Seleman Mwalimu Simba SCSeleman Mwalimu Simba SC
  • Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League wanakutana kwa mara ya kwanza 2025/26.
  • Moussa Camara, Mohamed Bajaber, Kante wachezaji muhimu wa Simba SC kukosekana kwenye mchezo ujao.
  • Nsingizini Hotspurs ni mabingwa katika ligi ya Eswatini watawakaribisha Simba SC mabingwa mara 22 Ligi Kuu ya NBC Oktoba 19 2025.

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League ni mechi kali itakayokuwatanisha wababe wawili Jumapili Oktoba 19 2025 Uwanja wa taifa wa Somhlolo. Katika mechi 19 zilizopita kwa Nsingizini Hotspurs ina rekodi yakushinda mechi 14, kupoteza mechi 2 na sare 3. Upande wa mnyama katika mechi 19 zilizopita ilipata ushindi mechi 11, ilipoteza 5 na sare 3.

SOMA HII: Kuelekea Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champion League 2025

Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Hujashinda na kindege cha SportPesa? Leo ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League utabiri

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League
Pantev Meneja Mkuu wa Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Kutokana na upinzani uliopo kila timu ina nafasi yakupata matokeo. Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League utabiri unaonyesha nafasi ya sare ni asilimia 39. AI imeipa ushindi Simba SC asilimia 41 na Nsingizini Hotspurs asilimia 20.

Mechi 6 za Simba SC

Oktoba Mosi 2025, Simba SC 3-0 Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Septemba 28 2025, Simba SC 1-1 Gaborone United, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Septemba 25 2025, Simba SC 3-0 Fountain Gate mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Septemba 20 2025, Gaborone United 0-1 Simba SC, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Septemba 16 2025, Yanga SC 1-0 Simba SC, Ngao ya Jamii.

Septemba 10 2025, Simba SC 2-0 Gor Mahia mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

SOMA HII: Simba SC 1-0 Gaborone United CAF Champion League | Goli la Ellie Mpanzu, kadi nyekundu

image

Mechi 6 za Nsingizini Hotspurs

Nsingizini Hotspurs 1-0 Simba Bhora, ilishinda kwa penalti 4-2, Septemba 28,2025 mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba Bhora 1-0 Nsingizini Hotspurs, Septemba 21 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Black Bulls 1-0 Nsingizini Hotspurs, Septemba 19,2025, mchezo wa kirafiki.

Sidvwashini United 0-5 Nsingizini Hotspurs, Mei 25 2025, mchezo wa MTN Premier League.
Nsingizini Hotspurs 2-1 Rangers Shiselweni, Mei 17 2025, MTN Premier League.

Mbabane Highland FC 2-1 Nsingizini Hotspurs, MTN Premier League, Mei 11 2025.

H2H

Ladack Chasambi
Ladack Chasambi nyota wa kikosi cha Simba SC. Source: Simba SC.

Nsingizini Hotspurs vs Simba SC, Oktoba 19 2025, CAF Champions League.

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs, Oktoba 24,2025, CAF Champions League.

Orodha ya wachezaji wa Simba SC waliosafiri mpaka Eswatini

Makipa

Yakoub Suleiman
Hussen Abel

Mabeki

Shomari Kapombe
David Kameta
Anthony Mligo
Karabou Chamou
Rushine De Reuck
Wilson Nangu
Vedastus Masinde

Viungo
Yusuph Kagoma
Mzamiru Yassin
Naby Camara
Joshua Mutale
Kibu Dennis
Elie Mpanzu
Ladack Chasambi
Jean Ahoua
Neo Maema
Morice Abraham


Washambuliaji
Jonathan Sowah
Steven Mukwala
Seleman Mwalimu

SOMA HII: Kocha Fadlu Davis kuondoka Simba SC? Utata waibuka! Simba watoa tamko hili

image

Wachezaji watakaokosekana

Camara wa Simba SC
Moussa Camara kipa namba moja wa Simba SC. Source: Simba SC.

Kwa upande wa Simba SC wachezaji muhimu wanne watakosekana. Moussa Camara kipa namba moja. Hamza Jr ambaye ni beki, Mohamed Bajaber huyu ni kiungo na Allasane Kante kiungo mkabaji.

Sababu kubwa za wachezaji hawa kukosekana ni kutokuwa fiti. Camara alipata maumivu mchezo dhidi ya Gaborone United, Uwanja wa Mkapa. Kante inatajwa kuwa kwenye uwanja wa mazoezi alipata maumivu.

Hitimisho

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League timu zote ni ngumu licha ya Simba SC kupewa nafasi kubwa kushinda. Simba Bhora ya Zimbabwe iliondolewa na Nsingizini Hotspurs je Simba SC kutoka Tanzania itahimili vishindo?

Shinda mamilioni kwa kucheza Supa Jackpot 17, bofya hapa chini

image

Share this: