Ibrahim BaccaIbrahim Bacca
  • Beki wa Yanga SC Ibrahim Bacca amefungiwa mechi 5 na TPLB.
  • Bacca atakosekana kwenye Kariakoo Dabi kati ya Yanga SC vs Simba SC
  • Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) wamemfungia beki huyu.

Beki wa Yanga SC Ibrahim Bacca atakosekana kwenye Dabi hii Yanga SC vs Simba SC. Hii ni mojawapo ya kati ya michezo mitano ambayo atakosa baada ya kuadhibiwa na TPLB. Bacca ambaye ni askari alicheza rafu dhidi ya beki wa Mbeya City Ibrahim Ame. Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) wamempa adhabu mchezaji huyu wa Yanga SC kwa utovu wa nidhamu.

SOMA HII: Yanga SC 2-0 Simba SC mchezo wa Kariakoo Dabi/ Bingwa 2024/25/ Pacome balaa

Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

Ni sasa hivi unavuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa. Ni rahisi sana hasa ukizingatia Marubani wapo makini. Cheza Aviator upate mgao wako.

image

Je nani kuvaa viatu vya Ibrahim Bacca?

Bacca kukosekana Yanga SC vs Simba SC
Ibrahim Bacca beki wa Yanga SC akiwa na wachezaji wenzake Prince Dube jezi namba 29 na nahodha Bakari Nondo. Source: Yanga SC.

Kutokana na adhabu Ibrahim Bacca hatacheza mchezo wa Yanga SC vs Simba SC jambo ambalo litapangua kikosi hicho kwenye safu ya ulinzi. Kwenye mechi ya Ngao ya Jamii iliyochezwa Uwanja wa Mkapa alianza kikosi cha kwanza. Kuna uwezekano Dickson Job na Bakari Nondo wakiwa fiti wakaunda safu ya ulinzi.

Miongoni mwa wachezaji wazawa wanaopiga kazi mwanzo mwisho ni Bacca. Rekodi zinaonyesha 2024/25 beki huyo alicheza mechi 23 kati ya 30 za ligi. Alitumia dakika1,883 akifunga magoli 5.

Zijue mechi atakazokosekana Bacca

Bacca ----
Bacca msimu wa 2024/25 alifunga magoli 5 kwenye mechi za ligi. Source: Yanga SC.

Yanga SC vs Mtibwa Sugar, Oktoba 29 2025, Uwanja wa KMC, Complex.

Yanga SC vs KMC FC, Novemba 4 2025, Uwanja wa KMC Complex.

Coastal Union vs Yanga SC, Desemba 10 2025, Uwanja wa Mkwakwani.

Yanga SC vs Dodoma Jiji FC, Uwanja wa KMC Complex, Februari 18 2026.

SOMA HII: Yanga SC 2-0 JKT Tanzania; Yanga yatinga Fainali Shirikisho CRDB yawasubiri Simba/Singida BS

image

Sababu ya Bacca kukosekana katika mechi 5

Bacca Vibe
Bacca beki wa Yanga SC atakosekana katika mechi tano za Ligi Kuu ya NBC. Source: Yanga SC.

Sababu kubwa ya kuukosa mchezo dhidi ya Simba SC na michezo mingine ni adhabu ya mechi tano ambazo amefungiwa. Rungu hilo limetoka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB). Kosa la kumchezea faulo Ibrahim Ame limemhukumu kwa kipigo hicho.

Ibrahim Bacca alifanya kosa hilo kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City. Huo ulikuwa mchezo nambari 22, ambao ulifanyika katika Uwanja wa Sokoine.

Sio Ibrahim Bacca pekee mwamuzi Mdoe yupo kwenye kifungo

Mbali na Bacca, mwamuzi Omary Mdoe kutoka Tanga ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa mizunguko mitano. Adhabu hiyo ilitolewa Oktoba 3 2025.  Sababu ya kuondolewa ni kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira na kukosa kuchukua hatua kwa ukiukwaji.

Dakika 3 ya mchezo mwamuzi Mdoe alishindwa kuchukua hatua baada ya Ame kuchezewa faulo na Ibrahim Bacca. Licha ya hili, alishindwa kutafsri sheria dakika ya 46  ambapo mchezaji wa Mbeya City FC, Matheo Anthony alishika mpira ndani ya eneo la penati. Msululu huu wa maamuzi yasiyofaa yamepindukia kukua adhabu kwake.

SOMA HII: Mechi ya Tanzania Prisons vs Yanga SC itawaka Juni 18 2025 live, uchanganuzi, H2H | Kutawaka Mbeya na Aucho awashtua!

image

Hitimisho

Beki wa Yanga SC Ibrahim Bacca atakosekana kwenye mechi ya Yanga SC vs Simba SC kupitia hili benchi la ufundi huenda likabadilisha aina ya mfumo wao wa kucheza benchi. Bacca atarejea kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars baada ya marufuku hii.

image
Share this: