Algeria vs NigeriaAlgeria vs Nigeria
  • Michuano ya Kombe la Matifa ya (AFCON 2025) yanazidi kuchanja mbuga.
  • Kesho Jumamosi itapigwa michezo miwili, lakini mchezo wa Algeria vs Nigeria ndiyo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa.
  • Makala hii inaangazia baadhi ya dondoo muhimu za mchezo huo uliobeba tiketi ya nusu fainali.

Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), yanaelekea mwishoni. Mashindano hayo sasa yanaingia katika hatua ya Nusu Fainali, ambapo kesho Jumamosi zitapigwa Nusu Fainali 2. Algeria vs Nigeria ndio unatajwa kuwa mchezo utakaofuatiliwa zaidi. Makala hii inaangazia baadhi ya dondoo muhimu za mchezo huo.

SOMA HII PIA: AFCON 2025: Matokeo na Ratiba ya Robo Fainali, hizi hapa timu zilizofuzu

Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

H2H, Algeria vs Nigeria AFCON 2025

Historia ya soka la ushindani kati ya Algeria na Nigeria inaonyesha timu hizi zimekutana mara 9. Algeria imeshinda michezo 4, huku Nigeria wakishinda mechi 5. Hivyo hii ni nafasi nyingine kwa timu hizi kuandika rekodi mpya.

Fomu ya Nigeria kwenye AFCON 2025

W W W W

Fomu ya Algeria kwenye AFCON 2025

W W W W

Vikosi tarajiwa Algeria vs Nigeria

Mahrez (-)
Mahrez

Algeria

Kipa: Zidane

Walinzi: Belghali, Mandi, Bensebaini, Ait Nouri

Viungo: Boudaoui, Zerrouki, Chaibi

Washambuliaji: Mahrez, Amoura, Maza

Nigeria

Kipa: Nwabali

Walinzi: Osayi-Samuel, Ajayi, Bassey, Onyemaechi

Viungo: Onyeka, Ndidi, Iwobi; Lookman

Washambuliaji: Osimhen, Adams

SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 Cameroon vs Morocco: Ratiba Robo Fainali Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu

Habari za timu

AFCON 2025
Kikosi cha Nigeria

Timu zote zilizosalia katika hatua hii ya Robo Fainali ni timu nane zilizojuu zaidi kwenye viwango vya ubora Afrika kulingana na viwango vya sasa vya FIFA. Algeria wako nafasi ya 34 kimataifa na watatu Afrika, huku Nigeria wakiwa nafasi ya 38 na ya 5 Afrika.

Algeria walishinda mechi zote tatu za makundi dhidi ya Sudan, Burkina Faso na Equatorial Guinea, wakifunga mabao saba.

Hatua ya 16 bora walivaana na DR Congo, mchezo unaotajwa kuwa mgumu zaidi kwao katika michuano ya mwaka huu.  Algeria ilibidi wasubiri goli la dakika ya 119 kufuzu Robo Fainali likifungwa na Adil Boulbina. Hata hivyo, licha ya kasi yao Algeria ni lazima watachukua tahadhari kuelekea pambano la Jumamosi.

Nigeria wana rekodi nzuri ya AFCON ambapo wamefika angalau nusu fainali katika ushiriki wao 15 kati ya 20. Hii ni ikiwemo mashindano ya mwaka 2023 wakimaliza washindi wa pili. Vijana wa Eric Chelle wameshinda mechi zao zote nne kwenye dimba hili, wakifunga mabao 12 na kuruhusu manne.

Nigeria haijashinda katika mechi nne zilizopita dhidi ya Algeria, ikipoteza mechi tatu za hivi karibuni zaidi, ikiwa ni pamoja na kushindwa kwa mabao 2-1 katika nusu fainali ya AFCON 2019, huku vipigo vingine viwili vikipatikana katika mechi za kirafiki mnamo 2020 na 2022.

Taarifa ya majeruhi

Osimhen (-)
Osimhen

Algeria wanahofu juu ya upatikanaji wa kiungo Ismael Bennacer, ambaye alilazimika kutoka nje kwenye mchezo dhidi ya DR Congo. Jaouen Hadjam, ambaye alikosa mechi mbili zilizopita baada ya kupata jeraha dhidi ya Burkina Faso, anaweza kurejea. Anis Hadj Moussa huenda akakosekana kwa muda uliosalia wa mchuano kutokana na utimamu wa mwili.

Lookman wa Nigeria na Osimhen pia wamefungana mabao matatu, huku Alexander Iwobi akiwa na jukumu la kutoa ubunifu katika safu ya kiungo. Nigeria wanaonekana kuwa na kikosi fiti kabisa, kumaanisha kwamba Chelle huenda akabaki na mfumo wake maarufu wa 4-4-2.

SOMA HII PIA: AFCON 2025: Sami Trabelsi kufukuzwa kazi timu ya taifa Tunisia/ Highlights, fixtures, standings

Hitimisho

Algeria vs Nigeria kweli ni mchezo wa hadhi ya Robo Fainali. Unatarajiwa kuwa mchezo wa kuvutia, mchezo huu unatarajiwa kuwa na matokeo ya kushangaza kwa kila upande, lakini Nigeria wanapewa nafasi kubwa. Hili ni pambano lenye uwiano mzuri kati ya pande mbili pekee ambazo zimeshinda mechi zote nne hadi sasa.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.