- Ligi Kuu ya England inaendelea tena wikiendi hii kwa msisimko mkubwa.
- Hii ni kuelekea mechi kali ya Liverpool vs Manchester United kwenye Uwanja wa Anfield.
- h2h timu hizi zimekutana katika mechi 66, Man United wameshinda mechi 28. Liverpool wameshinda mechi 25, huku michezo 13 ikiisha kwa matokeo ya sare.
Wikiendi hii ni ya moto pale Ligi Kuu soka England, maarufu EPL. Ipo michezo mingi, lakini mchezo unaotupiwa jicho zaidi ni ule wa Liverpool ambao wataikaribisha Manchester United Jumapili. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Anfield. Kila timu inaonekana kujidhatiti kusaka ushindi na makala hii inagusia taarifa muhimu za mchezo huo.
SOMA HII PIA: Manchester United vs Liverpool – A Title-Defining Premier League Saga
Ushindi mzito wa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

H2H Liverpool vs Manchester United

Timu hizi zimekutana katika mechi 66, ambapo Man United wamekuwa na wakati mzuri zaidi wakishinda mechi 28. Liverpool wao wameshinda mechi 25, huku michezo 13 ikiisha kwa matokeo ya sare. Hii inatoa taswira ya ushindani mkali, pale timu hizi zinapokutana.
SOMA HII ZAIDI: Liverpool vs Man United: Preview, Prediction & Team News
Mechi 5 zilizopita za Liverpool
4 Oct Chelsea 2-1 Liverpool
30 Sep Galatasaray1-0 Liverpool
27 Sep Crystal Palace 2-1 Liverpool
23 Sep Liverpool 2-1 Southampton
20 Sep Liverpool 2-1 Everton
Mechi 5 zilizopita za Manchester United
4 Oct Manchester United 2-0 Sunderland
27 Sep Brentford 3-1 Manchester United
20 Sep Manchester United 2-1 Chelsea
14 Sep Manchester City 3-0 Manchester United
30 Aug Manchester United 3-2 Burnley
Kikosi cha Liverpool kinachotarajiwa kucheza dhidi ya Manchester United

Kipa: Mamardashvili
Mabeki: Frimpong, Konaté, Van Dijk, Kerkez
Viungo wa kati: Gravenberch, Szoboszlai
Washambuliaji: Salah, Wirtz, Ekitike, Isak
Kikosi cha Manchester United kinachotarajiwa kucheza dhidi ya Liverpool

Kipa: Lammens
Mabeki: Yoro, De Ligt, Shaw
Wing‑backs: Dalot, Dorgu
Viungo wa kati: Casemiro, Fernandes
Washambuliaji: Mbeumo, Cunha, Sesko
Habari za timu zote kwa ujumla
Arne Slot anakabiliwa na maamuzi magumu kutokana na majeruhi, wakati huu anapojaribu kuirudisha timu yake kwenye fomu. Hii ni baada ya kushuhudia wakipoteza michezo mitatu mfululizo katika mashindano yote. Hali ambayo imezua minong’ono mingi kutokana na ulinganifu wa usajili wao.
Ruben Amorim wa Manchester United, hatimaye angalau anaonekana kuwa na kikosi kilicho imara. Hii ni baada ya kushinda mechi mbili kati ya tatu za mwisho. Faida kwake ni kuwa na machaguo mengi hasa kwenye upande wa ushambuliaji.
Kutokan ana jeraha la kipa, Alisson kuna uwezekano mkuba wa kipa Giorgi Mamardashvili kuanza. Kipa huyu ameonyesha kuaminika na anaonekana ni kipa mbadala bora.
Liverpool inahitaji kumtumia zaidi, Mohamed Salah kusababisha madhara. Nyota huyo amekuwa na wastani mzuri wa kuifunga United. Staa wao mpya, Florian Wirtz ameonekana bora akiicheza katikati zaidi kuliko kushoto.
Kwa Manchester United, Senne Lammens alionesha kujiamini katika debuti yake dhidi ya Sunderland. Anaonekana kuwa imara na kuaminika katika lango. Kuna uwezekano mkubwa Amad Diallo atapoteza nafasi ya kuanza kikosini.
Amorim ana jambo lake na Ugarte

Kocha mkuu wa Manchester United, Ruben Amorim, anaripotiwa kuwa anafikiria kwa umakini kuanza na, Manuel Ugarte katika mechi dhidi ya Liverpool. Ikumbukwe kuwa Ugarte ameanza mara mbili pekee kwenye Ligi Kuu msimu huu, alipopewa nafasi ya kuanza dhidi ya Manchester City. Kumbukumbu mbaya kwake, ni pale United ilipopoteza mechi zote hizo mbili.
Gazeti la The Sun limeripoti kuwa, Amorim anafikiria kumrejesha Ugarte kikosini dhidi ya Liverpool. Hii ni kutokana na Casemiro kucheza mechi nyingi akiwa na Brazil, wakati wa mapumziko ya kimataifa ya mwezi Oktoba. Kwa upande mwingine, Ugarte hakucheza mechi yoyote kwa ajili ya Uruguay dhidi ya Jamhuri ya Dominika na Uzbekistan.
Casemiro hakushiriki mazoezi ya Man United siku ya Alhamisi, kwani alipewa muda wa ziada kupumzika. Hali ambayo pia ilitokea kwa Bruno Fernandes ambaye naye aliitumikia Ureno. Licha ya yote inatarajiwa kuwa Fernandes ataanza Anfield.
SOMA HII PIA: Man United vs Liverpool – A Deep Dive into the Heart of Rivalry
Hitimisho:
Liverpool vs Manchester United haujawahi kuwa mchezo rahisi. Timu hizi zina upinzani mkali ndani na nje ya uwanja, hii inaweza kuthibitishwa na rekodi ya matokeo wanapokutana. Hivyo inatarajiwa mchezo huu wa Jumapili, utakuwa wa kuvutia na vita halisi ya dakika 90 pale Anfield.

