Romain Folz (-)Romain Folz (-)
  • Kwa mara ya kwanza Wananchi chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz wameangusha pointi ugenini.
  • Yanga SC 0-0 Mbeya City NBC Premier League dakika 90 za ushindani kwa wababe wawili uwanjani.
  • Kibarua cha Folz kigumu kutokana na mwendo wa timu hiyo katika mechi za ushindani.

 Yanga SC 0-0 Mbeya City matokeo haya yanaongeza ugumu kibarua cha Kocha Mkuu wa Jangwani Romain Folz kusalia hapo. Tetesi zinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa kocha huyo ataondoka hivi karibuni. Licha ya kutopoteza mchezo hata mmoja kati ya sita ambayo alikaa benchi baada ya kutambulishwa Yanga SC inaelezzwa mwenendo wake bado haujaeleka kwa mabingwa hao watetezi.

SOMA HII: Yanga SC vs Mbeya City Septemba 30 | H2H, vikosi, takwimu muhimu

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

image

Ni muda wa kushinda milioni sasa hivi ikiwa utapaisha Kindege cha SportPesa. Unachotakiwa kufanya ni rahisi sana paa hewani. Cheza Aviator upate mgao wako.

Yanga SC 0-0 Mbeya City ziliongezwa dakika 9

Yanga SC 0-0 Mbeya City
Pacome alianza kikosi cha kwanza mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine. Source: Yanga SC.

Katika mchezo wa leo Yanga SC 0-0 Mbeya City ziliongezwa jumla ya dakika 9. Katika kipindi cha kwa kwanza ziliongezwa 3 na kipindi cha pili ziliongezwa 6. Licha ya dakika hizo kuongezwa bado milango ilikuwa migumu kwa timu zote.

Romain Folz kibarua chake kigumu

Taarifa zinaelezwa kuwa mabosi wa Yanga SC hawafurahishwi na mwendo wa timu. Katika mechi sita ambazo Folz alikuwa benchi inatajwa kuwa hakukuwa na utulivu kwa wachezaji. Licha ya kwamba kocha ni mgeni kuna fukuto ndani.

Folz wakati wa maandalizi ya mchezo dhidi ya Mbeya City alibainisha kuwa anaheshimu maoni. Kocha huyo aliongeza kuwa anahitaji muda zaidi kuwa na kikosi bora. Mchezo dhidi ya Mbeya City ulikuwa unatajwa kuwa ni wa mwisho kwake. Mchezo wake uliopita ilikuwa dhidi ya Wiliete SC.

Yanga SC yashusha chuma kingine kutoka Ghana
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Romain Folz na Rais wa Yanga SC Injinia Hersi Said. Source: Yanga SC.

“Nadhani tuna kikosi bora sana na kwa sasa tunapambana kufika kwenye ubora wa juu. Ni sawa watu kutoa maoni lakini sisi kama klabu ni lazima tuwe kitu kimoja nyakati hizi tunaposuka kitu kizuri kwa ajili ya timu yetu. Nadhani ndani ya kipindi kifupi kijacho tutakuwa sehemu nzuri sana,” alisema Folz.

SOMA HII: Romain Folz kocha mpya Yanga SC mwenye CV kubwa | Wachezaji wenye uhakika 2025/26

image

 Mechi 6 za Yanga SC vs Mbeya City za ligi

13/02/2021Mbeya City 1-1 Yanga SC
05/02/2022Yanga SC 0-0 Mbeya City
25/06/2022Mbeya City 1-1 Yanga SC
26/11/2022Yanga SC 2-0 Mbeya City
6/6/2023Mbeya City 3-3 Yanga SC  
30/09/2025Mbeya City 0-0 Yanga SC

Sare 5 ushindi mechi 1

Mbeya City wamekuwa na rekodi nzuri katika uwanja wa nyumbani. Kwenye mechi 6 ambazo walikutana na Yanga SC walipata sare 5. Mchezo mmoja walipoteza wakiwa ugenini.Katika sare tano, nne Mbeya City walikuwa nyumbani.

Kikosi cha Yanga SC kilichoanza dhidi ya Mbeya City

Mlinda mlango

Djigui Diarra

Mabeki

Dickson Job

 Chadrack Boka

Israel Mwenda

Ibrahim Bacca

Viungo

 Aziz Andambilwe

 Maxi Nzengeli

 Duke Abuya

Mohamed Doumbia

 Pacome Zouzoua

Mshambuliaji

Andy Boyel

Wachezaji wa akiba

Mo Doumbia
Mo Doumbia kiungo wa kikosi cha Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Balla Conte

Lassine Kouma

Abutwalib Mshery

Ecua Elastin

Mohamed Hussen

Edmund John

Prince Dube

Offen Chikola

Abdulanassir Abdallah

Abubakar Othman

SOMA HII: Usajili wa Yanga SC orodha ya wapya 11 msimu wa 2025/26 | Rekodi, magoli na timu walizotoka

image

Kikosi cha Mbeya City kilichoanza dhidi ya Yanga SC

Mlinda mlango

Beno Kakolanya

Walinzi

Ibrahim Ame

Yahya Mbegu

Mwani Thobias

Gabriel Mwaipola

Viungo

Omary Chibada

Baraka Filemon

 Adilly Buha

Matheo Anthony

Washambuliaji

Vitalisy Mayanga

Eliud Ambokile


Wachezaji wa akiba

Peter Mwalyanzi

Pillar Kelvin

David Mwasa

Stewart Theodory

Daniel Lukandamila

Mukrim Juma

Jonathan Mwaibindi

Riphat Khamis

Malack Joseph

Hashimu Mussa

Hitimisho

Yanga SC 0-0 Mbeya City hii ni sare ya kwanza kwa mabingwa watetezi. Wapinzani hawa katika mechi zao zote wanazokutana huonyeshana ubabe kwelikweli. Katika mchezo wa leo kulikuwa na matumzi makubwa ya nguvu na spidi ndani ya dakika 90 na mwamuzi wa kati alikuwa ni Omary Mdoe.

image
Share this: