Ecua vs Rayon SportsEcua vs Rayon Sports
  • Hatimaye Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga SC, wamewatangaza rasmi wapinzani wao katika ‘wananchi day’
  • Yanga SC vs Bandari FC Septemba 12, ndiyo burudani kubwa ya ushindani wa soka kwenye kilele wiki ya wananchi
  • Mashine zote mpya za Yanga kutambulishwa rasmi mbele ya Maelfu ya Wananchi.

Uongozi wa Yanga SC wamethibitisha mechi kali ya Yanga SC vs Bandari FC Septemba 12, ndiyo burudani rasmi ya soka kwenye siku ya kilele wiki ya wananchi. Hayo yameelezwa Makamu Rais wa timu hiyo, Arafat Haji wakati wa maandalizi ya hamasa kuelekea tukio hilo. Ikumbukwe kilele cha wiki ya wananchi ni siku maalum, ambayo hutumiwa kwa ajili ya kutambulisha wachezaji na kikosi kipya mbele ya mashabiki.

SOMA HII PIA: Yanga SC wiki ya wananchi ni Ijumaa Septemba 12

Paisha ‘Kindege’ cha Sportpesa ushinde mamilioni sasa kwa kubonyeza picha hii chini

SEO Banner LV

Historia ya Tamasha la Wananchi

Haji Manara na Mobetto
Haji Manara na Mobetto

Wiki ya wananchi ni miongoni mwa matamasha makubwa ya soka kwa ukanda wa Afrika Mashariki. Kwa kawaida Tamasha hili, hutumiwa kwa ajili ya kutambulisha wachezaji na kikosi kipya mbele ya mashabiki. Sambamba na hilo burudani za muziki na mechi kali ya soka pia hunogesha.

Ili kusherehesha zaidi tukio hilo, katika miaka ya karibuni mara nyingi tamasha hilo huhusisha burudani mbalimbali za wasanii wakubwa wa ndani nan je ya Tanzania. Wasanii hao hutoka katika viwanda mbalimbali ikiwemo muziki, sarakasi n.k.

SOMA HII ZAIDI: Usajili Yanga SC: Clement Mzize haendi popote | Takwimu muhimu, magoli, mechi | Kariakoo Dabi

Alichosema Makamu rais wa Yanga

Arafat Haji
Arafat Haji

Makamu wa Rais wa Yanga SC, Arafat akiongoza hafla maalum iloyoandaliwa na Tawi la Yanga Bandari, ikiwa ni maandalizi kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi leo Agosti 30, amesema: “Mshindani wetu kwenye kilele cha siku ya wananchi ni klabu ya Bandari kutoka Kenya. Niwatakie kila la kheri kwenye matawi yenu kwenye mchakato wa hamasa.

“Hakikisha hautamwacha mwanayanga mwenzako nyuma. Wote kwa pamoja tukaujaze uwanja wa Mkapa. Kumbukeni uwanja wa Mkapa ndio uwanja wetu wa nyumbani msimu huu. Haikuwa rahisi kufanyika siku ya Mwananchi.

“Ratiba ilikuwa ngumu sana. Viongozi tulifanya jitihada kubwa sana kuhakikisha tukio hili muhimu la kihistoria lifanyike. Kwa mantiki hii Wanachama na Mashabiki wetu tunao wajibu mkubwa kwa kumaliza tiketi zote.

Semaji Ali Kamwe naye atoa tamko zito kuhusu mechi ya Yanga SC vs Bandari FC Septemba 12

Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema: “Niwaombe tumpongeze sana makamu wa rais kwa kutenga muda wake kujumuika nasi. Tunafahamu ratiba zake zilivyombana siku ya leo lakini kwa heshima ameamua kujumuika nasi, kwenye mkutano wa maandalizi kuielekea sikukuu yetu Wananchi.

“Tayari klabu imetangaza tarehe ya Kilele cha wiki ya mwananchi ambayo ni tarehe 12/9/2025. Wengi wenu mmekuwa mkijiuliza kwanini Tamasha hili linafanyika siku ya Ijumaa na siyo jumamosi, au jumapili kama ilivyozoeleka. Niwaambie tu, ndugu zangu hawa viongozi wetu wamepambana sana mpaka tamasha hili kuwepo msimu huu.

“Kwa sababu ratiba za mechi za kalenda ya FIFA zimebana sana. Kama tungepanga tarehe nyingine, tungewakosa wachezaji wengi ambao wanaitwa kwenye timu zao za timu za Taifa. Mbali na hapo kuna ratiba ya Ngao ya Jamii na Ligi.

Mastaa wapya wanaosubiriwa kwa hamu kutambulishwa ndani ya Yanga Day ni:

Ecua Celestin
Ecua Celestin

Mohamed Doumbia

Alisaini kuitumikia Yanga SC ilimshusha staa huyu usiku wa Agosti 3, 2025. Doumbia ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC 2025/26, ambapo nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 amejiunga na Yanga SC akitokea FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech.

Boyeli

MVP wa zamani wa Ligi Kuu ya Zambia, ambaye naye amejiunga na Wananchi kutokea Afrika Kusini. Alitambulishwa Julai 31, 2025. Staa huyo mwenyw umri wa miaa 24 alikuwa anacheza Sekhukhune United ya Afrika Kusini. Sasa nyota huyo atahudumu kwa mkopo wa mwaka mmoja na Wananchi.

Ecua Elastin

1/08/ 2025 uongozi wa Yanga ulimtambulisha Ecua kwa dili la miaka miwili. Ikumbukwe Msimu wa 2024/25 alikuwa anacheza Zoman FC, ambapo alifunga magoli 15 na pasi 12 za magoli.

Balla Conte

Huyu ndiye staa ambaye usajili wake ulikuwa na mvutano mkubwa, hii ni baada ya kuelezwa kuwa alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC na Yanga SC. Julai 18, 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea.

Mastaa wengine ambao watatambulishwa Yanga Day ni Pamoja na Offen Chikola, Casemiro, Ninju na kocha wao Roman Folz.

SOMA HII ZAIDI: Usajili 2025/26: Yanga SC imetambulisha wachezaji wapya 11 Zimbwe Jr atikisa | Benchi jipya la ufundi

Hitimisho: Mbosso wa Aviola kulibeba tamasha mwaka huu?

Yanga SC vs Bandari FC Septemba 12
Mbosso na Aviola

Ukiachana na mechi ya Yanga SC vs Bandari FC Septemba 12, na ukweli kuwa tayari kashapata dili la kutumbuiza Simba Day, upo uwezekano mkubwa wa msanii wa kizazi kipya Mbosso Khan kulibeba tamasha hili. Hii ni baada ya kuwa na mafanikio makubwa alivyobeba sherehe za ubingwa wa Yanga, mwishoni mwa msimu uliopita. Ikumbukwe Mbosso kupiia ‘Hit Song’ yake ya Aviola alipata heshima kubwa, kutumbuiza katika hafla ya ubingwa wa Yanga. Hii inamuweka kwenye nafasi nzuri ya kupata tenda ya wiki yam wananchi.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.