- Dickson Job kusaini mkataba mpya kwa ajili ya kuvuja jasho ndani ya kikosi cha Yanga SC msimu wa 2025/26 ligi ya NBC.
- Mkataba wake unakaribia kugota mwisho, mwenyewe afunguka hali ilivyo na kinachoendelea kwa sasa.
- Simba SC walipata tabu mbele ya Job walipokutana msimu wa 2024/25 kwenye mechi za ushindani ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika.
Dickson Job kusaini mkataba mpya Yanga SC kutokana na kiwango alichonacho. Job alijiunga na Yanga SC Januari 11 2021 akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro. 2022/23 alitwaa tuzo ya beki bora wa ligi. Mkataba wake na Yanga SC unakwenda kugota mwisho kwa mujibu wake yeye mwenyewe.
Cheza kindege uvune mamilioni sasa hivi
Sasa hivi unanafasi yakuvuna mamilioni hapo ulipo. Ni rahisi sana, cheza kindege uvune mamilioni yako. Ni Aviator, cheza kila siku uwahi mgao wa mamilioni.


Soma hii: Yanga SC inaongoza orodha ya timu zilizofungwa mabao machache
Msikie Job mwenyewe akifunguka
Juni 29 2025 mara baada ya fainali ya CRDB Federation Cup dhidi ya Singida Black Stars, Job alisema kuwa mkataba wake umeisha. Katika mchezo huo Yanga SC ilishinda mabao 2-0. Ilitwaa taji hilo mbele ya wapinzani wao.
“Kikubwa tusubiri kwa sababu ninakwenda kumaliza mkataba hayo mengine yakiwa sawa kila mtu atajua. Kila kitu kinawezekana. Kikubwa ni maelewano na mazungumzo mazuri,” alisema Job.
Yanga SC ni namba moja
Yanga SC ni namba moja kwa timu ambazo zimefungwa mabao kidogo ndani ya ligi. Msimu wa 2024/25 wa NBC ni mabao 10 timu hiyo ilifungwa. Kipa namba moja ni Djigui Diarra.
Diarra alikuwa akifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na mabeki wa timu hiyo wakiongozwa na Dickson Job. Alikusanya jumla ya hati safi 17. Ni kipa namba mbili kukusanya hati safi nyingi ndani ya ligi.
Kinara kwenye eneo hilo ni Moussa Camara wa Simba SC. Camara ana hati safi 19. Katika hati hizo Camara alikwama kukusanya mbele ya Yanga SC. Kwenye Kariakoo Dabi mechi zote mbili ambazo ni dakika 180 alitunguliwa.

Soma hii: Dickson Job beki wa Yanga SC anatajwa Simba SC
Yanga SC vs Simba SC
Yanga SC kwa msimu wa 2024/25 safu yao ya ulinzi ilikuwa imara mbele ya Simba SC. Kwenye mechi mbili za ligi walizokutana hawajafungwa bao na watani zao wa jadi kwenye Kariakoo Dabi. Jumla ni mabao matatu yalikusanywa huku Simba SC ikifungwa nje ndani.
Safu ya ushambuliaji ya Yanga SC iliwafunga Simba SC mabao matatu. Safu ya ushambuliaji ya Sima SC ilikwama kupita ngome ya Yanga SC inayoongozwa na Dickson Job.
Katika mataji, Simba SC iliambulia patupu na Yanga SC ilitwaa mataji matano. Muungano Cup, Toyota Cup, CRDB Cup, Ngao ya Jamii na Ligi Kuu ya NBC.
Rekodi za Job 2024/25

Soma hii: Yanga SC haina utani kuelekea 2025/26 kuwapiga pini mastaa
Dickson Job alikuwa chaguo la kwanza msimu wa 2024/25. Ni chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi aliyekuwa mchora ramani ya mipango. Mchezo wa mwisho kwa Miloud ambaye amepewa Thank You ilikuwa ni CRDB Federation Cup dhidi ya Singida Black Stars.
Katka mchezo huo Job alianza kikosi cha kwanza. Baada ya dakika 90 kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, ubao ulisoma Yanga SC 2-0 Singida Black Stars. Ubingwa ulikuwa ni mali ya Yanga SC.
Yanga SC ilitwaa ubingwa wa ligi ya NBC ikiwa na pointi 82 kwenye mechi 30 ambazo ni dakika 2,700. Job alicheza jumla ya mechi 26. Ni dakika 2,252 Job alikumba uwanjani.
Ni mechi nne pekee alikosekana ndani ya msimu ambazo ni dakika 360 ndani ya uwanja. Miongoni mwa mchezo ambao aliukosa ilikuwa dhidi ya Tabora United. Mchezo huo ulichezwa Aprili 2 2025, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Tabora United 0-3 Yanga SC. Pointi tatu zilikuwa ni mali ya Yanga SC. Kwenye mzunguko wa kwanza, Yanga SC 1-3 Tabora United, hivyo wababe hawa waligawana pointi tatutatu.
Job na kufunga ndani ya Yanga SC
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Job alikuwa mfungaji wa bao la kwanza kwenye ligi ndani ya Yanga SC. Bao hilo alifunga kwenye mchezo dhidi ya KMC. Ilikuwa ni Uwanja wa Azam Complex Yanga SC ilipotwaa pointi tatu.

Mwisho wa msimu Yanga SC ilimaliza ikiwa imetupia mabao 71. Katika mabao hayo 71 Job bao alilofunga ilikuwa ni moja pekee. Yote hii inatokana na nafasi ambayo anacheza yeye ni beki.
msimu wa 2024/25 umegota mwisho bila yeye kufunga. Mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Yanga SC alikuwa ni Maxi Nzengeli. Ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.
Kuhusu mkataba wake ndani ya Yanga SC
Taarifa zinaeleza kuwa Yanga SC inahitaji kuendelea kupata huduma ya Dickson Job jambo ambalo limefanya mabosi wa timu hiyo kufanya naye mazungumzo. Katika mazungumzo hayo Yanga SC inahitaji kumpa kandarasi ya miaka miwili. Hivyo ni suala la muda beki huyo taarifa zake kuwa wazi kuhusu kuongeza mkataba mpya.
Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe aliweka wazi kuwa kwa mchezaji ambaye wanahitaji huduma yake itakuwa ngumu kuodoka kwenye kikosi hicho. Kamwe aliongeza kuwa kila mchezaji ndani ya kikosi hicho thamani yake ni kubwa. Nukuu hiyo inaondoa ugumu wa Job kuondoka hapo.
“Ikiwa mchezaji tunahitaji huduma yake basi tutaweka hela ili abaki. Unakumbuka kuhusu Aziz Ki? Kuna timu zilikuwa zinamuhitaji lakini tukamuongezea mkataba.
“Ambacho tunakifanya ni kuboresha kikosi chetu. Ni kama nyumba vile unaona kuna sehemu hakupo imara unaboresha. Sio kuanza kujenga timu hiyo hatua tayari tumeshatoka.”
Hitimisho
Job ni miongoni mwa mabeki wenye utulivu mkubwa ndani ya uwanja katika kutimiza majukumu yake. Nyota huyo alikuwa anatajwa kuwa kwenye hesabu za watani wa jadi Simba SC ambao walipishana na saini yake. Kuna uwezekano mkubwa akasalia Jangwani kutokana na kiwango alichoonesha msimu uliopita wa 2024/25 ndani ya Ligi Kuu ya NBC.


