- Wenyeji Kenya wamefungashiwa virago katika mchezo wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Madagascar kwa mikwaju ya penati.
- Dakika 120 zilikuwa zenye ushindani mkubwa kwa wababe hawa wawili waliokuwa wakisaka nafasi kutinga nusu fainali.
- Kenya walianza kufunga bao la kuongoza likawekwa usawa kwa penati na wapinzani wao Madagascar.
Timu ya taifa ya Madagascar imefuzu hatua ya nusu fainali CHAN 2024 kwa kuwaondoa wenyeji Kenya. Timu hiyo imeshinda kwa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya Kenya katika mchezo wa hatua ya robo fainali. Mchuano mkali wa kwanza wa robo fainali umeshuhudia vinara wa kundi A wakifungashiwa virago.
Rubani ni muda wa kufurahia mamilioni wikiendi
Wikiendi kwa marubani huwa ni kicheko. Jambo lakufanya ni kupaisha Kindege cha SportPesa uvuna mkwanja wako. Rahisi sana, cheza Aviator sasa hivi upate mgao wako.

Hapa ndipo mchezo ulichezwa
Mchezo huo mkubwa Afrika ulichezwa Uwanja wa taifa wa Moi. Ni Agosti 22 2025 mashabiki walishuhudia mtanange huo mkali. Huzuni kwa wenyeji Kenya kuondoka katika mchezo huo.
Ni robo fainali ya kwanza kuchezwa huku mashabiki wengi wa Kenya wakijitokeza uwanjani. Kasarani, Moi ilikuwa ni kazi ya dakika 120 kwa wababe hawa kusaka mshindi. Katika dakika za 90 ilikuwa ni 1-1.
Muda wa kawaida ambao ni dakika 90 ulikamilika bila mshindi kupatikana hivyo ziliongezwa dakika 30. Ndani ya dakika 120 bado mshindi hakupatikana hivyo mshindi alitafutwa kwa penati. Hapo ndipo bahati ikawa upande wa Madagascar ambao waliibuka wababe.
Dakika 45 tasa kwa timu zote mbili
Dakika 45 za mwanzo milango ilikuwa migumu migumu kwa timu zote mbili. Sio wenyeji Kenya wala wageni Madagascar ngoma ilikuwa ni nzito. Mbinu za makocha wote zilikuwa zimekwama kuwanyanyua mashabiki uwanjani kushangilia kwenye mchezo wa CHAN 2024.
Wafungaji wa mabao dakika 90

Soma hii: CHAN 2024: Kenya 1-0 Morocco
Kwa dakika 45 za mwanzo mpaka zinagota mwisho hakuna bao. Ilibidi wenyeji Kenya kusubiri mpaka kipindi cha pili kufunga kwenye mchezo wa robo fainali. Shukrani kwa Alphonce Omija ambaye alifunga bao la kwanza dakika ya 48. Hiyo ilikuwa ni kipindi cha pili cha mchezo zikiwa zimepita dakika tatu. Wenyeji hao walistahili kupata bao hilo kutokana na kutengeneza nafasi za mara kwa mara katika mchezo huo na mwisho wakapata bao la kuongoza.
Madagascar waliweka usawa kwa pigo la penati
Baada ya Lalaina Rafanomezantsoa nyota wa Madagascrar katika harakati za kutaka kufunga bao alichezewa faulo ndani ya 18. Hali hiyo ilipelekea mwamuzi kutoa faida ya penati. Fenohasina Gilles Razafimaro alipewa jukumu la kupiga penati hiyo akafunga dakika ya 68.
Mpigaji huyo hakukosa aliwarejesha kwenye mchezo wachezaji wenzake. Kasi iliendelea kwa kila timu kusaka ushindi ndani ya dakika ambazo zilibaki. Mwisho matokeo yalibaki hivyo mpaka mwisho wa mchezo zikichezwa jumla ya dakika 120.
Kikosi cha Kenya kilichoanza
Omondi B, Esambe Bandi, Kibwage M, Muchiri B, Nabwire M, Ogam R, Okwaro M, Omar A huyu ni nahodha. Omija A, Omondi B. S, Onyango A.
Madagascar
Ramandimbisoa M, Andrianarimanana A, Rabearivelo B, Rabemanjara R, Rafanomezantsoa L. C, Ranaivoson J. Randriamanampisoa N. Randriamanampisoa N. Randrianirina H, Razafima hatana M, Razafimaro F.
Hawa hapa wapigaji penati robo fainali
S. Mohammed, D. Sakari, na S. Owino hawa walifunga penati kwa Kenya, huku M. Kibwage na A. Omija hawa walikosa kwenye mapigo ya penati ambazo walipiga.
Kwa upande wa Madagascar, Rafanomezantsoa, Razafimaro, Rakotondraibe na Randriamanampisoa hawa walifunga huku Randrianirina pekee akikosa pigo la penati.
Mechi nne za Madagascar zilizopita
Burkina Faso 1 – 2 Madagascar Agosti 16, 2025 mchezo wa CHAN 2024. Madagascar 2 – 0 Central African Republic Agosti. 13, 2025 CHAN 2024. Tanzania 2 – 1 Madagascar Agosti. 9, 2025 CHAN 2024. Madagascar 0 – 0 Mauritania Agosti. 3, 2025 CHAN 2024.
Mechi tano za Kenya zilizopita

Soma hii: Tanzania vs Burkina Faso na Kenya vs DR Congo: Wenyeji waanza kwa kishindo CHAN 2024.
Zambia 0 – 1 Kenya Agosti 17, 2025 CHAN 2024. Kenya 1 – 0 Morocco Agosti. 10, 2025 CHAN 2024. Angola 1 – 1 Kenya Agosti. 7, 2025 CHAN 2024. Kenya 1 – 0 Democratic Republic of Congo Agosti 3, 2025 CHAN 2024. Kenya 2 – 1 Chad Juni 10, 2025 mchezo wa kirafiki.
Hitimisho
Kenya ni wenyeji wa kwanza kuaga mashindano ya CHAN 2024. Katika kundi Kenya ilimaliza ikiwa namba moja baada ya kukusanya pointi 10. Imeumaliza mwendo ikiacha rekodi nzuri ya mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani.


