- Matokeo ya Yanga SC ni kicheko kwa mashabiki kutokana na mwendo ambao wanakwenda nao kwenye mechi za ushindani.
- Yanga SC 2-0 Wiliete SC CAF Champion League, Waangola wabebeshwa zigo la magoli 5-0 kimataifa
- Romain Folz mbinu zimejibu huku tetesi zikieleza kuwa kocha huyo atafungashiwa virago vyake hivi karibu
Yanga SC 2-0 Wiliete SC CAF Champion League ni ushindi wa pili mfululizo kwenye mashindano makubwa Afrika. Wananchi wanasonga mbele hatua ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika,(CAF). Baada ya kufuzu watakutana na Silver Strikers ya Malawi katika hatua inayofuata anga la kimataifa.
Paisha Kindege cha SportPesa upate mamilioni sasa hivi

Ni muda wakupaisha Kindege cha SportPesa sasa hivi upate mamilioni. Inawezekana kwako rubani bila shida hata kidogo. Cheza sasa Aviator upate mgao wako haraka.
Yanga SC 2-0 Wiliete SC CAF Champion League magoli

Septemba 27 2025 Yanga SC 2-0 Wiliete SC CAF Champion League nyota wawili walifunga. Goli la kwanza lilifungwa na Pacome Zozuzoa dakika ya 70 akitumia pasi ya Andy Boyel. Goli la pili lilifungwa na Aziz Andambwile dakika ya 85 kwa pasi ya Offen Chikola.
Soma hii: Young Africans SC vs Wiliete SC CAFCL 27 Sept 2025: live score, Takwimu, vikosi, H2H, Utabiri
Magoli 2-0 waliyopata Yanga SC mbele ya Waangola Uwanja wa Mkapa Septemba 27 2025 yanawapeleka hatua inayofuata. Katika hatua ijayo watakutana na Silver Strikers ya Malawi. Wababe hawa wawili watakutana katika kuwania kufuzu hatua ya makundi.
Namna Yanga SC ilivyotinga hatua ya pili CAF

Yanga SC ya Tanzania imefuzu hatua ya pili kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-0. Mchezo wa ugenini ilipata ushindi wa mabao 3-0 na nyumbani ikawa ni mabao 2-0. Ndani ya dakika 180 kimataifa hawajaruhusu kufungwa Yanga SC.
Soma hii: Wiliete SC 0-3 Yanga SC Caf Champions League 2025
Katika mechi zote mbili Yanga SC ilikuwa na mbinu tofautitofauti. Kwenye mchezo wa ugenini walipata goli la ufunguzi kipindi cha kwanza. Mchezo wa pili Uwanja wa Mkapa walipata goli la ufunguzi kipindi cha pili.
Aziz Andambwile huyu alifungua ukurasa wa mabao ugenini. Alipopata nafasi ya kuanza Uwanja wa Mkapa alifunga pia. Katika mchezo wa pili ni Pacome alifungua ukurasa wa magoli.
Silver Striker itakayokutana na Yanga SC imefuzu hatua hiyo kwa kuwafungashia virago Elgeco Plus ya Madagascar. Ni faida ya bao la ugenini imewapa tiketi kutinga hatua ya pili. Mchezo wa kwanza ilikuwa Elgeco Plus 1-1 Silver Striker na mchezo wa pili nchini Malawi ilikuwa 0-0 Septemba 27 2025.
Mchezo ujao kimataifa Yanga SC
Katika hatua ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa kati ya Oktoba 17-19 nchini Malawi. Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Oktoba 24-29 Uwanja wa Mkapa. Mshindi kwenye mchezo atatinga hatua ya makundi.
Mbinu za Romain Folz zimejibu
Mbali na kutofungwa kimataifa katika mechi tano mfululizo ambazo wamecheza Yanga SC hawajaruhusu bao la kufungwa. Mbinu za Kocha Mkuu Romain Folz zimejibu licha ya tetesi kueleza kuwa huenda akaondoka ndani ya timu hiyo. Sababu inatajwa timu hiyo kutocheza katika kiwango kinachovutia.

Soma hii: Yanga SC 3-0 Pamba Jiji FC
Mechi tano za Yanga SC chini ya Kocha Romain Folz
| Mchezo | Aina ya mashindano |
| Yanga 1-0 Bandari ya Kenya | Mechi ya kirafiki, Yanga Day |
| Yanga SC 1-0 Simba SC | Ngao ya Jamii |
| Wiliete 0-3 Yanga SC | Ligi ya Mabingwa Afrika |
| Yanga SC 3-0 Pamba Jiji | Ligi ya NBC |
| Yanga 2-0 Wiliete SC | Ligi ya Mabingwa Afrika |
Hitimisho
Yanga SC 2-0 Wiliete SC CAF Champion League dakika 90 zilizokuwa na ushindani mkubwa. Wiliete walifanya jaribio moja la hatari kupitia kwa Junior liligonga mwamba. Wazawa wamekuwa katika ubora kimataifa wakiongozwa na Aziz ambaye kafunga jumla ya magoli mawili.


