- Yanga SC inaongoza orodha ya timu zilizofungwa mabao machache Ligi Kuu Tanzania NBC 2024/25 ikiwa imefungwa mabao 10 tu.
- Simba SC imefungwa mabao 13 katika hayo matatu imefungwa na Yanga SC ikipoteza mechi zote mbili ndani ya dakika 180
- JKT Tanzania rekodi zao zina maajabu, idadi ya mabao waliyofunga ni 27 ni sawa na mabao waliyofungwa ikiwa ndani ya tano bora zilizofungwa mabao machache.
Yanga SC inaongoza orodha ya timu zilizofungwa mabao machache Ligi Kuu Tanzania NBC 2024/25. Baada ya mechi 30 timu hiyo inayofundishwa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ni mabao 10 yaliokotwa kwenye nyavu zao. Simba SC ambao ni watani wa jadi ni timu namba mbili kufungwa mabao machache ambayo ni 13. Katika mabao hayo 13 ilifungwa mabao matatu na Yanga SC zilipokutana katika Kariakoo Dabi.


Ipo wazi kwamba Yanga SC ilitwaa ubingwa wa NBC ikiwa na pointi 82 na Simba SC nafasi ya pili na pointi 78. Timu zote zimecheza mechi 30 ambazo ni dakika 2,700. Kwa upande wa mabeki wa Yanga SC Dickson Job ni chaguo la kwanza la Miloud Hamdi wa Yanga SC akiwa amecheza jumla ya mechi 26 akikosekana kwenye mechi nne.
Sio Simba SC na Yanga SC orodha ni kubwa kwa timu zilizofungwa mabao machache. Hapa tunakuletea rekodi ya timu hizo ndani ya ligi ambayo ni namba nne kwa ubora. Hizi hapa na mabao waliyofungwa namna hii:-
Yanga SC – 10
Kwenye msimamo wa ligi Yanga SC ni namba moja chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Beki kiongozi ni Dickson Job timu hiyo imeruhusu jumla ya mabao 10 kufungwa msimu wa 2024/25 ikiwa ni timu namba moja kufungwa mabao machache kwenye ligi namba nne kwa ubora Afrika. NBC Premier League wakiwa ni mabingwa.
Safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Clement Mzize na Prince Dube ambao ni washambuliaji imetupia mabao 83. Mzize ana mabao 14 na Dube ana mabao 13. Ni wazi kwamba Yanga SC imefunga msimu ikiwa ni timu namba moja kufunga mabao mengi.
Timu hiyo ambayo Juni 30 2025 ilifunga kwa Paredi la Ubingwa la Kihistoria ina mataji 31 ya ligi. Ni mataji matano ilitwaa msimu wa 2024/25. Toyota Cup, Ngao ya Jamii, Muungano Cup, Ligi Kuu Bara ya NBC na CRDB Federation Cup.
Simba SC-13

Soma hii: Yanga SC waifunika Dar kwa Paredi la ubingwa la kihistoria
Hii ni namba mbili kwenye msimamo na Simba SC ni namba mbili kwa timu iliyoruhusu mabao machache. Ukuta wat imu hiyo umeokota jumla ya mabao 13 kwenye nyavu za Moussa Camara. Mabao yote hayo langoni alikuwa Camara kwenye mechi za ushindani.
Camara amefunga msimu akiwa kinara wa hati safi. Baada ya kukaa langoni kwenye mechi 28 ni hati safi 19 kakusanya. Mbele ya Yanga SC msimu wa 2024/25 mechi zote alitunguliwa walipokuwa kwenye msako wa pointi tatu muhimu.
Baada ya kucheza mechi 30 ambazo ni dakika 2,700 ilipoteza mechi mbili. Ilikuwa Yanga SC mzunguko wa kwanza na ule wa pili. Kwenye mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga SC. Pointi tatu zilikuwa za Yanga SC mzunguko wa pili Kariakoo Dabi Juni 25 2025 ilikuwa Yanga SC 2-0 Simba SC.
Azam FC-19

Soma hii: Tetesi usajili ligi Kuu ya NBC 2025/26 wanaoondoka Yanga hawa hapa – SportPesa Tanzania
Matajiri wa Dar, Azam FC kwenye msimamo wa ligi wamekusanya pointi zao 63 nafasi ya tatu na pia kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache ndani ya ligi ni namba tatu ikiwa imeruhusu mabao 19 pekee kwenye mechi 30. Ndani ya dakika 2,700 Azam FC safu ya ushambuliaji imetupia mabao 56.
Timu hiyo ilikuwa kwenye ushindani mkubwa na Singida Black Stars ambayo imegotea nafasi ya tatu. Mbio za ubingwa zilikwama ni mashuhuda Yanga SC wakiwa ni mabingwa. Kwenye CRDB Federation Cup pia walikwama kutinga hatua ya fainali.
Singida Black Stars-26
Ndani ya nne bora ukiwa ni msimu bora kwao. Ni uhakika kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika. Singida Black Stars inatumia Uwanja wa Liti kwa mechi za nyumbani. Jumla imefungwa mabao 26.
Timu hiyo inaingia kwenye orodha ya timu zilizokuwa katika ubora msimu wa 2024/25. Ni miongoni mwa timu ambazo zimefungwa mabao machache. Imegotea nafasi ya nne ikiwa na pointi 57 kibindoni.
JKT Tanzania-27
Wajeda hawa ndani ya ligi wameonyesha ushindani mkubwa kwenye mechi ambazo wanacheza ndani ya uwanja. Itakumbukwa mechi yao ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Simba SC, Uwanja wa KMC Complex walikaza na dakika za jioni Simba ikapata penalty na mtupiaji alikuwa Jean Ahoua dakika ya 90.
JKT Tanzania ni mabao 27 imefungwa ikiwa namba tano kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache kwenye msimamo ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi zake 36 ndani ya msimu wa 2024/25. Ipo ndani ya 10.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya sita ndani ya ligi namba nne kwa ubora. Ni timu pekee iliyovuna pointi moja mbele ya Yanga SC msimu wa 2024/25. Rekodi zinaonyesha kuwa Yanga SC amba oni mabingwa kwenye mechi 30 sare ilikuwa moja pekee ilikuwa JKT Tanzania 0-0 Yanga SC.
Coastal Union-31
Kutoka Tanga ikiwa inatumia Uwanja wa Mkwakwani, Coastal Union ni namba tano. Timu hiyo baada ya mechi 30 imeruhusu mabao 31. Nafasi yake kwenye msimamo ni 8 ikiwa na pointi 35.


