Yanga SC vs Silver Strikers CAFPacome vs Silver Strikers
  • Yanga SC 0-1 Silver Strikers CAF Champions League ushindi wa kwanza kwa wenyeji kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Bingu-Malawi.
  • Goli la kwanza limefungwa na Andulu Yosefe aliyekuwa ndani ya 18 kwa kumchagulia upande uliomshinda Djigui Diarra.
  • Yanga SC wanakibarua cha kupata ushindi wa angalau magoli 2-0 mchezo ujao Uwanja wa Mkapa, Oktoba 25.

Yanga SC 0-1 Silver Strikers CAF Champions League ni matokeo rasmi katika mchezo wa kwanza, Uwanja wa Bingu. Goli la ushindi limefungwa dakika ya 76 na Andulu Yosefe. Unakuwa ni ushindi wanne kwa Silver Strikers wakiwa nyumbani hivyo wamendeleza ubabe wao. Bado mchezo mmoja wa maamuzi utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 25 na Yanga SC wakitakiwa kupata ushindi wa angalau magoli 2-0 ili kutinga hatua ya makundi.

SOMA HII: Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League 2025| Lineup, H2H
Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

image

Yanga SC 0-1 Silver Strikers CAF Champions League goli limefungwaje?

Yanga SC 0-1 Silver Strikers CAF Champions League
Yanga SC vs Silver Strikers ugenini Oktoba 18 2025. Source: Yanga SC.

Yanga SC 0-1 Silver Strikers CAF Champions League goli lilifungwa kipindi cha pili. Katika dakika 45 za mwanzo hakukuwa na timu iliyoona lango la mpinzani. Wenyeji walilazimika kusubiri mpaka dakika ya 76 kupata goli la kuongoza.

Mpira ulianza kwa mlinda Chikoka George aliyepiga pasi ndefu. Uchizi vunga aliweka pasi ya kupenyeza ndani ya 18 ikapenya kwa walinzi wa Yanga SC. Ernest alitoa pasi ya goli kwa Andulu Yosefe ambaye aliwaadhibu Yanga SC kwa kumfunga mlinda mlango namba moja Djigui Diarra.

Kikosi cha Yanga SC dhidi ya Silver Strikers

Kipa

Djigui Diarra

Mabeki

Israel Mwenda

Boka

Dickson Job

Ibrahim Bacca

Viungo

Maxi Nzengeli

Mudathir Yahya

Mo Doumbia

Pacome

Aziz

Mshambuliaji

Boyeli

Wachezaji wa akiba

Mshery

 Nondo

Zimbwe

Duke

 Ecua

Balla

 Edmund

 Dube

SOMA HII: Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League | H2H, takwimu muhimu, utabiri

image

Mechi 6 za Yanga SC zilizopita

Yanga Tena
Mshambuliaji wa Yanga SC, Prince Dube kwenye mchezo wa kimataifa. Source: Yanga SC.

Septemba 16, 2025 – Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii).

Septemba 19, 2025 – Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika

Septemba 24,2025 – Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).

Oktoba 27,2025 -Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).

Septemba 30,2025, Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).

Oktoba 18, 2025, Silver Strikers 1-0 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika)

 Mechi 6 za Silver Strikers zilizopita

Yanga CAF
Yanga SC vs Silvers Strikers, Malawi. Source: Yanga SC.

Shire FC 1-4 Silver Strikers, Septemba 11 2025 Malawi Cup

Elgeco Plus 1-1 Silver Strikers, Septemba 21 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Silver Strikers 0-0 Elgeco Plus Septemba 27 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Blue Eagles 0-3 Silver Strikers Oktoba 2 2025, Malawi Cup.

Bullets 2-1 Silver Strikers Oktoba 5 2025, Malawi Cup.

Oktoba 18, 2025, Silver Strikers 1-0 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika)

SOMA HII: Matokeo ya Yanga SC 2025/26 | Wafungaji, magoli, ratiba ya mechi zijazo

image

H2H

Silver Strikers FC 1-0 Yanga SC CAF Champions League, Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu, Malawi.

Yanga SC vs Silver Strikers FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 25, 2025.

Mchezo wa kwanza Yanga SC kupoteza

Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza Yanga SC kupoteza msimu wa 2025/26. Chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz katika mechi sita zilizopita haikupoteza. Joto ya kupoteza Romain anaipata leo ugenini katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hitimisho

Yanga SC 0-1 Silver Strikers CAF Champions League matokeo ya raundi ya kwanza. Mchezo wa pili utaamua mshindi wa jumla atakayekata tiketi hatua ya makundi. Je nani atatinga hatua inayofuata?

Share this: