- Macho na masikio ya wapenzi wa soka barani Afrika yatakuwa Francistown, Botswana leo jioni.
- Hii ni kushuhudia mechi kali ya Gaborone United vs Simba SC.
- Mechi hii ya Ligi ya Mabingwa Afrika ‘Caf Champions League itapigwa kwenye uwanja wa Obedi Itani Chilume kuanzia saa 20:00 usiku, kwa saa za Afrika Mashariki.
Usiku wa leo Jumamosi, jiji la Francistown, Botswana linatarajiwa kuwaka moto. Hii ni kufuatia mechi kali wa Ligi ya Mabingwa Afrika ‘Caf Champions League’ ya Gaborone United vs Simba SC. Huu ni mchezo wa hatua ya awali kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya makundi. Mechi hii unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Obedi Itani Chilume kuanzia saa mbili usiku, kwa saa za Afrika Mashariki.
SOMA HII PIA: Ratiba ya Caf Champions League 2025/26: Elewa kiundani droo zilizofanyika kwenye hii michuano mikali
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kuhusu Gaborone United vs Simba SC kupigwa Botswana
Ni wazi mchezo huu una umuhimu mkubwa kwa pande zote mbili, hasa kwa Simba SC ambao wamelenga kuanza kwa kishindo kampeni zao za kutafuta taji la Afrika msimu huu wa 2025/2026. Kwa upande wa Gaborone United, mechi hii ni fursa ya kuonyesha uwezo wao wakiwa nyumbani na mbele ya mashabiki wao. Hili pia ni daraja la kujitengenezea mazingira mazuri kabla ya mchezo wa marudiano.
Simba SC watangaza malengo makubwa Caf Champions League

Simba SC imeingia Botswana ikiwa thabiti na kufanya maandalizi kabambe. Kikosi cha wachezaji 22 kilisafiri kutoka Tanzania na kuwasili salama nchini Botswana. Wachezaji hao walionekana kuwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi, kwenye ardhi ya ugenini.
Katika mazungumzo na vyombo vya habari, Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, amesisitiza kuwa mechi hii haitakuwa rahisi kutokana na ubora wa Gaborone United kama mabingwa wa Botswana. Hata hivyo, aliweka wazi kuwa uzoefu na maandalizi waliyonayo, hususani kupitia mechi mbili za hivi karibuni walizocheza. Ikumbukwe Simba walivaana na Gor Mahia kwenye mchezo wa ushindi Simba Day, kabla ya kukubali kipigo kutoka kwa watani zao Yanga SC katika mchezo wa Ngao ya Jamii.
“Kwenda hatua ya makundi unahitaji kushinda mechi zote nyumbani na ugenini na sisi tumejiandaa kufanya hivyo. Timu yangu imecheza mechi mbili zenye uzito mkubwa kwenye Simba Day na Ngao ya Jamii. Hivyo wachezaji wangu wapo tayari kwa ushindani,” alisema Fadlu.
SOMA HII ZAIDI: Simba Day Septemba 10 2025 fullhouse mapema | Matukio yalibamba
Watamba kikosi timamu, licha ya mapungufu kidogo

Katika upande wa kikosi, Simba SC imebeba nguvu kazi iliyokamilika kwa asilimia kubwa. Nahodha wa timu hiyo, Shomari Kapombe, alithibitisha kuwa wachezaji wote waliopo Botswana wako fiti kwa asilimia 100. Lengo likiwa ni kupigania ushindi.
“Haitakuwa mechi rahisi, lakini tupo tayari kujitoa kwa ajili ya kuisaidia timu kupata ushindi. Kila atayepata nafasi ya kucheza atapambana kwa ajili ya timu,” alisema Kapombe.
Makocha hawa Simba, Kagoma hawatakuwepo kwenye benchi leo
Licha ya utimamu wa kikosi, Simba SC inatarajiwa kuwakosa baadhi ya watu muhimu kutokana na sababu mbalimbali. Kocha Msaidizi, Darian Wilken, na Kocha wa viungo, Riedoh Berdien, hawatakuwepo kwenye benchi. Hii ni baada ya kumbukumbu ya adhabu ya kadi nyekundu waliyoipata kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya RS Berkane.
Aidha, kiungo mkabaji Yusuph Kagoma, naye ameachwa Dar es Salaam kutokana na adhabu hiyohiyo ya kadi nyekundu. Pia, Simba itaendelea kumkosa kiungo mshambuliaji Mohamed Bajaber pamoja na beki Abdulrazak Hamza. Bajaber alipata majeraha kabla ya kuanza kwa msimu huku Hamza akipata maumivu katika mchezo wa Ngao ya Jamii.
SOMA HII PIA: Goli la Pacome Zouzoua ni offside au onside? | Wachambuzi wajibizana Edo Kumwembe vs Jemedari
Gaborone United: Wenyeji na ndoto yao kubwa

Kwa upande wa Gaborone United, huu ni mchezo wa hadhi kubwa na wa kihistoria. Kama mabingwa wa Botswana, wanajua kuwa wana jukumu la kulinda heshima yao nyumbani. Hii inaenda sambamba na kutoa matumaini kwa mashabiki wao kabla ya mchezo wa marudiano.
Ingawa taarifa nyingi kuhusu maandalizi ya Gaborone United hazijawekwa wazi. Historia yao ya hivi karibuni kwenye mashindano ya CAF, inatoa picha ya timu inayoweza kuwa kikwazo kikubwa kwa wapinzani wao. Hili linatarajiwa kwa kiasi kikubwa hasa wanapocheza nyumbani.
Kocha, Fadlu Davids aliweka wazi kuwa anawaheshimu wapinzani wao na anatambua kuwa watakutana na timu iliyoandaliwa vizuri: “Hata hivyo namheshimu sana kocha wa upinzani pamoja na timu yake, kwa sababu nao ni mabingwa. Hivyo tunategemea upinzani mkubwa, lakini tupo tayari kwa changamoto hiyo,” aliongeza.
Kikosi Kilichosafiri: Simba SC yapeleka mziki wote

Hiki hapa ni kikosi cha Simba SC kilichosafiri kwenda Botswana:
Makipa: Moussa Camara, Yakoub Suleiman, Alexander Erasto
Walinzi: Shomari Kapombe, Anthony Mligo, Rushine De Reuck, Karabou Chamou, Wilson Nangu, Naby Camara
Viungo: Allasane Kante, Kibu Denis, Elie Mpanzu, Ladaki Chasambi, Mzamiru Yassin, Neo Maema, Joshua Mutale, Jean Charles Ahoua, Morice Abraham, Daudi Semfuko
Washambuliaji: Steven Mukwala, Seleman Mwalimu, Jonathan Sowah
Kikosi hiki kinapewa nafasi kubwa, kutokana na uzoefu wa wachezaji wake wengi kimataifa na ndani ya mashindano ya CAF.
Hitimisho
Macho na masikio ya wapenzi wa soka barani Afrika yatakuwa Francistown, Botswana leo jioni kushuhudia mechi kali ya Gaborone United vs Simba SC. Huu ni mmoja wa michezo ya kuvutia ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa Simba, huu ni mwanzo wa safari ya matumaini kuelekea hatua ya makundi na hatimaye kutimiza ndoto ya kutwaa ubingwa wa Afrika. Kwa Gaborone United, ni fursa ya kuthibitisha ubora wao mbele ya timu iliyojaa historia ya mafanikio barani Afrika.

