- JKT Tanzania 1-2 Simba SC matokeo ya mchezo wa NBC Premier League Novemba 8,2025 Uwanja wa Meja Isahmuyo.
- Wilson Nangu ametwaa tuzo ya mchezaji bora mbele ya waajiri wake wa zamani.
- Dimitar Pantev mchezo wa kwanza wa ligi baada ya kurithi mikoba ya Fadlu Davids.
JKT Tanzania 1-2 Simba SC NBC Premier League 2025/26 matokeo rasmi kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Meja Jeneral Isamuyo Novemba 8,2025. Wenyeji JKT Tanzania walitangulia kupata goli dakika ya 60 kupitia kwa Edward Songo likasawazishwa na Wilson Nangu dakika ya 64. Mnyama alichukua pointi tatu ugenini.
SOMA HII: Simba SC vs JKT Tanzania Novemba 8,2025
Vuna mamilioni sasa hivi na SportPesa
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

JKT Tanzania 1-2 Simba SC NBC Premier League 2025/26 kazi ilikuwa nzito

Wakati matokeo yakiwaJKT Tanzania 1-2 Simba SC NBC Premier League 2025/26 kazi ilikuwa nzito kwa timu zote mbili. Mchezo huo dakika 45 za mwanzo hakukuwa na timu iliyopata goli. Simba SC walifanya majaribio mawili kupitia kwa Joshua Mutale na Kibu Dennis yaliokolewa na mlinda mlango wa JKT Tanzania Omar Gonzo.
Mlinda mlango wa Simba SC Yakoub Suleman aliokota nyavuni mpira dakika ya 60 uliokwamishwa na Songo. Iliwachukua Simba SC dakika 4 kuweka usawa kupitia Nangu. Jonathan Sowah alianzia benchi kwenye mchezo huo alipachika bao la ushindi dakika ya 76 likipeleka pointi tatu unyamani.
Ni mchezo wa kwanza kwa Meneja Mkuu wa Simba SC Dimitar Pantev kwenye ligi baada ya kuchukua mikoba ya Fadlu Davids. Kwenye mchezo huo alianza na mshambuliaji mmoja Steven Mukwala. Mabadiliko ya kipindi cha pili alipoingia Abraham Morice, Jean Ahoua, Ellie Mpanzu na Jonathan Sowah yalibadilisha ari ya mchezo.
Tuzo ya mchezaji bora ameibeba beki Nangu
Nangu alichaguliwa kuwa mchezaji bora katika mchezo huo. Beki huyo alifunga goli la usawa kwa Simba SC dakika ya 64. Licha ya kufunga alifanya kazi kubwa katika kuhakisha timu inalinda ushindi.
Kazi nyingine ambayo alipewa ilikuwa ni kupiga faulo na kurusha mipira. Miongoni mwa faulo ambazo alipiga ilikuwa dakika ya 14, 15,16 kipindi cha kwanza. Alisajiliwa na Simba SC akitokea JKT Tanzania hivyo alifunga mbele ya waajiri wake wa zamani.
Nangu amesema: “Tulikuwa tunahitaji pointi tatu muhimu kwenye mchezo wetu. Sikupanga kushangilia nikifunga lakini ilitokea kwa kuwa sikutarajia. Mchezo ulikuwa mgumu tunamshukuru Mungu kupata pointi tatu muhimu,”.
SOMA HII: Mechi za Simba SC 2025/26 CAF Champions League, NBC Premier League

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

1.Simba SC pointi 9, mechi 3
2.Pamba Jiji pointi 9, mechi 6
3.Mbeya City pointi 8, mechi 6
4.Mashujaa FC pointi 8, mechi 6
5.Yanga SC pointi 7, mechi 3
6.Singida Black Stars pointi 7 mechi 3
7.JKT Tanzania pointi 7, mechi 6.
Kikosi cha JKT Tanzania kilichoanza dhidi ya Simba SC
Gonzo
Wahabi
Msengi
Pascal
Roony
Sospeter Bajana
Hassan Nassoro
Kilemile
Najimu Mussa
Paul
Hassan Dilunga
Wachezaji wa akiba
Joseph
Kapalata
Gamba
Said Ndemla
Edward Songo
Makame
Elia
Salum
Abel
Kikosi cha Simba SC kilichoanza dhidi ya JKT Tanzania

Mlinda mlango
Yakoub Suleman
Mabeki
Shomari Kapombe
Athony Mligo
Wilson Nangu
Rushine De Reuck
Viungo
Yusuph Kagoma
Kibu Dennis
Naby Camara
Neo Maema
Joshua Mutale
Mshambuliaji
Steven Mukwala
Wachezaji wa akiba
Hussen Abel
Duchu
Chamou
Kante
Mzamiru Yassin
Ellie Mpanzu
Jonathan Sowah
Seleman Mwalimu
Jean Ahoua
Abraham Morice
SOMA HII: JKT Tanzania FC Vs Simba SC 5/5/2025 : Mabosi Simba wafanya kikao kizito cha Ubaya ubwela

Hitimisho
JKT Tanzania 1-2 Simba SC NBC Premier League 2025/26 pointi tatu zinaipeleka Simba SC kuongoza msimamo wa ligi. Songo anakuwa mchezaji wa kwanza kumfunga mnyama msimu wa 2025/26. Kwenye mechi mbili walizochezwa walikuw hawajaruhusu goli.

