- Baada ya ‘Tshabalala’ na Conte Yanga SC yashusha straika Boyeli kutoka Afrika Kusini
- Msimu wa 2022/23 Boyeli akiwa na Power Dynamos alibeba tuzo ya kiatu cha mfungaji bora wa ligi ya Zambia.
- Hii ni baada ya kuweka kambani mabao 18, msimu huo Boyeli pia aliibuka na tuzo ya mchezaji bora wa msimu.
Yanga hawapoi, kwani baada ya kukamilisha usajili wa aliyekuwa mlinzi wa kushoto na nahodha wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’. Young Africans wamemtambulisha Balla Conte siku ya Ijumaa. Uongozi wa timu leo umeelezwa kumalizana na straika wa Sekhukhune United ya Afrika kusini hiyo, Andy Boyeli. Soma kwa undani habari mpya za usajili za Yanga SC kwenye makala hii.
‘Kindege’ cha SportPesa kinakupa Mamilioni cheza sasa
Huku ukiendelea kuhabarika na makala hii, unasubiri nini? Shinda mamilioni sasa kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.

Mkataba wa Boyeli na rekodi zake

Taarifa ambayo imeripotiwa na vyanzo mbalimbali ni kuwa Yanga SC wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Andy Bobwa Boyeli. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, ametoka Sekhukhune United ya Afrika Kusini kwa mkopo. Mkataba huo ni wa kipindi cha mwaka mmoja na una kipengele cha mchezaji huyo kununuliwa mazima kwa gharama ya dola 100,000.
Staa huyo alikuwa na wakati mzuri msimu wa 2022/23 akiwa na kikosi cha Power Dynamos ya Zambia. Boyeli alifanikiwa kutwaa kiatu cha mfungaji bora wa ligi ya Zambia baada ya kufunga magoli 18. Kufuatia mafanikio hayo mwishoni mwa msimu, nyota huyo alifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu (MVP).
SOMA HII PIA: Balla Conte amesaini rasmi Yanga SC na kutambulishwa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26
Dili la Sowah na Yanga limeyayuka rasmi
Kufuatia usajili huo wa Andy Boyeli, inaelezwa kuwa uongozi wa Yanga SC umefuta mpango wa kumsajili straika hatari wa Singida Black Stars Jonathan Sowah. Iliripotiwa kwa muda mrefu kuwa Yanga SC walikuwa wanamfukuzia kwa ukaribu Sowah wakihitaji huduma zake. Nyota huyo sasa anatajwa kuwa kwenye rada za watani zao wa jadi klabu ya Simba SC.
Kuhusu utambulisho wa Conte na usajili wa Tshabalala Yanga

Ikumbukwe hivi karibuni Yanga SC walitangaza rasmi kukamilisha usajili wa kiungo Balla Conte. Nyota ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili na kutambulishwa siku ya Ijumaa. Stori ya Conte imekuwa gumzo kubwa kwenye dirisha hili la usajili hasa kwa kuwa ilikuwa ikielezwa kuwa Yanga SC na Simba SC zote zilikuwa vitani kusaka saini ya nyota huyu.
SOMA HII PIA: Mohamed Hussein aaga rasmi Simba atajwa kusaini Yanga, mabosi Msimbazi wamgeukia Kamagate Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26
Conte, Tshabalala vita ilikuwa kubwa na umafia wa kutosha
Kwa mujibu wa taarifa ishu ya Conte, Yanga SC ndiyo ilikuwa timu ya kwanza Bongo kuulizia uwezekano wa kumpata kiungo huyo, kabla ya Simba kumpandia dau. Simba SC ililazimika kuingilia dili la Conte baada ya maelekezo ya kocha wao mkuu, Fadlu Davis. Baada ya vita kubwa kati ya Simba na Yanga, Wananchi walituma ofa kubwa zaidi kwenda kwa Conte na CS Sfaxien. Ofa hiyo ilikubalika na pande hizo mbili, hivyo dili kukamilika pande zote.
Ishu ya Tshabalala na Yanga ikoje?

Yanga na Tshabalala wamemalizana na kilichobaki ni Yanga kumtangaza staa huyo. Baada ya kuwepo kwa mazungumzo ya muda mrefu kutoka kwa pande zote mbili kabla ya kufikia muafaka usiku wa kuamkia jana Jumapili. Tshabalala amesaini mkataba wa miaka miwili kucheza Yanga.
Kufuatia hatua hiyo, Tshabalala amewaaga rasmi Simba na familia nzima ya timu hiyo kwa barua yake rasmi. Barua hiyo aliiweka katika kurasa za mitandao yake ya kijamii. Kama Sehemu ya kuheshimu mchango wa familia hiyo katika maisha yake kwa kipindi cha miaka 11 aliyodumu na kikosini.
SOMA HII PIA: Khadim Diaw mrithi wa Zimbwe Jr Simba SC | Msindo atajwa | Yanga SC hawapoi
Hitimisho
Kutokana na namna timu zinafanya usajili, uzito wa dirisha hili la uhamisho wa wachezaji umeonekana kwa uwazi. Yanga SC wamemalizana na mastaa kama Balla Conte, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Boyeli. Ni wazi kuwa msimu ujao wa 2025/26 unatarajiwa kuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa. Ni wito kwa kila timu kuweka mipango yao sawa kabla ya msimu kuanza, ili kuondokana na uwezekano wa matokeo mabaya.

