BoyeliBoyeli
  • Yanga SC yatambulisha wapya 9 kuelekea msimu ujao wa 2025/26 ni watu wa kazikazi.
  • Andy Boyel mwenye miaka 24 ni miongoni mwa nyota hao huku Balla Conte akiwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa.
  • Orodha bado haijaisha kwa kuwa wapo wengine wapya watashushwa na kutambulishwa Jangwani.

Yanga SC imetambulisha wachezaji wapya 9 akiwemo mshambuliaji Andy Bobwa Boyeli ikiwa ni kuelekea msimu wa 2025/26. Huo ni mwanzo kwa kuwa wapo wengine wanafuata. Ikumbukwe kwamba Yanga SC ni mabingwa watetezi wa ligi baada ya kutwaa taji hilo msimu wa 2024/25.

Cheza Aviator uvune mamilioni sasa hivi

Wikiendi Kindege hakifeli kwa marubani ni kuvuna mamilioni yakutosha. Muda ni sasa cheza Aviator. Ushindi unakusubiri na mgao upo.

Aviator banner

Mshambuliaji Boyeli utambulisho wake

Andy Boyel
Andy Boyel ingizo jipya Yanga SC.

Soma hii: Baada ya ‘Tshabalala’ na Conte Yanga SC yashusha straika Boyeli: Tetesi usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Ni Julai 31 2025 alitangwaza mshambuliaji Andy Bobwa Boyeli mwenye miaka 24. Nyota huyo alikuwa Sekhukhune United ya Afrika Kusini kwa mkopo kwa msimu mmoja. Mkataba wake ulikuwa na kipengele cha kununuliwa moja kwa moja.

2022/23 akiwa na Power Dynamos, Andy Boyeli alitwaa kiatu cha mfungaji bora. Ilikuwa ni kwenye ligi ya Zambia. Alikamilisha msimu kwa kufunga magoli 18 na msimu huo alitwaa tuzo ya MVP.

Orodha ya wapya Yanga SC 2025/26

Romain

Julai 23 2025 Kocha Mkuu wa Yanga SC Romain Folz alitambulishwa. Kocha huyo anabeba mikoba ya Miloud Hamdi aliyekuwa akikinoa kikosi hicho. Msimu wa 2025/26 atakuwa kwenye benchi la ufundi.

Paul Matthews

Paul Matthews alitambulishwa ndani ya Yanga SC Julai 29 2025. Hivyo atakuwa Jangwani msimu wa 2025/26. Huyu ni Mkurugenzi wa Ufundi.

Manu Rodriguez

Manu alitambulishwa Julai 29 2025. Huyu ni kocha msaidizi ndani ya Yanga SC. Kocha Mkuu ni Romain Folz ambaye naye ni mpya mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi.

Lassine Kouma

Lassine Kouma ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC. Huyu ni mrithi wa mikoba mikoba ya Khalid Aucho. Kasajiliwa Yanga SC akitokea Stade Malien.

Balla Conte

Balla Conte
Balla Conte mchezaji wa kwanza kutambulishwa Yanga SC kuelekea 2025/26. Source: Yanga SC.

Soma hii: Balla Conte amesaini rasmi Yanga SC na kutambulishwa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26

Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea. Nyota huyu mpya alisaini mkataba wa miaka mitatu.

Offen Chikola

 Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025. Ni kandarasi ya miaka miwili. 2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo.

Casemiro

 Anaitwa Abdulnassir Mohamed maarufu kwa jina la Casemiro alitambulishwa rasmi Jangwani, Julai 23 2025. Ni mzawa ambaye atakuwa kwenye changamoto mpya. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania nafasi ndani ya uwanja.

Ninju

Abubakar Nizar Othuman, maarufu kwa jina la Ninju kutoka Azam FC alitambulishwa rasmi Julai 27 2025. Atakuwa kwenye changamoto mpya. 2024/25 alikuwa kwenye timu ya vijana.

Walioongeza mikataba wengine Yanga SC

Israel Mwenda

Julai 29 2025 Yanga SC ilimtambulisha Israel Mwenda kuongeza mkataba. Mwenda alitambulishwa kuongeza kandarasi ya miaka miwili Jangwani. Yupo Jangwani msimu wa 2025/26.

Mudathir Yahya

Mudathir Yahya kiungo mkabaji bado yupo ndani ya kikosi cha Yanga SC. Julai 22 2025 aliongeza mkataba wa miaka miwili. Atakuwa ndani ya Yanga SC mpaka 2027.

Dennis Nkane

Kiungo mshambuliaji Dennis Nkane aliongeza mkataba wa miaka miwili mpaka 2027. Nkane hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza msimu wa 2024/25. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania namba msimu ujao kwenye benchi jipya.

Kiungo huyu alitambulishwa rasmi kuongeza mkataba Ilikuwa ni Julai 25 2025. Hivyo bado mchezaji huyo ataendelea kuwa Jangwani. Ni miongoni mwa wachezaji waliovaa medali za ubingwa msimu wa 2024/25.

Pacome

Nyota huyu alikamilisha msimu akiwa kafunga jumla ya mabao 12 na pasi 10. Kwenye mabao hayo 12 alifunga mabao mawili kwa penati. Jina ni Pacome Zouzoua aliongeza mkataba wa miaka miwili Julai 24 2025.

Kiungo huyu mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia. Kafunga mabao 7 kati ya 12 aliyofunga. Mguu wa kushoto katupia mabao manne. Ni pigo la kichwa alifunga bao moja mchezo dhidi ya Coastal Union.

Abuya

Duke Abuya winga wa Yanga SC ameongeza mkataba wa miaka miwili. Yupo Jangwani mpaka 2027. Julai 27 2025 alitangazwa kuongeza mkataba.

Maxi

Maxi Nzengeli aliongeza mkataba Julai 28 2025 wa miaka miwili. Yupo hapo mpaka 2027. Huyu ni mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Yanga SC msimu wa 2024/24 alifunga dhidi ya Kagera Sugar.

Aziz Andambwile

Aziz Andambwile
Aziz Andambwile bado yupo Jangwani. Source: Yanga SC.

Soma hii: Aziz yupo sana Jangwani mpaka 2027

Aziz Andambwile alitangazwa kuwa bado yupo Jangwani baada ya kuongeza mkataba wa miaka miwili. Andambwile ni uhakika njano na kijani 2025/26. Yeye ni kiungo ambaye alicheza jumla ya mechi tano za ligi msimu wa 2024/25.

Rekodi zinaonyesha kuwa kwenye mechi hizo alitumia dakika 125. Hakufunga wala kutoa pasi ya bao. Yanga SC ilitwaa ubingwa wa ligi ikiwa na pointi 82 na ilifunga mabao 83.

Katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Azam Complex alikomba dakika 90. Unakuwa ni mchezo pekee aliovuja jasho mwanzo mwisho ndani ya ligi. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukasoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania.

Mchezo huo ulichezwa Oktoba 22 2024, mwamuzi alikuwa Ahmed Arajiga. Yanga SC ilivuna pointi tatu jumlajumla. Ameongeza mkataba wa miaka miwili bado yupo Jangwani mpaka 2027.

Hitimisho

Yanga SC inafanya maboresho makubwa kwenye kikosi hicho kuelekea msimu mpya wa 2025/26. Malengo ya Yanga SC ni kuwa na wachezaji bora na imara. Wachezaji hao watakuwa na kazi kwenye anga la kitaifa na kimataifa kupambania mataji.

image
Share this: