- Khadim Diaw beki wa Al Hilal mwenye spidi akiwa uwanjani anatajwa kuwa mrithi wa mikoba ya Zimbwe Jr ndani ya Simba SC.
- Yanga SC kwenye usajili hawapoi wanatajwa kumalizana na Zimbwe Jr ambaye alikuwa katika kikosi cha Simba SC msimu wa 2024/25.
- Simba SC kufanya maboresho makubwa kuelekea msimu wa 2025/26 wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC.
Khadim Diaw beki wa kushoto anatajwa kusaini dili nono ndani ya Simba SC. Beki huyo ambaye ni mali ya Al Hilal ni raia wa Mauritania ana uwezo wa kukaba na spidi akiwa uwanjani. Taarifa zinaeleza kuwa ameandaliwa mkataba wa miaka miwili awe mrithi wa Zimbwe Jr ambaye anatajwa kupewa ofa na Yanga SC.

Soma hii: Simba SC kufanya usajili mkubwa
Paisha kindege uvune mamilioni
Cheza Aviator sasa hivi hapo ulipo. Ni rahisi sana na mamilioni yanakusubiri. Ushindi unakusubiri sasa hivi.

Mchezaji mwenyewe inaelezwa yupo tayari kucheza ndani ya kikosi cha Simba SC. Ikiwa dili lake litajibu atakuwa mrithi wa Zimbwe Jr. Ipo wazi kuwa Zimbwe alikuwa chaguo la kwanza chini ya Fadlu Davids mkataba wake umeisha na hajaongeza mwingine. Baada ya mkataba wa Zimbwe Jr kuisha kulikuwa na mvutano kwenye kuongeza mkataba mpya.
Rekodi za Zimbwe Jr

Soma hii: Simba SC yakata tamaa kuhusu Zimbwe Jr
Rekodi zinaonyesha kuwa msimu wa 2024/25 Zimbwe Jr alicheza mechi 27 za ligi. Simba SC ilicheza mechi 30 alikosekana kwenye mechi tatu pekee. Kwenye eneo la ulinzi Simba SC ni namba mbili kwa kufungwa mabao machache ambayo ni 13.
Zimbwe Jr alikuwa kwenye kikosi cha kwanza kilichoeza fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane. Simba SC katika anga la kimataifa iliishia nafasi ya pili. Mabingwa ni RS Berkane walioshinda kwa jumla ya mabao 3-1.
Mrithi wa Zimbwe Jr
Taarifa zinaeleza kuwa beki huyo atakuja Bongo kukamilisha masuala ya kusaini mkataba mpya. Ikumbukwe kwamba kwa sasa ni dirisha la usajili na Simba SC bado haijatambulisha mchezaji mpya. Ikiwa dili lake litakamilika atakuwa mchezaji wa kwanza kutambulisha.
Mbali na mchezaji huyo kuna orodha ndefu ya wachezaji wanaotajwa kuwa katika rada za Simba SC. Ikumbukwe kwamba wapo wachezaji wengine ambao wameachwa na Simba SC. Miongoni mwa wachezaji hao ni Valentino Nouma ambaye alikuwa ni beki wa kushoto.
Hapa tunakuletea orodha ya wachezaji wanaotajwa kuwa kwenye rada za Simba SC. Ni Balla Conte huyu Simba SC haitampata kwa sasa mpaka miaka mitatu iishe. Conte aliyekuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC amesaini mkataba wa miaka mitatu Yanga SC.
Msindo
Beki Pascal Msindo wa Azam FC anatajwa kuwa katika rada za Simba SC. Sababu kubwa ya beki huyo kutajwa ni uwezo wake kwenye kukaba na spidi awapo uwanjani. Kuondoka kwa Zimbwe Jr kunatoa nafasi kwake kuwa chaguo la kwanza ikiwa watampata.
Taarifa zinaeleza kuwa Azam FC wamefunga madirisha kuhusu mchezaji huyo. Beki huyo bado ni mali ya Azam FC kwa kuwa aliongeza mkataba. Ili Simba SC ipate huduma yake ni lazima ivunje mkataba wake.
Feisal Salum – Simba SC

Soma hii: Simba SC wamefungukia kuiwinda saini ya Feisal Salum kiungo wa Azam FC
Nyota Feisal aliibuka Azam FC akitokea Yanga SC. Imekuwa inaelezwa kuwa Simba SC inahitaji huduma. Ni pasi 13 za mabao alitengeneza na kufunga mabao manne msimu wa 2024/25 katika kikosi cha Azam FC kwenye NBC.
Jonathan Sowah- Simba SC
Mshambuliaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC. Nyota huyo ni ingizo jipya kwenye dirisha dogo na alifunga mabao 13. Uwezo wake kwenye kucheka na nyavu unatajwa kuwa sababu ya kuwafanya Simba SC wamfuatilie kwa ukaribu.
Mohamed Hussen Zimbwe Jr
Nahodha Mohamed Hussen Zimbwe Jr aliwaaga Simba SC rasmi Julai 19 2025. Zimbwe alibainisha kuwa miaka 11 ilikuwa yenye furaha na huzuni. Bado anawashukuru Simba SC kwa kuwa pamoja naye kwenye nyakati zote.
Mavambo
Deborah Mavambo alipewa Thank You Julai 19 2025. Nyota huyo alikuwa ni kiungo mkabaji. Amedumu Simba SC kwa msimu mmoja pekee.
Ngoma
Fabrince Ngoma wa Simba SC alitoa Thank You Juni 29 2025. Mkataba wake wa miaka miwili ulikuwa umegota mwisho. Simba SC rasmi walimpa Thank You Ngoma Julai 12 2025.
Omary Omary
Nyota huyu ametolewa kwa mkopo kuelekea Mashujaa. Ni Julai 12 taarifa ilitolewa rasmi. Hivyo hatakuwa na uzi wa Simba SC msimu wa 2025/26.
Air Manula
Aishi Manula, maarufu kwa jina la Air Manula, alipewa Thank You na Simba SC, Julai 12 2025. Kipa huyu msimu wa 2025/26 atakuwa ndani ya kikosi cha Azam FC. Kwa msimu wa 2024/25 hakupata nafasi kikosi cha Simba SC kwenye mechi za ligi.
Valentino Nouma
Nouma alipewa Thank You Julai 12 2025. Huyu ni beki wa kushoto. Ni msimu mmoja pekee amehudumu Simba SC.
Hussen Kazi
Beki Hussen Kazi alipewa Thank You rasmi na Simba SC Julai 13 2025. Hakupata nafasi ya kucheza kwenye mechi za ushindani msimu wa 2024/25. Hivyo atakuwa kwenye changamoto mpya msimu ujao wa 2025/26.
Kelvin Kijili
Alipewa Thank You Julai 13 2025. Beki huyu bado atakuwa kwenye anga la kimataifa. Singida Black Stars walimtambulisha.
Agustine Okejapha
Mchezaji Okejapha alipewa Thank You rasmi na Simba SC Julai 13 2025. Nyota huyu ni msimu mmoja pekee amehudumu ndani ya Simba SC. Akiwa na Simba SC alicheza fainali Kombe la Shirikisho Afrika.
Hitimisho
Simba SC kwenye maboresho kuelekea 2025/26 itasajili beki wa kushoto. Mbali na eneo la ulinzi katika eneo la ushambuliaji kati Leonel Ateba na Steven Mukwala mmoja anatajwa kuachwa hivyo atatambulishwa mshambuliaji mpya. Simba SC haijatoa taarifa yoyote kuhusu usajili wake kuelekea msimu wa 2025/25.


