KenGold FC vs Simba SCKenGold FC vs Simba SC
  • KenGold FC vs Simba SC ‘live’, hii ni zaidi ya mechi bali ni moto ambao utawaka kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi katika kusaka pointi 3.
  • Katika mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulipigwa Desemba 18, mwaka jana 2024 Simba walishinda mabao 2-0
  • Mpaka sasa kwenye msimamo wa ligi Kuu Bara, Simba SC wamekusanya pointi 72 katika michezo 27 waliyocheza.

Saa chache zijazo Umma wa wapenda soka la Bongo, wanakwenda kushuhudia mfululizo wa mechi kali za Ligi Kuu Bara ‘NBC Premier League’, huku pale Tabora moto utawaka kwa mechi ya KenGold FC vs Simba SC ‘live’.

Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB

Kuhusu mechi ya KenGold FC vs Simba SC ‘live’

Huu ni mchezo wa mzunguko wa 28 wa Ligi Kuu Bara kwa Simba SC lakini unakuwa mchezo wa mzunguko wa 29 kwa KenGold FC ambao wanauendea mchezo huu wakiwa hawana cha kupoteza mara baada ya kushuka daraja.

Mpaka sasa kwenye msimamo wa ligi Kuu Bara, Simba SC imeachwa na Yanga SC kwa pointi moja kwenye msimamo Yanga wakiwa kileleni na pointi zao 73 walizokusanya katika michezo 27, huku Simba SC wao wakikusanya pointi 72 katika michezo 27 waliyocheza.

Utofauti wa pointi hiyo moja ndio ambao umezidi kuchochea vita ya ubingwa msimu huu, ambapo mpaka sasa kama timu zote zikishinda michezo yao iliyosalia basi matokeo ya mchezo wa dabi ya Kariakoo ya Juni 25, mwaka huu huenda ikaamua bingwa.

SOMA HII PIA: Simba SC vs RS Berkane 25/5/2025 live: H2H, uchambuzi, vikosi hivi hapa, Simba kubeba ubingwa?

Matokeo ya mchezo wa mzunguko wa kwanza yalikuwaje?

KenGold FC vs Simba SC
KenGold FC vs Simba SC

Wakiongozwa na kocha wao mkuu mpya Msauzi, Fadlu Davids Simba SC wanawaendea KenGold FC wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, katika mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex Desemba 18, mwaka jana.

Mchezo dhidi ya KenGold unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ikiwa ni mzunguko wa pili. Wakati huu kila timu inamalengo yake, KenGold wenyeji mpango mkubwa ni kulipa kisasi, huku Simba SC wao wakisaka pointi 3 muhimu za ubingwa.

Simba SC wakiwa Tabora, huku  watani zao wa jadi na mabingwa watetezi wa mashindano hayo Yanga SC nao watakuwa uwanjani kwenye  kazini Juni 18 kwenye msako wa pointi tatu dhidi ya Tanzania, Prisons, huko jijini Mbeya.

SOMA HII PIA: JKT Tanzania FC Vs Simba SC 5/5/2025: Mabosi Simba wafanya kikao kizito cha Ubaya ubwela

Msimamo unasemaje kuhusu KenGold vs Simba SC

Wenyeji KenGold kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 28 msimu wa 2024/25. Nafasi iliyopo kwa KenGold inathibitisha kuwa tayari wameshuka daraja na haitakuwa na nafasi kushiriki ligi msimu wa 2025/26.

Simba SC wao wapo nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi 72 baada ya mechi 27 ikiwa inapambania kutwaa ubingwa mbele ya Yanga SC ambao ni vinara wenye pointi 73. Tofauti ya wababe hawa wawili ni pointi moja pekee wakiwa wamecheza mechi sawa.

Kwa upande wa mabao Simba SC imefunga mabao 63, inakutana na KenGold ambayo imefunga jumla ya mabao 22. KenGold rekodi zinaonyesha kuwa safu yake ya ushambuliaji haijawa imara kwenye mechi za ushindani.

Ukiachana na kufunga mabao machache KenGold imeruhusu mabao 52 yakufungwa, ikiwa ni timu namba mbili kuruhusu mabao mengi yakufungwa ndani ya ligi vinara wakiwa ni Fountain Gate ambao wameruhusu jumla ya mabao 54.

Kwa upande wa Simba SC ni timu namba mbili kuruhusu mabao machache ambayo ni 11 baada ya mechi 27. Mabao yote hayo katunguliwa kipa namba moja, Moussa Camara ambaye kacheza jumla ya mechi 25 huku mechi mbili tu ndio, Ally Salim alikaa langoni.

Hitimisho: Walichosema Simba kuelekea mchezo wa leo

Akizungumzia mchezo huo kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema: “Tunatarajia mchezo mgumu kwa kuwa tunakwenda kucheza na timu ambayo tayari imeshuka daraja, wao hawana cha kupoteza lakini sisi tunahitaji zaidi pointi 3 za mchezo huu.

“Tutapambana kuhakikisha tunapata matokeo kwa kuwa tunatofautiana pointi moja na vinara wa msimamo Yanga na kama tunataka kushinda ubingwa ni lazima tushinde mechi zote zilizobaki.”

Ikumbukwe mchezo wa mwisho wa ligi Simba walifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars. Mchezo huu ulipigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, goli pekee la Steve Mukwala na asisti ya Ahoua.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.