AFCON 2025 Uganda 1-1 Tanzania, Simon Msuva aandika rekodi Morocco
Nigeria 3-2 Tunisia matokeo ya kundi C
AFCON 2025 Uganda 1-1 Tanzania ni matokeo rasmi mchezo wa pili kwa kundi C, Desemba 27,2025. Uganda walikuwa na nafasi kushinda dakika ya 89 kupitia penati waliyopata mpigaji Allen Okello alipaisha. Magoli yalifungwa na Simon Msuva dakika ya 59 kwa Tanzania na Uche Ikpeazu kwa Uganda dakika ya 80. Wababe hawa kutoka Afrika Mashariki wamegawana pointi mojamoja.
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.
Msuva Simon nyota wa timu ya taifa ya Tanzania. Source: Taifa Stars.
Desemba 27,2025, Uwanja wa Al Medina, Morocco AFCON 2025 Uganda 1-1 Tanzania. Jumla ya magoli mawili yalifungwa kwenye mchezo huo. Mwamuzi Jalal Jayed aliamuru penati mbili kupigwa, Tanzania walianza kufunga na Uganda walikosa.
Simon Msuva winga wa Tanzania aliandika rekodi ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo. Inakuwa tuzo ya kwanza kwake katika mashindano haya makubwa 2025. Mchezo wa kwanza dhidi ya Nigeria Tanzania ilipoteza hivyo hawakutwaa tuzo baada ya mchezo kukamilika.
Uganda walikuwa kwenye umiliki mkubwa wa mchezo mwanzo mpaka mwisho wa mchezo. Tanzania nafasi ambazo walikuwa wakizipata ilikuwa ngumu kwao kuzibadili kuwa magoli. Katika mechi mbili timu hiyo imefunga magoli mawili.
Feisal Salum nyota wa Tanzania vs Uganda. Source: Taifa Stars.
Kikosi cha Uganda vs Tanzania
Onyango, Sibbick, Obita, Kayondo, Semakula, Mato, B. Alhassan, B.Bobosi, Allen Okelo, T. Mutyaba, J. Ssemugabi. Kocha Mkuu ni Paul Put.
Tanzania kikosi cha kwanza vs Uganda
Timu ya taifa ya Tanzania AFCON 2025. Source: Taifa Stars.
Zuber Foba, Haji Mnoga, Bakari Mwamnyeto, Hamad Bacca, Mohamed Hussen, Msanga, Mirosh, T. Allarakhia, Simon Msuva, Feisal Salum, Kelvin John. Kocha Mkuu ni Miguel Gamondi.
Kipa wa Tanzania, Yacoub Suleiman alikosekana katika mchezo wa pili kutokana na kuumia mazoezini. Aliukosa mchezo wa ufunguzi dhidi ya Nigeria.
Orodha ya wachezaji walioonyeshwa kadi za njano
Kenneth Semakula wa Uganda dakika ya 45+4 Uche Ikpeazu wa Uganda dakika ya 90+4 Kipa Onyango naye alionyeshwa kadi ya njano Dickson Job wa Tanzania dakika ya 72 Haji Mnoga wa Tanzania dakika ya 88
AFCON 2025 Uganda 1-1 Tanzania mataifa mawili kutoka Afrika Mashariki yaligawana pointi. Kwenye kundi C vinara ni Nigeria. Tunisia nafasi ya pili watakutana na Tanzania mchezo ujao na vinara watakutana na Uganda kusaka tiketi kutinga 16 bora.