Stars kikosiStars kikosi
  • Fashion Sakala nyota wa timu ya taifa ya Zambia alifunga goli pekee la ushindi kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  • Tanzania 0-1Zambia FIFA World Cup Qualifier 2026 matokeo yasiyofurahisha kwa Watanzania, kichezo Zambia.
  • Vijue vikosi vya timu zote mbili kwenye mchezo huo wa Kundi E Oktoba 8 2025.

Tanzania 0-1 Zambia FIFA World Cup Qualifier 2026 yamezima ndoto za Watanzania kushuhudia wapambanaji wakifuzu hatua hiyo kubwa. Timu hizi zipo kundi E linaongozwa na timu ya taifa ya Morocco. Ni dakika 90 zilizokuwa na purukushani kubwa na matumizi ya nguvu nyingi. Hilo lilisababisha kuwa na jumla ya faulo 28 na kadi 5 za njano zikitolewa Oktoba 8 2025.

SOMA HII: CHAN 2024: Tanzania kuikabili Madagascar leo Agosti 9 2025/ Matokeo, vikosi, utabiri

image

Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

Ni sasa hivi unavuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa. Ni rahisi sana hasa ukizingatia Marubani wapo makini. Cheza Aviator upate mgao wako.

 Tanzania 0-1 Zambia goli lilifungwa kipindi cha pili

Tanzania 0-1 Zambia FIFA World Cup Qualifier
Timu ya taifa ya Zambia imepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Tanzania. Source: MWN

Mchezo wa kundi E ulichezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Tanzania 0-1 Zambia FIFA World Cup Qualifier 2026 goli la ushindi likifungwa kipindi cha pili. Mfungaji ni Fashion Sakala dakika ya 75 akitumia pasi ya Lubambo Musonda.

Goli la Zambia linaamnisha nini kwa Taifa Stars?

Hemed Morocco
Hemed Morocco Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania, Taifa Stars.

Goli hilo liliwawapa Zambia nafasi ya kuongoza lilidumu mpaka mwisho wa mchezo. Katika dakika 45 za mwanzo hakuna timu ambayo ilipata goli. Hivyo Tanzania imeangusha pointi tatu muhimu ikiwa nyumbani.

Kupoteza kwa Tanzania kunazima matumaini ya kupata tiketi kufuzu Kombe la Dunia 2026. Kwenye mchezo huo Zambia ilikuwa na umiliki asilimia 54 ilipiga jumla ya mashuti 11 huku 4 yakilenga lango. Tanzania ni mashuti 7 ilipiga ni mashuti 2 yalilenga lango huku wakicheza faulo 15 na Zambia faulo 13.

Zambia ina mchezo mmoja mkononi dhidi ya Niger ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa katika hatua ha makundi. Zambia ina pointi 9 inakutana na Niger yenye pointi 12. Ikiwa itapata ushindi itafikisha pointi 12.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Levy Mwanawasa Oktoba 12 2025. Morocco tayari wamekata tiketi ya kufuzu baada ya kuongoza kundi. Matokeo ya mchezo wa Zambia na Niger yataamua nani atakuwa nafasi ya pili.

Wajue wachezaji walioonyeshwa kadi za njano

Feisal kwenye majukumu Stars
Feisal nyota wa timu ya Tanzania, Taifa Stars.

Kwenye mchezo huo jumla ya kadi tano za njano zilitolewa na mwamuzi wa kati Ibrahim Traoreh. Tanzania ni wachezaji watatu wakionyeshwa kadi. Wawili walionyeshwa wa timu ya taifa ya Zambia.

Bakari Mwamnyeto dakika ya 56, Yahya Omary dakika ya 30 na kiungo Feisal Salum dakika ya 33 walionyeshwa kadi za njano kwa upande wa Tanzania. Lawarence Mulega dakika ya 89 na Benson Sakala dakika ya 78 walionyeshwa kadi kwa upande wa timu ya Zambia. Sababu kubwa ni kucheza faulo kwa wapinzani.

SOMA HII: Mauritania 0-1 Tanzania CHAN 2024 Kapombe shujaa/ Magoli, takwimu/ Robo fainali yanukia

image

Kikosi cha Tanzania vs Zambia

Yakoub Suleiman

 Ibrahim Bacca

 Bakari Mwamnyeto

 Pascal Msindo

 Israel Mwenda

 Khalid Habibu

 Yahya Omary

 Feisal Salum

 Charles M’Mombwa

 Abdul Sopu

Paul Peter

Wachezaji wa akiba

Yusuph Kagoma

 Lameck Lawi

 Hussen Masalanga

 Miano Danilo

 Zuber Masudi

Kikosi cha Zambia vs Tanzania kilichoanza

Lawrence Mulenga

 Kabaso Chongo

 Benson Sakala

 Kennedy Musonda

 Gift Mphande

 Kelvin Kapumbu

 Obino Chisala

 Fashion Sakala

 Kelvin Kampamba

 Kings Kangwa

Daka Patson

Wachezaji wa akiba

Frankie Musonda

 Mathew Banda

 Joseph Sabobo

 Gift Siame

 Charles Kalumba

 Patrick Chooma

 Clatous Chama

 Dominic Chanda.

Msimamo Kundi E

TimuMechiPointi
1.Morocco721
2.Niger712
3.Tanzania810
4.Zambia79
  5.Congo 71
 6.Eritrea00

Hitimisho

Tanzania 0-1 Zambia FIFA World Cup Qualifier 2026 ulikuwa ni mchezo uliobeba matumaini kwa Watanzania kufuzu hatua inayofuata. Kutokana na kupoteza pointi tatu milango imefungwa kutoka kundi E. Mchezo wa mwisho kwa Zambia na Niger utampata atakayekuwa nafasi ya pili ya msimamo wa kundi.

image
Share this: