Zimbwe Jr na JobZimbwe Jr na Job
  • Beki Mghana Assiki ni mchezaji wa mwisho mpya kutambulishwa Yanga SC akitokea Singida Black Stars.
  • Mohamed Hussen Zimbwe Jr usajili wake umekuwa gumzo kubwa kwa kuwa alikuwa nahodha wa watani wa jadi wa Yanga SC ambao ni Simba SC.
  • Conte Balla kwenye orodha ya wachezaji wapya waliotambulishwa Yanga SC ukiwa ni utambulisho wa kwanza kabisa Jangwani.

Yanga SC imetambulisha wachezaji wapya 11 kuelekea msimu mpya wa 2025/26. Katika wachezaji hao Mohamed Hussen Zimbwe Jr ni usajili uliotikisa kila kona. Hilo lilitokana na Zimbwe Jr kuwa muhimili ndani ya kikosi cha Simba SC 2024/25.

Shinda mamilini na Kindege cha SportPesa muda huu

Ni muda wa rubani kutua ardhini akiwa na mamilioni aliyoshinda. Rahisi sana ukicheza Aviator. Mgao ni mkubwa unakusubiri sasa hivi.

SEO Banner LV

Sababu za Zimbwe Jr saini yake kutikisa

Zimbwe Kapten
Mohamed Hussein ingizo jipya Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Soma hii: Mohamed Hussen Zimbwe Jr ni Yanga SC

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC aliweka wazi kuwa waliamua kumsajili beki huyo kutokana na ubora wake. Aliongeza kuwa usajili wa beki Zimbwe Jr umetikisa kila kona kutokana na ukubwa wa mchezaji na ubora alionao. Zimbwe Jr amesaini dili la miaka miwili atakuwa kwa mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara NBC.

“Usajili wa Zimbwe Jr umekuwa gumzo kila kona. Hii inatokana na ukubwa wa mchezaji na maamuzi yake kuchagua kusaini Yanga SC. Tuna mashindano mengi ambayo tunashiriki hivyo lazima tuwe na wachezaji wakubwa,”.

Orodha ya wachezaji wapya waliotambulishwa Yanga SC

Balla Conte

Balla Conte
Balla Conte mchezaji mpya Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Soma hii: Balla Conte amesaini rasmi Yanga SC na kutambulishwa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26

Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea. Nyota huyu mpya alisaini mkataba wa miaka mitatu.

Andy Boyeli

 Julai 31 2025 Andy Bobwa Boyeli mwenye miaka 24 alitambulishwa Yanga SC. Mshambuliaji huyo alikuwa anacheza Sekhukhune United ya Afrika Kusini kwa mkopo kwa msimu mmoja. Julai 31 alifunga ukurasa kwa wachezaji waliotambulishwa ndani ya mwezi huo ambao umeisha na sasa ni Agosti.

Lassine Kouma

Lassine Kouma ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC. Huyu ni mrithi wa mikoba mikoba ya Khalid Aucho. Kasajiliwa Yanga SC akitokea Stade Malien.

Offen Chikola

 Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025. Ni kandarasi ya miaka miwili. 2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo.

Casemiro

 Anaitwa Abdulnassir Mohamed maarufu kwa jina la Casemiro alitambulishwa rasmi Jangwani, Julai 23 2025. Ni mzawa ambaye atakuwa kwenye changamoto mpya. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania nafasi ndani ya uwanja.

Ninju

Abubakar Nizar Othuman, maarufu kwa jina la Ninju kutoka Azam FC alitambulishwa rasmi Julai 27 2025. Kulikuwa na kesi kuhusu usajili wa mchezaji huyu kutoka kwa Azam FC. Mwisho taarifa zilieleza kuwa wamefikia maafikiano mazuri hivyo mchezaji atabaki Yanga SC.

Ecua Elastin

Agosti Mosi 2025 alitambulishwa Yanga SC kwa dili la miaka miwili. Msimu wa 2024/25 alikuwa anacheza Zoman FC alifunga magoli 15 na pasi 12 za magoli. Rekodi hizo ni kwenye mashindano yote. Yeye ni raia wa Ivory Coast.

Doumbia

Agosti 3 2025 Yanga SC ilimtambulisha kiungo, Mohamed Doumbia. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 amejiunga na Yanga SC kutokea FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech. Staa huyo ana uwezo mkubwa wa kupiga mashuti ya mbali na kutengeneza nafasi kwa wengine.

Zimbwe Jr

Nahodha wa Simba SC 2024/25 Mohamed Hussen Zimbwe Jr alitambulishwa Yanga SC Agosti 6 2025 saa sita usiku.

Zimbwe Jr alitwaa tuzo ya beki bora msimu wa 2021/22. Ana tuzo ya MVP msimu wa 2016/17. Msimu wa 2023/24 alikuwa kwenye kikosi bora cha msimu ni mchezaji bora ambaye atakuwa na uzi wa Yanga SC 2025/26.

Edmund John

Agosti 15 2025 Yanga SC ilimtambulisha rasmi winga Edmund John kutoka Singida Black Stars. Nyota huyo alitambulishwa kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Rayon Sports 1-3 Yanga SC. Kwenye mchezo huo Edmund aliazia benchi.

Assinki

Assinki mazoezini
Assinki beki mpya wa Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC yamsajili Frank Assinki kutoka Ghana kwa mkopo | Usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Agosti 21 2025 Yanga SC ilimtambulisha nyota mpya kuelekea msimu wa 2025/26 ambaye ni beki wa kati. Anaitwa Frank Assinki ambaye ni raia wa Ghana na msimu wa 2024/25 alikuwa ndani ya kikosi cha Singida Black Stars.

Benchi jipya la ufundi Yanga SC

Romain

Romain Folz
Romain Folz Kocha Mkuu wa Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Soma hii: Romain Folz kocha mpya Yanga SC mwenye CV kubwa

Julai 23 2025 Kocha Mkuu wa Yanga SC Romain Folz alitambulishwa. Kocha huyo anabeba mikoba ya Miloud Hamdi aliyekuwa akikinoa kikosi hicho. Msimu wa 2025/26 atakuwa kwenye benchi la ufundi.

Mkurugenzi wa ufundi ni Paul

Paul Matthews alitambulishwa ndani ya Yanga SC Julai 29 2025. Hivyo atakuwa Jangwani msimu wa 2025/26. Huyu ni Mkurugenzi wa Ufundi.

Manu Rodriguez

Manu alitambulishwa Julai 29 2025. Huyu ni kocha msaidizi ndani ya Yanga SC. Kocha Mkuu ni Romain Folz ambaye naye ni mpya mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi.

Hitimisho

Yanga SC kambi yake kuelekea msimu mpya wa 2025/26 ni Avic, Kigamboni. Ilialikwa Rwanda kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Rayon Sports ikishinda kwa mabao 2-1. Inatarajiwa kushuka uwanjani Septemba 16 2025 dhidi ya Simba SC mchezo wa Ngao ya Jamii.

Share this: