- Baada ya Conte Yanga SC yatua kwa Tshabalala wa Simba SC tetesi usajili, Yanga yatishia kuibomoa Simba.
- Inaelezwa Yanga Rasmi wamefungua mazungumzo na Zimbwe, wanajadili ishu za Mshahara, ada ya uhamisho na Bonasi.
- Kama watafikia makubaliano basi Kiongozi wa Yanga atasafiri kwenda Misri kumsainisha mkataba.
Baada ya kutajwa kukamilisha usajili wa staa wa kimataifa wa Guinea, Balla Moussa Conte tetesi za usajili zimethibitisha kuwa uongozi wa Yanga sasa unaelezwa kuwa umemgeukia mlinzi wa kushoto na nahodha wa Simba, Mohamed Hussein maarufu ‘Zimbwe Jr’.
Shinda mamilioni na ‘Kindege’ cha SportPesa

Endelea kuhabarika na makala hii, huku pia ukicheza na kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.
Kuhusu dili la Conte na Yanga

Yanga SC na Simba SC siku chache zilizopita duru za masuala ya usajili ziliwataja kuwa kwenye vuita kali ya kumwania Conte kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26, huku habari hiyo ikiteka kwa ukubwa kwenye tetesi za usajili kuelekea Ligi Kuu NBC msimu ujao.
Conte ni staa wa kimataifa wa Guinea ambaye anakipiga kwenye klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia. Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya usajili, Hans Raphael aliweka wazi kuwa Yanga SC ndiyo ilikuwa timu ya kwanza Bongo kuulizia uwezekano wa kumpata kiungo huyo, kabla ya Simba kumpandia dau baada ya maelekezo ya kocha wao mkuu, Fadlu Davis.
Hans alinukuliwa akiandika: “Kulikuwepo na makubaliano kati ya klabu na klabu (CS Sfaxien na Yanga), ambapo Yanga walipewa ruhusa ya kuzungumza na mchezaji Conte, kabla makubaliano ya mchezaji na Yanga hayajakamilika ndipo usiku Simba walienda na ofa kubwa.
“Kocha mkuu wa Simba, Fadlu alifanya mazungumzo ya moja kwa moja na mawakala wa mchezaji kwa njia ya Simu. Ofa ya Simba kwenda CS Sfaxien ilikuwa ni kubwa sana kuliko Yanga na Fadlu aliendelea kuwapush viongozi wake kumpata kijana kwani ndio chaguo namba moja sokoni.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC vitani usajili wa Conte kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26. Yanga watangaza Tofali la ubingwa
Ofa ya Yanga kwa Conte
Hans aliendelea kusema: “Niko hapa kuthibitisha Yanga wamekamilisha usajili wa kiungo wa CS Sfaxien, Mussa Balla Conte (21) kwa mkataba wa miaka miwili. Baada ya vita kubwa kati ya Simba na Yanga, usiku wa jana Rais wa Yanga alituma ofa kubwa zaidi kwenda kwa Conte na CS Sfaxien.
“Ofa hiyo imekubalika na pande hizo mbili, hivyo asubuhi hii dili limekamilika pande zote. Conte ameahidiwa na Yanga kupewa Gari, Nyumba ya kuishi na mshahara mnono huku akihakikishiwa nafasi ya kucheza kikosini kitu ambacho amekubaliana nacho.
“Simba waliweka ofa mezani ila changamoto walitaka kulipa hela hiyo kwa awamu mbili, kitu ambacho CS Sfaxien wamekataa, hivyo Yanga wamekubali kulipa hela zote kwa Awamu moja na CS Sfaxien wamekubali biashara.
Yanga kuibomoa Simba? Yatua kwa Tshabalala

Baada ya mbilinge hilo la Conte kuisha, imeelezwa kuwa Yanga Rasmi Yanga wamefungua mazungumzo na beki na nahodha wa Simba Mohamed Hussein ‘Zimbwe’. Akizungumzia hilo Hans amesema: “Hivi sasa Yanga wanajadili na Zimbwe issue za Mshahara na Sign on fee na Bonus.
“Niko hapa kuthibitisha dili la Zimbwe na Yanga bado halijakamilika, ila mazungumzo yanaendelea na Kama watafikia makubaliano basi Kiongozi wa Yanga atasafiri kwenda Misri kumsainisha mkataba. Zimbwe kwa sasa ni mchezaji huru, hivyo anaruhusiwa kuzungumza na timu yoyote.”
Hapa inasubiriwa uamuzi wa mwisho wa mchezaji na wakala wake ambaye anafahamika kama Carlos ‘Mastermind’ ndiye anasimamia michakato yote ya kimkataba ya mlinzi huyo ambaye kwa sasa yuko na majukumu ya kikosi cha timu ya taifa kambini Misri kikijiandaa na mashindano ya Chan.
SOMA HII PIA: Kibu Dennis mkandaji wa Simba SC anatajwa kupata timu Marekani | Bosi abainisha
Hitimisho: Yanga mipango mikubwa ya maandalizi ya msimu 2025/26

Ukiachana na mipango mikubwa ya usajili ambayo Yanga wanaendelea nayo, uongozi wa timu hiyo pia umejitanabaisha kuwa kwenye mipango mikubwa ya maandalizi ya msimu ujao wa 2025/26, huku miongoni mwa mipango hiyo ikiwa ni maandalizi ya kabla ya msimu ‘Pre Season’ ambapo uongozi wa timu hiyo umethibitisha safari ya Rwanda.
Akizungumzia hilo Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema: “Tutakuwa na Yanga imara itakayofanya maandalizi bora kuanzia Pre Season mpaka kutimiza malengo yetu kwa msimu mzima. Nataka kuwaambia kuwa tumejipanga vizuri kuhakikisha tunatetea ubingwa msimu ujao.”

