- Wababe Sudan vs Senegal kwenye mchezo wa makundi waliacha gumzo kutokana na mchezo mkali baini yao kusaka ushindi.
- Sudan wanamaliza wakiwa vinara kwenye kundi D huku Senegal wakifuata nafasi ya pili wote wakiwa na alama 5.
- Timu zote mbili zitacheza robo fainali CHAN 2024 mashindano makubwa Afrika yanayozihusu timu za ndani.
Sudan vs Senegal ilikuwa ni mechi dume katika kundi D CHAN 2024. Mchezo huo ulikuwa gumzo ulichezwa Agosti 19 2025, Uwanja wa Amaan Complex. Mpaka dakika 90 zinakamilika hakuna mbabe aliyeona lango la mwenzake ikiwa ni 0-0.
Vuna mamilioni na kindege cha SportPesa
Ushindi ni wako leo unakusubiri sasa hivi. Unachotakiwa kufanya ili uvune mamilioni paisha kindege. Haujachelewa cheza Aviator upate mgao wako.

Senegal wanawapa tabu Sudan
Senegal chini ya Kocha Mkuu Pape Thiaw imekuwa ikipata matokeo mbele ya Sudan. Tofauti yao kwenye kundi D ilikuwa ni bao moja pekee. Hivyo Senegal walikuwa wakisaka nafasi kuongoza kundi hilo.
Sudan ambayo kwenye rekodi za FIFA za hivi karibuni ni nafasi ya 114 inafundishwa na Kocha Mkuu Kwesi Appiah ambaye ni rai awa Ghana. Imecheza mechi tatu za hatua ya makundi bila kupoteza. Na wamemaliza wakiongoza kundi wakiwa na pointi 5.
H2H Sudan vs Senegal

Soma hii: CHAN 2024: Sudan 0-0 Senegal kundi D
Mechi hii ni mechi ya nne kwa timu hizi mbili. Katika mechi hizo Senegal alipata ushindi kwenye mechi mbili na walitoshana nguvu mechi mbili. Sudan hajawahi kupata ushindi mbele ya Senegal kwenye rekodi za hivi karibuni.
Rekodi zinaonyesha kuwa Machi 22 2025 Sudan 0-0 Senegal. Huu ulikuwa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia. Oktoba 16 2018 Sudan 0-1 Senegal huu ulikuwa mchezo wa kuwania kufuzu African Cup of Nations, (AFCON). Oktoba 13 2018 Senegal 3-0 Sudan mchezo wa AFCON na Agosti 19 2025, Sudan 0-0 Senegal, mchezo wa CHAN hatua ya makundi.
Dakika 450 za Senegal
Katika mechi 5 zilizopita kwa Senegal ambazo ni dakika 450, Senegal ilipata ushindi kwenye mechi mbili, sare mechi moja na ilipoteza mechi mbili. Agosti 12 2025, Senegal 1-1 Republic Of Congo, (CHAN). Agosti 5 2025, Senegal 1-0 Nigeria, (CHAN). Julai 24 2025 Uganda 2-1 Senegal, mchezo wa kirafiki. Julai 22 2025, Tanzania 2-1 Senegal mechi ya kirafiki. Julai 7 2025 Senegal 1-0 Guinea, mechi ya kirafiki.
Dakika 450 za Sudan
Kwenye mechi 5 za Sudan ambazo ni dakika 450 walipata ushindi mchezo mmoja pekee na nne ilikuwa ni sare. Agosti 12 2025, Sudan 4-0 Nigeria, (CHAN). Agosti 5 2025 Republic of Congo 1-1 Sudan, (CHAN). Machi 25, Sudan 1-1 Sudan ya Kusini kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Machi 22 2025 Sudan 0-0 Senegal, mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Machi 13 2025 Oman 0-0 Sudan mchezo wa kirafiki.
Kikosi cha Sudan ambacho kilichoanza mchezo wa tatu
Mchezo wa tatu wa makundi CHAN 2024 kikosi kilikuwa namna hii:-Mohamed Abooja mlinda mlango, Yaser Awad, Altayeb Abaker, Mazen Simbo, Ahmed Yousif. Abdel Raouf, Salah Adel, Walieldin Khedr, Mazin Fadul Al-Bahli. Ali Abdalla, Musa Hussien.
Wachezaji wa akiba wa Sudan
Ahmed Al Fatih (mlinda mlango), Mohamed Madani (mlinda mlango), Mohamed Saeed Ahmed (beki wa kati). Musab Makeen (beki wa kulia), Faris Abdallah (beki wa kushoto). Khater Gumaa (kiungo), Maaz Kandani (kiungo), Al Misbah Faisal (kiungo), Mohamed El-Rasheed (kiungo), Mubark Abdalla (winga). Mohamed Tia Asad (winga), Awad Zayed (mshambuliaji wa kati).
Kikosi cha Senegal ambacho kilianza dhidi ya Sudan
M. Diof, J. Samb, (13), M. Sembene, (14), S.Ndiaye, (2). D. Ba, (22), O.Ba, (11), M. Yaya Ly, (17) Moussa Cisse, (6), L.Gueye, (7), C.Gomis, (9), P.Badji, (24).
Wachezaji wa akiba wa Senegal
Cheikh Ndoye (mlinda mlango), Mbaye Ndiaye (beki wa kati), Baye Ciss (beki wa kati), Amadou Coly (beki wa kulia), Ousseynou Seck (kiungo). Bonaventure Fonseca (kiungo), Moctar Koite (kiungo). Insa Boye (kiungo), Issa Kane (kiungo), Ameth Niang (kiungo), Vieux Cisse (kiungo), Ababacar Sarr (winga).
Kadi za njano na penati kukataliwa na VAR

Soma hii: Uganda imeishinda Niger 2-0 mchuano wa Kundi C
Kwenye mchezo huo kadi ya njano ya kwanza ilionyeshwa kwa mchezaji wa Senegal. Ni kiungo mwenye miaka 23, Mbaye Yaya Ly ambaye anacheza Klabu ua AS Pikine. Alionyeshwa kadi hiyo ya njano kwa kumchezea faulo Ahmed Tabanja wakati akiokoa hatari.
Kadi ya pili ya njano ilikuwa ni ya kwanza kwa Sudan. Beki mwenye miaka 23 ambaye anacheza Klabu ya Al Hilal Omdurman Mazen Simbo. Alionyeshwa kadi hiyo baada ya kucheza faulo mbaya kwa mpinzani.
Dakika ya 43 Sudan walipata penati. Oumar Ba alimsukuma mchezaji Walieldin na hilo lilimpa ruhusa mwamuzi kutoa adhabu ya pigo la penati kwa Sudan.
Wakati Sudan wakiwa na faida ya adhabu ya penati mwamuzi Brighton Chimene alifanya mawasiliano na wasimamizi wa VAR. Baada ya kurudia mara kadhaa, penati hiyo ilifutwa.
Hitimisho
Sudan itacheza na Algeria robo fainali Agosti 23 Uwanja wa Mandela. Uganda na Senegal ni Agosti 23, Uwanja wa Nelson Mandela. CHAN 2024 imekuwa yenye kasi ndani ya dakika 90.


