Yamal na DembeleYamal na Dembele
  • Yamal na Dembele watikisa listi mastaa 30 Tuzo ya Ballon d’Or. Joto lapanda, Dunia yagawanyika
  • Tuzo hizo kwa mwaka huu zinatarajiwa kutolewa rasmi Septemba 22, nchini Ufaransa.
  • Afrika nayo yaingiza mastaa 3 kwenye listi ya mwaka huu.

Agosti 7, 2025 ilikuwa siku ya kihistoria kwa soka duniani. Hii ni baada ya listi ya mastaa 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora duniani Ballon d’Or kwa mwaka 2025 kutangazwa rasmi. Ikumbukwe hii ni listi inayowakutanisha mastaa wa soka waliotamba msimu uliopita.

Shinda mamilioni ya kindege ‘Aviator’ cha SportPesa sasa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani Aviator ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda sasa kirahisi kwa kubonyeza picha hii chini.

SEO Banner LV

Hawa hapa mastaa 30 wanaowania tuzo hiyo mwaka huu

Majina ya wagombea tuzo
Majina ya wagombea tuzo 30

Majina 30 ya nyota waliopenya kwenye tuzo hizo mwaka huu ni kama ifuatavyo;

Ousmane Dembélé (PSG & Ufaransa)

Gianluigi Donnarumma (PSG & Italy)

Jude Bellingham (Real Madrid & England)

Désiré Doué (PSG & Ufaransa)

Denzel Dumfries (Internazionale & Uholanzi)

Serhou Guirassy (Borussia Dortmund & Guinea)

Erling Haaland (Manchester City & Norway)

Viktor Gyökeres (Arsenal & Sweden)

Achraf Hakimi (PSG & Morocco)

Harry Kane (Bayern Munich & England)

Khvicha Kvaratskhelia (PSG & Georgia)

Robert Lewandowski (Barcelona & Poland)

Alexis Mac Allister (Liverpool & Argentina)

Lautaro Martinez (Internazionale & Argentina)

Scott McTominay (Napoli & Scotland)

Kylian Mbappé (Real Madrid & France)

Nuno Mendes (PSG & Ureno)

João Neves (PSG & Ureno)

Pedri (FC Barcelona & Uhispania)

Cole Palmer (Chelsea & England)

Michael Olise (Bayern Munich & Ufaransa)

Raphinha (Barcelona & Brazil)

Declan Rice (Arsenal & England)

Fabián Ruiz (PSG & Uhispania)

Lamine Yamal (Barcelona & Uhispania)

Florian Wirtz (Liverpool & Uhispania)

Vitinha (PSG & Ureno)

Vinícius Júnior (Real Madrid & Brazil)

Virgil van Dijk (Liverpool & Uholanzi)

Mohamed Salah (Liverpool & Misri)

SOMA HII PIA: Dembele au Yamal nani atashinda Tuzo ya Ballon d’Or 2025?

Yamal, Dembele waigawa Dunia, joto lapanda

Washindani na uwezekano wa ushindi
Washindani na uwezekano wa ushindi

Ousmane Dembélé wa PSG ameonekana wazi kuwa kiongozi wa kasi katika ushindani huu. Dembele alichangia kwa kiwango cha juu kuhakikisha PSG ilishinda mataji matatu msimu uliopita. Mataji hayo ni Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu ya Ufaransa na Kombe la mfalme ‘Coupe de France’. 

Dembele anapata upinzani mkubwa kutoka kwa, Lamine Yamal wa Barcelona. Akiwa na umri mdogo kiasi cha kutimiza 18 hivi karibuni, nyota huyo amejizolea umaarufu mkubwa katika soka. Hii ni kutokana na uwezo wake mkubwa wa huduma zake za magoli na pasi kwa usahihi. Baadhi ya mastaa wa Barcelona ambao wameingia kwenye listi hiyo ni Raphinha, Lewandowski na Pedri.

SOMA HII ZAIDI: Lamine Yamal akabidhiwa jezi namba 10 ya Messi Barcelona, asaini Mkataba mpya mpaka 2031

MO Salah naye hayuko mbali

Mohamed Salah wa Liverpool pia ni miongoni mwa wachezaji ambao wanapewa nafasi kubwa pia. Hii ni kutokana na mchango wake mkubwa katika kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza. Sababu nyingine ikiwa takwimu binafsi za magoli na asisti.

PSG yaweka rekodi ya kuingiza wachezaji wengi zaidi

Ballon d'Or (-)
Ballon d’Or (-)

Mabingwa wa Ufaransa PSG wanashikilia nafasi ya kwanza kwa kuingiza wachezaji wengi. Kati ya mastaa 30 waliopenya PSG imeandikisha majina ya mastaa tisa kwenye orodha hiyo. Hii inathibitisha ushuhuda wa mafanikio yao ya kushinda taji kubwa kitu walichongojea kwa muda mrefu. Real Madrid wameandikisha majina matatu ya Mbappé, Bellingham na Vinícius Júnior.

SOMA HII PIA: Chelsea FC 3-0 PSG FIFA Club World Cup 2025 | Cole Palmer, Joao Pedro magoli ya ushindi

Afrika nayo yaingiza mastaa 3

Yamal na Dembele watikisa listi mastaa 30 Tuzo ya Ballon d’Or 2025
Guirassy

Soka la Afrika linazidi kukua ambapo kwenye listi ya mwaka huu wachezaji watatu wa Kiafrika wamepenya ambao ni: Mohamed Salah (Misri), Achraf Hakimi (Morocco) na Serhou Guirassy (Guinea).

Hitimisho: Scott aandika rekodi ya kipekee Scotland

Staa wa zamani wa Manchester United ambaye kwa sasa anakipiga na Napoli ya Italia, Scott McTominay naye ashtua. Staa huyo amepenya kwenye listi hii huku akiwa mchezaji wa kwanza wa kutoka Scotland kufanya hivyo tangu mwaka 1987. Hii inampa staa huyo nafasi kubwa ya kujipongeza.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.