- Tanzania 0-1 Morocco mchezo wa robo fainali ya pili Uwanja wa Mkapa ikiwa ni kilio kwa wenyeji wa mashindano hayo makubwa Afrika.
- Morocco inapenya mpaka hatua ya nusu fainali ikiwa ugenini, itakutana na mshindi kati ya Uganda na Senegal.
- Ouussama Lamlioui mfungaji pekee wa bao la ushini kwa Morocco kipindi cha pili bao ambalo limeipeleka timu hiyo hatua ya nusu fainali.
Tanzania 0-1 Morocco ni kilio kwa wenyeji baada ya kupoteza mchezo wa robo fainali CHAN 2024. Mchezo huo ulikuwa ni wa pili umechezwa Uwanja wa Mkapa Agosti 22 2025, saa mbili usiku. Tanzania inakuwa timu ya pili kwa wenyeji kuondolewa baada ya Kenya kuanza.
Furaha ya kupaisha Kindege cha SportPesa uhakika wa kuvuna
Marubani kuna furaha kubwa kwenye kupaisha kindege cha SportPesa. Kuna mamilioni kwa ajili yako cheza sasa Aviator na ushinde. Mgao upo wakutosha.

Mfungaji wa bao la ushindi
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Tanzania 0-1 Morocco. Bao la ushindi limefungwa na Ouussama Lamlioui. Ni dakika ya 65 bao hilo limedumu mpaka mwisho wa mchezo.
Morocco inatinga hatua ya nusu fainali. Itakutana na mshindi wa mchezo kati ya Uganda ama Senegal. Ni Uganda pekee mwenyeji aliyebaki katika mashindano ya CHAN 2024.
Tanzania vs Morocco mechi walizokutana

Soma hii: Tanzania vs Morocco robo fainali dume Uwanja wa Mkapa
Wababe hawa wawili jumla wamekutana katika mechi sita. Ushindi kwa Tanzania ni mechi moja. Morocco ilipata ushindi katika mechi 5
Morocco 2-0 Tanzania, mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia, Machi 26 2025, Morocco 3-0 Tanzania, Januari 17 2024, mchezo wa Afcon. Tanzania 0-2 Morocco, Novemba 21 2023, mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.
Morocco 2-1 Tanzania, Juni 8 2013, mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Tanzania 3-1 Morocco, Machi 24 2013, mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Agosti 22 2025, Tanzania 0-1 Morocco, CHAN 2024.
Kikosi cha Tanzania kilichoanza dhidi ya Morocco

Soma hii: CHAN 2024: Central African 0-0 Tanzania, Uwanja wa Mkapa
Yakuob Suleiman mlinda mlango, Shomari Kapombe beki, Mohammed Hussein Zimbwe Jr beki, Ibrahim Bacca beki, Dickson Job nahodha huyu ni beki.
Yusuph Kagoma ni kiungo mkabaji, Idd Nado ni kiungo, Mudathir Yahya ni kiungo, Feisal Salum ni kiungo, Clement Mzize ni mshambuliaji na Abdul Suleiman ambaye ni kiungo mshambuliaji.
Wachezaji wa akiba ni Aishi Manula, Hussen Masalanga. Abdulazack Hamza, Mishano Michael, Ahmed Pipino, Shekhan Khamis, Jammy. Pascal Msindo, Wilson Nangu, Lusajo Mwaikenda, Elias Lameck, Ibrahim.
Kikosi cha Morocco kilichoanza

Soma hii: CHAN 2024: Kenya 1-0 Morocco
Al Harrar mlinda mlango, Bach, Kairi, Boulacscout, Lamliour. Bougrine, Bellamari, Mehri. Hrimati, Baba, Mchakhchekh.
Hawa hapa wachezaji wa akiba
Fouad Zahouani , Reda Hajji , Khalid Ait Ouarkhane, Youness El Kaabi, Rachid Ghanimi. Amine Souane, Salaheddine Errahouli, Imad Riahi,Mohamed Moufid. Saifeddine Bouhra , Anas El Mahraoui, Hossam Essadak.
Rekodi ya mechi 8 za Tanzania
Eswatini 1-2 Tanzania, mchezo huu ulichezwa Juni 11 2025. Tanzania 1-0 Uganda ulichezwa Julai 22 2025. Tanzania 2-1 Senegal ulichezwa Julai 27 2025.
Tanzania 2-0 Burkina Faso ulichezwa Agosti 2 2025. Huu ulikuwa ni mchezo wa ufunguzi wa CHAN 2024 Uwanja wa Mkapa. Mauritania 0-1 Tanzania, Agosti 6 2025. Tanzania 2-1 Madagascar. Agosti 16 2025, Central African 0-0 Tanzania. Agosti 22 Tanzania 0-1 Morocco.
Matokeo ya Tanzania CHAN 2024
Agosti 2 2025, Tanzania 2-0 Burkina Faso. Mauritania 0-1 Tanzania. Tanzania 2-1 Madagascar, Agosti 9 2025. Agosti 16 Central African 0-0 Tanzania. Agosti 22 2025, Tanzania 0-1 Morocco. Huu ni mchezo wa kwanza Tanzania kupoteza katika CHAN 2024.
Katika mechi nne zilipota za CHAN Tanzania ilipata ushindi kwenye mechi tatu. Sare moja hivyo mwendo katika hatua ya makundi ulikuwa imara. Kwenye mchezo wa robo fainali imekwama kupaya ushindi ndani ya dakika 90.
Hitimisho
Wenyeji Tanzania wamepoteza mchezo wa kwanza katika mashindano ya CHAN 2024 mbele ya Morocco. Wachezaji baada ya mchezo walikuwa kwenye masikitiko na sura za vilio kutokana na malengo kuishia njiani. Safari imeishia hatua ya robo fainali.


