- AFCON 2025 Matchday 1 imemalizika kwa kishindo, huku mataifa makubwa kisoka yakianza vizuri kwa matokeo ya ushindi.
- Rekodi nyingi zimeandikwa katika michezo 12 ya kwanza.
- Wakati hatua ya mzunguko wa pili ikianza rasmi leo Ijumaa Desemba 26, Makala hii inaangazia baadhi ya rekodi kali kwenye mzunguko wa kwanza.
Mzunguko wa kwanza (AFCON 2025 Matchday 1) umemalizika kwa kishindo, huku mataifa makubwa kisoka yakianza vizuri kwa matokeo ya ushindi. Wakati hatua ya mzunguko wa pili ikianza kutimua vumbi leo Desemba Desemba 26, rekodi nyingi tayari zimeandikwa kwenye michuano yam waka huu. Makala hii inaangazia baadhi ya rekodi kali kwenye mzunguko wa kwanza.
SOMA HII PIA: AFCON 2025 Mahrez, Jackson, Achouri watikisa: Hawa hapa wafungaji bora wa Raundi ya 1
Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

AFCON 2025 Matchday 1 mechi 12 zapigwa

Mzunguko wa kwanza umeshuhudia michezo 12 ikipigwa katika viwanja takribani 9. Viwanja hivi viko katika miji 6 ya nchi hiyo. Kati ya michezo yote mchezo wa ufunguzi kati ya Morocco vs Comoros ndio unabaki kuwa wa kihistoria.
Achana na uwepo wa sherehe za ufunguzi zilizofanyika kabla ya kuanza kwa mchezo. Lakini uwepo wa mashabiki wanaokadiriwa kuwa 60,180 ulitoa msisimko mkubwa. Kama hii haitoshi Morocco waliibuka na ushindi wa mabao 2-0, huku bao la ‘tiktak’ la Ayoub El Kaabi likibaki kuwa gumzo kuu.
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 Match round 1: Hawa hapa washindi wa tuzo za mchezaji bora wa kila mechi
Magoli 29 kambani

Katika michezo hiyo 12 ya kwanza mashabiki wameshuhudia magoli 29 yakiwekwa kambani. Magoli hayo yamewekwa kambani na wachezaji kutoka mataifa tofauti, ambapo wapo waliofunga mabao 2 na wale waliotupia bao moja kila mmoja. Ni mastaa watatu tu ndio ambao wamefunga mabao 2 kila mmoja ambao ni Riyad Mahrez (Argeria), Nicholas Jackson (Senegal) na Elias Ashouri (Tunisia). Kati ya mabao yote bao la Ayoub El Kaabi ndilo linatajwa kuwa bao kali zaidi.
Goli la mapema zaidi

Katika mashindano ya mwaka huu, nyota wa Algeria Riyad Mahrez ameweka rekodi ya kuwa staa aliyefunga bao la mapema zaidi. Mahrez alifunga bao hilo sekunde ya 81 ya mchezo, ambao Algeria waliibuka na ushindi wa mabao 3-0. Katika mchezo huo, Mahrez alifunga mabao 2 na kuifanya Algeria, iingie kwenye rekodi ya kufunga mabao 100 ya mashindano ya AFCON.
SOMA HII ZAIDI: Afcon 2025: Hawa hapa wachezaji 10 wanaolipwa pesa nyingi
Alex Iwobi kinara wa asisti

Nyota wa kikosi cha Nigeria, Iwobi ameingia katika vitabu vya rekodi vya mashindano ya AFCON 2025. Hii ni baada ya kuandikisha asisti 2 katika mchezo wao dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania. Katika mchezo huo, Nigeria waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Hitimisho
AFCON 2025 Matchday 1 imemalizika kwa kishindo huku mataifa makubwa kisoka yakianza vizuri kwa matokeo ya ushindi. Rekodi nyingi zimeandikwa katika michezo 12 ya kwanza. Hatua ya mzunguko wa pili imeanza rasmi leo Ijumaa Desemba 26, na kila timu sasa inaingia katika vita mpya ya rekodi.

