- Goli la Mohamed Salah laipeleka hatua ya 16 bora Misri ikiongoza kundi B na pointi 6
- AFCON 2025 Misri 1-0 Afrika Kusini hatua ya makundi nchini Morocco
- Zambia 0-0 Comoros matokeo ya mchezo wa hatua ya makundi Desemba 26,2025
AFCON 2025 Misri 1-0 Afrika Kusini ni matokeo rasmi mchezo wa makundi kwa kundi B. Mohamed Salah alifunga goli pekee la ushindi kwa mkwaju wa penalty dakika ya 45. Goli hilo linaipa tiketi Misri kutinga hatua ya mtoano. Licha ya Misri kuwa pungufu kwenye mchezo huo walipambana kuvuna pointi tatu muhimu.
SOMA HII: AFCON 2025 matokeo na ratiba hii hapa/ Msimamo, live scores
Hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

AFCON 2025 Misri 1-0 Afrika Kusini rekodi yaandikwa

Kwenye AFCON 2025 Misri 1-0 Afrika Kusini rekodi imeandikwa kwa timu kutinga hatua ya 16 bora ikiwa pungufu. Mchezaji muhimu kwa kikosi cha Misri alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 45 kipindi cha kwanza. Afrika Kusini mapambano yote kipindi cha pili hayakuleta matunda.
Ni Mohamed Hany alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano. Licha ya kadi hiyo dakika ya 45+2 bado goli la Salah lilidumu mpaka mwisho wa mchezo. Misri inatinga hatua ya 16 bora ikiwa inaongoza kundi B pointi zake ni 6.
SOMA HII: AFCON 2025 Match round 1: Hawa hapa washindi wa tuzo za mchezaji bora wa kila mechi

Mabadiliko katika mchezo
Misri

Eman Ashour in 45 Omar Marmoush out
Mohamed Shehata in out Mahmoud Trezeguet dk 80
Afrika Kusini
Sipho Mbule in Thelenthe Mbatha out dk 45
Relebohile Ratomo in out Oswin Appollia dk 69
Evidence Makgopa in out Sphephelo Sithple dk 75
Elias Mokwana in out Tshepang Moremi dk 79
Kadi za njano
Dakika ya 20 Teboho Mokoena alionyeshwa kadi ya njano kwa Afrika Kusini.
Dakika ya 30 Mohamed Hany alionyeshwa kadi ya njano kwa Miari.
Dakika ya 43 Lyle Foster alionyeshwa kadi ya njano kwa Afrika Kusini
Dakika ya 43 Khuluso Mudau alionyeshwa kadi ya njano mwa Afrika Kusini.
Msimamo kundi B
| MP | W | D | L | PTS | |
| 1.Misri | 2 | 2 | 0 | 0 | 6 |
| 2. A.Kusini | 2 | 1 | 0 | 1 | 3 |
| 3.Zimbabwe | 2 | 0 | 1 | 1 | 1 |
| 4.Angola | 2 | 0 | 1 | 1 | 1 |
Safari ya Misri mpaka hatua ya 16 bora

Misri katika kundi B mchezo wa ufunguzi ilipata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Zimbabwe. Licha ya mchezo wa kwanza kutengeneza nafasi nyingi na kumiliki mpira kwa asilimia kubwa walifungwa goli mapema. Dakika ya 20 ni Prince Dube alifunga goli kwenye mchezo huo.
Misri waliweka usawa kupitia magoli ya Omar Marmoush dakika ya 64. Mohamed Salah alifunga goli la ushindi. Hivyo Misri walifanya Comeback kwenye mchezo wa ufunguzi wakivuna pointi tatu mazima.
SOMA HII: AFCON 2025 Matchday 1: stats, Mechi 12, Magoli 29

Matokeo ya mechi nyingine
Zambia 0-0 Comoros
Angola 1-1 Zimbabwe
Hitimisho
AFCON 2025 Misri 1-0 Afrika Kusini ni mchezo uliozua mjadala mkubwa hasa goli la ushindi. Penalti aliyofunga Mohamed Salah inatajwa kuwa na maajabu yake. Kocha Mkuu wa Afrika Kusini Hugo Broos ameweka wazi kuwa alishangazwa na adhabu hiyo iliyowapa ushindi Misri.

