu.
Baada ya kupitia kipindi kigumu, ikiwemo vipigo vitatu mfululizo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatimaye mnyama amefufuka! Hii ni baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo wa Simba SC 2-0 Mashujaa FC. Mchezo huu ulipigwa kwenye Uwanja wa Meja Generali Isamuhyo, Dar es Salaam. Makala hii inakuletea kwa ufupi ‘highlits” za mchezo huo.
SOMA HII PIA: Simba SC vs Mashujaa FC Ligi Kuu Bara NBC: Matokeo, Ratiba, Live score, H2H, lineups, Habari za timu
Je, Unataka kushinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege kupitia kampuni bora ya kubashiri ya SportPesa. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Simba SC 2-0 Mashujaa FC, mechi ilikuwaje?

Simba SC waliuanza mchezo wakionekana kudhamiria kupata matokeo ya ushindi, hii ni baada ya kupeleka mashambulizi mfululizo langoni kwa Mashujaa FC. Juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 27 ya mchezo baada ya nyota wa Kimataifa wa Senegal, Libasse Gueye kufunga bao kutoka nje ya 18 kwa shuti kali la mguu wa kushoto. Gueye alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi ya Kibu Denis. Bao hilo liliendelea kudumu mpaka kipindi cha kwanza kilivyomalizika.
Dakika ya 39 ya mchezo Simba SC walipata faida ya mkwaju wa Penalti, kufuatia mwamuzi, Ahmed Arajiga kutafsiri, Libasse Gueye alifanyiwa madhambi ndani ya 18. Nyota wa Simba SC, Kibu Denis alijitwisha jukumu la kupiga Penalti hiyo ambayo iliokolewa na mlinda mlango wa mashujaa na kufanya mchezo uzidi kuwa na upinzani. Kipindi cha Pili Simba waliendelea kusukuma mashambulizi mfululizo langoni kwa mashujaa, kwa lengo la kuhakikisha wanapata mabao zaidi na kuimaliza mechi.
Dakika ya 76 ya mchezo Simba SC ilipata bao la pili lililofungwa na mshambuliaji, Selemani Mwalimu. Nyota huyo alifunga bao akitumia madhaifu ya walinzi ambao walishindwa kuondosha mpira wa hatari uliopigwa na mlinzi, Nickson Kibabage na kuokolewa na kipa. Baada ya bao hilo Simba SC iliendelea kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo na kutengeneza nafasi kadhaa ambazo hazikutumiwa na mchezo kuisha 2-0. Huu unakuwa ushindi wa kwanza kwa kocha mpya wa Simba SC, Steve Barker kwenye mashindano ya Ligi Kuu Bara.
H2H, Simba SC vs Mashujaa FC

Simba SC wameendeleza uwiano mzuri mbele ya Mashujaa ambapo mchezo wa leo unawafanya wafanikiwe kushinda mechi 5 mfululizo za karibuni walizokutana na Mashujaa FC. Mashujaa bado hawajafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Simba kwenye michezo ya ligi. Hivyo bado Mashujaa FC wanatafuta nafasi ya kuandika rekodi kuifunga Simba SC kwenye Ligi Kuu Bara.
SOMA HII ZAIDI: Simba SC vs Mashujaa FC dakika 90 za hesabu kubwa Mei 2 2025
Kikosi cha ushindi wa Simba SC 2-0 Mashujaa FC
Kipa: Kassali
Walinzi: Duchu, Nangu, De Ruck, Kibabage
Viungo: Chama, Kagoma, Camara, Morice, Kibu, Gueye
Washambuliaji: Oura
Rekodi ya kocha mpya Simba SC

Mchezo huu ulikuwa kipimo kingine kwa kocha mpya wa Simba SC, Steve Barker ambaye akiiongoza Simba SC katika mchezo wa pili wa ligi, hatimaye amefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza wa mashindano hayo. Ushindi huu unaingia kwenye rekodi kwani kocha huyo anakuwa kocha wa 2 kuiongoza Simba SC kupata ushindi kwenye ligi kuu Bara ya NBC. Ni wazi mashabiki wa Simba SC wameanza kuona mabadiliko ya kikosi chao chini ya kocha mpya na ushindi huu umekuwa wa muhimu kuipa morali kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa vs ES Tunis wikiendi hii.
Msimamo wa NBC Premier League wapi zilipo Simba SC na Mashujaa FC?
Matokeo ya mchezo wa leo yanaifanya Simba SC kukwea mpaka nafasi ya 4 ya msimamo wa Ligi Kuu Bara, hii ni baada ya kukusanya pointi 16 katika michezo 7 waliyocheza. Kwa upande wa mashujaa wao wameshuka kwa nafasi moja mpaka nafasi ya 9 katika msimamo na kusalia na pointi zao 13. Ikumbukwe Mashujaa wamekusanya pointi hizo baada ya kucheza mechi 11.
Hitimisho

Simba SC 2-0 Mashujaa FC ulikuwa ni zaidi ya mchezo. Hii ilikuwa ni nafasi kwa Simba SC kurejesha heshima yake ndani ya ligi, ambayo imeonekana kupungua katika michezo ya siku za karibuni. Lakini hii pia ilikuwa ni nafasi ya kurejesha hali ya kujiamini kuelekea mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ambao Simba SC wanahitaji ushindi kwa namna yoyote ili kufufua matumaini ya kucheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa Mashujaa wameshindwa kurekebisha makosa ya mchezo uliopita wa kipigo cha mabao 6-0 dhidi ya Yanga SC.
SOMA HII PIA: Simba SC yamalizana na Mashujaa FC yaipiga nje ndani dakika 180

