Mzee SamattaMzee Samatta
  • Chanzo kifo cha Mzee Samatta kimeelezwa na Mtoto Mkubwa wa familia ambaye ameweka wazi mazishi kufanyika leo Kibiti.
  • Katika kusimamia nidhamu za watoto wake kwenye soka, Mzee Samatta aliamuru malipo ya shilingi 5,000 hadi 10,000 kwa kila penalti ambazo wanakosa.
  • Kampuni ya SportPesa kama mdau mkubwa wa michezo nchini tuko pamoja nanyi katika kipindi hiki cha majonzi.

Hofu na huzuni zimetanda mitaa ya Mbagala, Dar es Salaam, baada ya kutolewa taarifa za kifo cha baba wa mshambuliaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta, huku familia ikieleza maradhi ya Sukari ambayo yamemsumbua kwa muda kuwa chanzo kifo cha Mzee Samatta.

Kuhusu kifo cha Mzee Samatta

Mzee Samatta
Mzee Samatta

Jana Jumapili asubuhi,Familia ya mzee Samatta kupitia kwa mtoto wake, Mohammed Samatta waliweka wazi kufikwa na msiba wa mzee wao uliotokea nyumbani kwake Mbagala Dar es Salaam. Mzee Ally Samatta akisumbuliwa na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yakimkabili kwa muda.

Kupitia kwa Mtoto wa kwanza wa Mzee Samatta aitwaye Rajabu amesema baba yao alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Sukari. Rajabu ameendelea kusema: “Kabla ya kifo chake Mzee Samatta alipata changamoto ya Sukari na kupelekwa hospitali ambapo alipatiwa matibabu lakini hali yake ikaendelea kuzorota na umauti kumfika.”

Alikuwa shabiki mkubwa wa watoto wake

Mbwana Samatta
Mbwana Samatta

Mzee Ally Samatta aliyejulikana kuwa na msimamo mkali juu ya utii na nidhamu, alikuwa ni mnyenyekevu na baba mwenye busara. Aliupenda sana mpira akiwa miongoni mwa wachezaji katika miaka ya 1960 na zaidi sana alikua shabiki namba 1 wa mtoto wake.

SOMA HII PIA: Aziz Ki atarejea Yanga SC | Wydad Casablanca kumtema | Tetesi za usajili

Awalipisha watoto wake 5,000 au 10,000 kwa kila Penalti wanayokosa

Mzee Samatta ana vijana wawili ambao wanacheza soka la ushindani akiwemo Mbwana Samatta, anayecheza soka la kulipwa nchini Ugiriki na Mohammed Samatta ambaye yupo hapa nchini kwa sasa akiwa hana timu lakini amecheza kwa mafanikio makubwa timu kadhaa za Ligi Kuu ya NBC.

Katika kusimamia nidhamu za watoto wake ili wazidi kufanya vizuri katika michezo wanayocheza, Mzee Samatta alikuwa akitilia mkazo kupiga penalti kwa ustadi kiasi cha kuamuru malipo ya shilingi 5,000 hadi 10,000 kwa kila penalti ambazo wanakosa.

Mzee Samatta alikuwa ni mtu wa kuheshimika na kupendwa si tu, ndani ya familia yake, bali pia ndani ya jamii nzima ya soka na ndiyo maana waombolezaji mbalimbali wakiwemo watu maarufu, wameonyesha kuguswa na msiba huo na kutuma salamu za pole kwa familia.

Mchango wa Mzee Samatta kwenye mafanikio ya Mbwana Samatta

Mbwana na Baba yake
Mbwana na Baba yake

Mbwana Samatta, anayejulikana kama ‘Samagol’, anafanya vyema soka katika anga za kimataifa amekuwa nahodha wa Taifa Stars, na kufanikiwa kuandika historia mbalimbali ikiwemo ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza Ligi Kuu ya Uingereza na Aston Villa.

Hata hivyo, nyuma ya mafanikio haya, wamekuwepo wazazi waki hususani baba yake mwenye busara aliyeongoza shughuli pia za malezi yake ya awali ya soka. Mchango wake ni wa thamani, akichangia nidhamu, ari, uongozi na dira kubwa katika maisha ya kijana wake.

SOMA HII PIA: Dickson Job kusaini mkataba mpya | Bosi Yanga SC afunguka | Simba SC walipata tabu

Mastaa wa soka wajitokeza

Kufuatia msiba huo viongozi mbalimbali wa soka, Serikali na wachezaji wenzake wamefika msibani kwa ajili ya kutoa faraja na salamu za rambirambi. Baadhi ya mastaa hao ni Thomas Ulimwengu, Himid Mao na viongozi akiwemo makamu Rais wa TFF, Athumani Nyamlani na wengine wengi.

Kuzikwa Kibiti leo

Chanzo kifo cha Mzee Samatta
Mbwana

Mwili wa Mzee Samatta unatarajia kupumzikwa kwao Kibiti ambapo ndipo kuna makaburi ya familia hususani wazazi wa mzee Samatta, na maelekezo ya mzee Samatta alitaka akifariki basi akazikwe huko.

Hitimisho

Katika hali ya ujumla kifo cha Mzee Ally Samatta ni kidonda chungu ndani ya hadithi nzuri nay a kipekee ya familia ya Samatta. Lakini kwa huruma yake, busara yake na mchango alioacha, urithi wake utaendelea kuishi katika maisha ya Mbwana na ndugu zake.

Watanzania wanaungana kwa mazishi yenye huzuni, na matumaini ya kuendeleza darasa aliyoweka mzizi, hasa kuhusu nidhamu na maarifa ya mchezo. Familia ya Samatta sasa inahitaji sana dua na msaada wa kijamii na maalumu sadaka ya upendo wa baba umeachwa kama zawadi ya milele.

Hakika, dunia ya soka imepoteza sauti ya mlinzi lakini kwa. Apumzike kwa amani, baba aliyeachia urithi wa thamani. Pole kwa Wanafamilia na Kampuni ya SportPesa kama mdau mkubwa wa michezo nchini tuko pamoja nanyi katika kipindi hiki cha majonzi na tunawasihi muendelezee urithi mzuri wa familia yenu.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.