Fadlu DFadlu D
  • Nyota wa Simba SC Hamza Jr ni mchezaji wa kwanza kufunga goli katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Uwanja wa Mkapa.
  • Simba SC 2-0 Gor Mahia zilikuwa dakika 90 za jasho kwa wababe hawa wawili kusaka ushindi kwenye mchezo wa kilele cha Simba Day.
  • Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC ameahidi kuwa msimu mpya utakuwa ni wa makombe baada ya kujenga kikosi msimu wa 2024/25

Simba SC 2-0 Gor Mahia ni matokeo kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Ushindi mkubwa kwa Simba SC Septemba 10 2025 ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya 2025/26. Huu ulikuwa maalumu kwa ajili ya kuhitimisha burudani za kilele cha tamasha la Simba Day.

Paisha Kindege cha SportPesa ushinde mamilioni

Ukipaisha Kindege cha SportPesa unavuna mamilioni sasa hivi. Rahisi sana, cheza Aviator uwe mmoja wa washindi. Mgao wa mamilioni unakusubiri.

image

 Simba SC 2-0 Gor Mahia wafungaji wa magoli

Simba SC 2-0 Gor Mahia
Chasambi nyota wa Simba SC kwenye mchezo wa kitaifa wa kirafiki Uwanja wa Mkapa.

Soma hii: Simba Day Septemba 10 2025 fullhouse mapema | Matukio yalibamba – SportPesa Tanzania

Magoli ya Simba SC yamefungwa na beki wa kati Hamza Abdulrazak dakika ya 7. Goli hilo lilitokana na pigo la Jean Ahoua ambaye alipiga Free Kick kwa mguu wake wa kulia akiwa nje ya 18. Hamza alimalizia kazi hiyo kwa pigo la kichwa na kuandika goli la kwanza kwa Simba SC.

Steven Mukwala alifunga goli la pili dakika ya 48. Mshambuliji huyu alipachika goli hilo akiwa ndani ya 18 likiwa ni alitumia mguu wa kulia. Mukwala alianzia benchi kwenye mchezo huo hivyo.

Simba SC yamakombe msimu wa 2025/26

Mashabiki Simba Day
Mashabiki wa Simba SC Uwanja wa Mkapa, Simba Day 2025.

Soma hii: Simba Day 2025 ni Simba SC vs Gor Mahia FC: highlight, vikosi, h2h, Ubaya Ubwela Part 2 moto utawaka!

Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC ameweka wazi itakuwa ni Simba SC ya makombe. Ikumbukwe kwamba 2024/25 timu hiyo iliambulia patupu. Katika Kombe la Shirikisho Afrika iligotea nafasi ya pili mabingwa wakiwa ni RS Berkane ya Morocco na kwenye ligi iligotea nafasi ya pili mabingwa wakiwa ni Yanga SC.

Fadlu amesema: “Msimu uliopita ulikuwa ni msimu wa kujenga timu. Msimu uliopita ulikuwa ni kwa ajili ya kutengeneza msingi. Msimu huu ni kwa ajili ya mataji, msimu huu ni kwa ajili ya makombe tunaamini Mungu atatusaidia,”

Kikosi cha Simba SC dhidi ya Gor Mahia

Moussa Camara anayevaa jezi namba 26 alianza langoni, Ladack Chasambi anayevaa jezi namba 36 alipewa majukumu ya kuwa beki. Anthony Mligo ingizo jipya kutoka Namungo alikabidhiwa jezi namba 5.

De Reuck ambaye ni beki alikabidhiwa jezi namba 23 huyu ni beki ingizo jipya. Hamza jezi namba 14 alicheza namba 6. Kibu Dennis kiungo mshambuliaji jezi namba 38 alipewa kitambaa cha unahodha. Jonathan Sowah mshambuliaji mpya wa Simba SC alikabidhiwa jezi namba 3. Jean Ahoua kiungo mshambuliaji alipewa jezi namba 10. Neo ingizo jipya alikabidhiwa jezi namba 35.

Wachezaji wa akiba

Hussen Abel, Yakoub Suleman, Alexader, Masinde. David Kameta, Shomari Kapombe, Mbegu, Yusuph Kagoma. Kante, Morice Abraham, Salum, Joshua Mutale, Awesu Awesu, Steven Mukwala, Seleman Mwalimu.

Rekodi kali kwa Simba SC mbele ya Gor Mahia

Simba Sc wakiwa nyumbani waliandika rekodi kali kwenye mchezo wa kwanza. Katika dakika 90 walifunga goli mojamoja kila dakika 45. Kipindi cha kwanza walifunga dakika ya 7 na kipindi cha pili walifunga dakika ya 48.

Mfungaji wa goli la kwanza alikuwa ndani ya 18 na mfungaji wa goli la pili alikuwa ndani ya 18. Kasi kubwa walianza kila kipindi katika dakika 15 za mwanzo. Goli la kwanza lilifungwa katika dakika 7 za mwanzo na goli la pili lilifungwa katika dakika 3 za mwanzo.

Wachezaji ambao walianza na walioingia kila mmoja alikuwa katika ubora wake. Mukwala alianzia benchi katika mchezo alipoingia alifunga goli la pili. Morice alianzia benchi alipoingia alipiga shuti kali akiwa nje ya 18 ambalo lilikuwa ni lenye hatari likilenga lango na kuokolewa na mlinda mlango wa Gor Mahia.

Taa za Uwanja wa Mkapa kuzimwa

Simba Day
Uwanja wa Mkapa

Soma hii: Simba SC vs Gor Mahia FC: Simba Day 2025 Highlight, vikosi, h2h, video ya Mbosso kuanguka yashtua

Kwenye tukio la Simba Day usiku taa za Uwanja wa Mkapa zote zilizimwa. Tukio hili lilikuwa na upekee wake. Baada ya taa za Uwanja wa Mkapa kuzimwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi waliwasha taa zao za simu.

Mbali na taa za simu kuwasha, ulipitishwa moto uliokuwa na ishara ya ndimi. Hii ilikuwa inamaanisha kwamba ni ndimi za Simba mnyama. Nembo ya Simba ilikuwa inatambulishwa uwanjani.

Utambulisho  wa kibabe kutoka kwa Ahmed Ally

Semaji Ahmed Ally alifanya utambulisho wa kibabe kwa wachezaji. Kila mchezaji alimtambulisha kwa aina yake katika tamasha kubwa la Simba Day. Miongoni mwa wachezaji aliowatambulisha ni kipa Suleman ambaye huyu alimtaja kuwa ni Tanzania One.

Kiungo Yusuph Kagoma huyu alitajwa kuwa ni kiumbe katili kuliko wote duniani. Kagoma ni kiungo mkabaji ambaye alikuwa na kikosi cha Simba SC msimu wa 2024/26. Bado yupo ndani ya Simba SC kwa msimu wa 2025/26.

Hitimisho

Simba sc 2-0 Gor Mahia ni ishara ya ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26. Simba SC itakuwa kwenye mchezo wa kwanza wa ushindani Septemba 16 2025 dhidi ya Yanga SC. Watani hawa wa jadi watakutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Share this: