Simba SC vs JKT Tanzania Novemba 8,2025 NBC Premier League/ Live score, H2H, lineups

ByLunyamadizo Mlyuka

November 7, 2025
Simba SC vs JKT TanzaniaMorice AMorice A
  • NBC Premier League msimu wa 2025/26 mechi zote za moto kutokana na ushindani uliopo.
  • Simba SC vs JKT Tanzania Novemba 8,2025 itachezwa saa 1:00 usiku Uwanja wa Meja Isahmuyo.
  • Wajeda niwagumu katika kupoteza mechi zao ndani ya ligi.

Simba SC vs JKT Tanzania ni ratiba ya mchezo ujao kwenye NBC Premier League. Saa 1:00 usiku itachezwa kwenye Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo. Mara ya mwisho wababe hawa walipokutana hapo, mnyama alipata ushindi wa goli moja lililofungwa na Fabrince Ngoma.

SOMA HII: Mechi za Simba SC 2025/26 CAF Champions League, NBC Premier League ni moto| Matokeo na wafungaji

Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

image

Simba SC vs JKT Tanzania utakuwa mchezo wa aina gani?

Simba SC vs JKT Tanzania
Kagoma Yusuph kiungo wa Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Mafahari wawili Simba SC vs JKT Tanzania wanapokutana huwa unakuwa mchezo wenye matumizi makubwa ya nguvu. Mnyama chini ya meneja Dimitar Pantev hupendelea mpira wa pasi nyingi. Wajeda chini ya Kocha Mkuu, Ahmed Ally wao hupendelea mpira wa kasi na kujilinda.

Katika msimamo JKT Tanzania ipo nafasi ya 5 bada ya mechi 5. Ushindi ni kwenye mechi moja na sare mechi 4. Hii inatoa taswira kuwa wapo imara katika eneo la ulinzi.

Upande wa Simba SC ni nafasi ya 7 pointi 6 baada ya mechi mbili. Katika eneo la ulinzi, haijaruhusu goli la kufungwa. Safu ya ushambuliaji imefunga magoli 6.

H2H

05/5/2025, JKT Tanzania 0-1 Simba SC

24/12/2024, Simba SC 1-0 JKT Tanzania

28/05/2024, Simba SC 2-0 JKT Tanzania

15/02/2024, JKT Tanzania 0-1 Simba SC

01/03/2021, Simba SC 3-0 JKT Tanzania

04/10/2020, JKT Tanzania 0-4 Simba SC

7/02/2020, Simba SC 0-1 JKT Tanzania

SOMA HII: Yanga SC vs Simba SC Septemba 16 Uwanja wa Mkapa | Takwimu, matokeo, H2H

image

Utabiri wa matokeo ya mchezo

Simba SC imekuwa na rekodi ya kupata matokeo inapokutana na JKT Tanzania. Katika mechi 7, wajeda walipata nafasi kufunga goli moja pekee. Nafasi kubwa ya ushindi anapewa mnyama.

Mechi 7 walizokutana, ushindi kwa JKT Tanzania ni mara moja. Mnyama alipata ushindi katika mechi 6. Magoli yalifungwa 13, katika hayo safu ya ushambuliaji ya Simba SC ilifunga magoli 12 na ile ya JKT Tanzania 1.

Licha ya kupewa nafasi kubwa ya kupata matokeo bado JKT Tanzania sio mpinzani mwepesi. Timu hiyo ni imara katika kujilinda kwenye mechi zake inazocheza. Dakika 90 zitaamua nani atavuna pointi tatu.

Kikosi cha JKT Tanzania kinachotarajiwa kuanza vs Simba SC

Ahmed Ally
Ahmed Ally, Kocha Mkuu wa JKT Tanzania. Source: JKT Tanzania.

Ramadhani Chalamanda, Hassan Dilunga, Abdulahim Bausi, Mohamed Bakari, David Bryson, Salehe Karabanka, Laurian Makame, Salum Khamis, Pascal Mussa, Ally Msengi na Paul Peter.

Mlinda mlango

Yakoub Suleman

Mabeki

Chamou

Mligo

David Kameta

De Reuck

Viungo

Yusuph Kagoma

Joshua Mutale

Ellie Mpanzu

Morice Abraham

Jean Ahoua

Mshambuliaji

Jonathan Sowah

Matokeo ya mechi 5 zilizopita JKT Tanzania kwenye ligi

Oktoba 24,2025 Mbeya City 2-2 JKT Tanzania
Oktoba 19,2025, JKT Tanzania 1-1 Namungo FC
Oktoba Mosi, JKT Tanzania 1-1 Azam FC
Septemba 22,2025 Coastal Union 1-2 JKT Tanzania
Septemba 18,2925, Mashuja FC 1-1 JKT Tanzania


SOMA HII: Simba SC 0-0 Nsingizini Hotspurs CAF Champions League Oktoba 26, 2025 | Highlights, aggregate 3-0, live score

image

Matokeo ya mechi 5 zilizopita Simba SC

Rushine (-)
Rushine beki wa Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Oktoba 26,2025 Simba SC 0-0 Nsingizini Hotspurs. Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nsingizini Hotspurs 0- 3 Simba SC, Oktoba 19,2025. Ligi ya Mabingwa Afrika.

Oktoba Mosi 2025, Simba SC 3-0 Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Septemba 28 2025, Simba SC 1-1 Gaborone United, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Septemba 25 2025, Simba SC 3-0 Fountain Gate mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Hitimisho

Simba SC vs JKT Tanzania ni mchezo unaotarajiwa kutokuwa na magoli mengi kutokana na aina ya mbinu za wapinzani. JKT Tanzania wamekuwa wakijilinda huku Simba SC wakishambulia kwa kushtukiza. Licha ya mnyama kuwa na rekodi yakupata ushindi wa magoli 4-0 bado mchezo unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili.

Share this: