- Matokeo kwenye mechi 6 ambazo aliziongoza ndani ya msimu wa 2025/26 ni ushindi katika mechi 5, suluhu mchezo mmoja dhidi ya Mbeya City.
- Romain Folz kuondoka Yanga SC ukweli umebainishwa na uongozi wa timu hiyo yenye maskani yake Jangwani.
- CV ya Folz ni kubwa kutokana na kufundisha timu mbalimbali Afrika kwa nyakati tofauti.
Romain Folz kuondoka Yanga SC umekuwa mjadala mkubwa mara baada ya kuangusha pointi mbili dhidi ya Mbeya City kwa ubao kusoma 0-0. Tetesi zimekuwa zikieleza kwamba mrithi huyo wa mikoba ya Miloud Hamdi amekalia kuti kavu. Uongozi umebainisha ukweli kupitia kwa Ofisa Habari Ali Kamwe ambaye ameweka wazi kuwa Folz bado yupo kwenye majukumu yake.
SOMA HII: Romain Folz kocha mpya Yanga SC mwenye CV kubwa | Wachezaji wenye uhakika 2025/26
Paisha Kindege cha SportPesa uvune mkwanja
Muda ni sasa kupaisha Kindege cha SportPesa na kuvuna mkwanja. Ni rahisi kweli, usiache kuwa hewani mara baada ya kusoma makala haya. Cheza sasa Aviator upate mgao wako.

Romain Folz kuondoka Yanga SC, mechi tatu zatajwa

Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC ipo mzunguko wa kwanza 2025/26. Yanga SC ni mabingwa watetezi wakiwa wameshuka uwanjani mara mbili. Romain Folz kuondoka Yanga SC inatajwa anafuatiliwa mwendo kwenye mechi tatu. Katika hizo mbili ni Ligi ya Mabingwa Afrika na moja ni ligi ya NBC.
Taarifa zinaeleza kuwa kuna asilimia ndogo kwa kocha huyo kubaki Jangwani. Ikiwa kutakuwa na mabadiliko katika uchezaji basi ataendelea kubaki. Mechi yake ya tatu Yanga SC itakuwa nyumbani, Oktoba 29 2025.
Katika mechi hizo tatu Yanga SC watacheza mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers ya Malawi. Mchezo wa kwanza itakuwa ugenini Malawi kati ya tarehe 17-19 na ule wa marudiano utapigwa nyumbani kati ya tarehe 24-26. Mshindi wa jumla kwenye mechi hizi atatinga hatua ya makundi.
Mchezo mmoja ni wa ligi ya NBC itakuwa dhidi ya Mtibwa Sugar. Huu unatarajiwa kuchezwa Oktoba 29 2025 Uwanja wa Mkapa katika msako wa pointi tatu muhimu. Tetesi zinaeleza kuwa matokeo ya mchezo yataamua hatma ya kocha huyo.
SOMA HII: Yanga SC wiki ya wananchi ni Ijumaa Septemba 12

Matokeo ya mechi sita za Romain Folz Yanga SC

Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki)
Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii).
Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).
Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).
CV ya Romain Folz
Romain Folz mwenye miaka 35 alizaliwa Bordeaux, Ufaransa. 2025 alikuwa mkurugenzi wa michezo wa Olympique Akbou ya Algeria. 2024 alikuwa kocha msaidizi wa Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini.
2023 alikuwa Kocha Mkuu wa Horoya ya Guinea. 2022 alikuwa Kocha Mkuu wa Amazulu ya Afrika ya Kusini. 2021 alikuwa Kocha Mkuu wa Township Rollers ya Botswana. 2019 alikuwa kocha msaidizi wa Pyramid ya Misri. 2018 alikuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uganda. Ana UEFA Pro Licence na Pro Licence ya CONMEBOL (America). Ni muumini wa (4-3-3).
SOMA HII: Orodha ya wachezaji waliosajiliwa Yanga SC 2025/26 | Vita yao na Simba SC balaa zito

Ali Kamwe abainisha ukweli kuhusu Romain Folz

Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe kupitia Spoga TV ameweka wazi kuwa hakuna taarifa iliyomfikia mezani kuhusu kocha huyo. Aliongeza kuwa ikiwa taarifa itafika basi mashabiki watajua. Hivyo kwa sasa watambue kwamba bado Romain yupo Yanga SC.
“Romain Folz bado ni Kocha Mkuu wa Yanga SC. Hakuna taarifa ya Romain Folz kusimamishwa kazi. Ingekuwepo hiyo taarifa ningewasilisha, kocha yupo na anaendelea kufanya kazi. Kwa sasa wachezaji wapo mapumziko watarejea kambini Jumatatu kwa maandalizi ya mechi za kimataifa.”
Hitimisho
Baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City, Septemba 30 2025 kocha huyo alibainisha kuwa uwanja haukuwa rafiki. Romain Folz kuondoka Yanga SC atakuwa amefungua msimu wa 2025/26 kuingoza timu hiyo kutwaa Ngao ya Jamii. Kwenye mechi ambazo alikuwa benchi mpaka sasa safu ya ulinzi haijaruhusu goli la kufungwa.


