- Man City vs Wydad AC 18/06/2025 ni zaidi ya mchezo wa Kombe la Dunia la klabu, hii ni vita ya kupinga ukoloni wa soka.
- Haya sio mashinado mapya, yamekuwa yakifanyika kila mwaka, lakini msimu huu yameboreshwa kuna nyongeza ya timu kutoka timu 7 hadi 32.
- Watanzania wanasubiri kwa hamu kuwashuhudia mastaa Aziz Kin a Selemani Mwalimu dhidi ya Guardiola .
Mbungi ya kufa mtu inatarajiwa kupigwa leo Jumatano nchini Marekani katika mchezo wa mashindano ya klabu bingwa dunia, kupitia mchezo wa Man City vs Wydad AC 18/06/2025, ambapo staa wa kimataifa wa Zamani wa Yanga, Azizi Ki atakutana ana kwa ana na kocha, Pep Guardiola na mastaa wengine wa City.
Man City ndio mabingwa watetezi

Manchester City wanarejea kwenye Kombe la Dunia la Klabu la FIFA kama mabingwa watetezi, wakishiriki katika mashindano ambayo yamebadilika sana. Ikumbukwe mnamo Desemba 2023, kikosi cha Pep Guardiola aliiongoza City kuicharaza Fluminese kipigo cha mabao 4-0.
City katika hatua ya Nusu Fainali ya mashindano ya msimu uliopita kilishinda na kuwaondosha Urawa Red Diamonds katika nusu fainali kabla ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fluminense kwenye fainali iliyofanyika Jeddah, Qatar.
SOMA HII PIA: Yanga na kocha Rulani Mokwena nini kinaendelea?
Mfumo mpya kutoka timu 7 hadi 32

Mashinado hayo sio mapya yamekuwa yakifanyika kila mwaka, lakini msimu huu yameboreshwa na kuwa kwenye aina mpya ya uendeshaji. Msimu huu kuna nyongeza ya timu kutoka timu 7 hadi 32 ambapo pia yanatarajiwa kuendelea kwa kwa kipindi kirefu cha mwezi mmoja nchini Marekani.
Baada ya msimu wa 2024/25 uliokuwa wa kuvunja moyo kwa Guardiola ambaye hakushinda taji lolote kwa mara ya kwanza tangu msimu wake wa kwanza alipojiunga na City mwaka 2016/17, na anasubiriwa kuwaona namna gani atawatumia wachezaji wake wapya watatu waliosajiliwa mpaka sasa.
Kuna pia wachezaji muhimu ambao hawakusafiri pamoja na mabadiliko ya benchi la ufundi, ishara kuwa huu unaweza kuwa mwanzo wa zama mpya kwa mabingwa hao wa England mara 10, lakini kama atafanya vibaya basi huenda tukaiona sura ya mwisho ya Guardiola baada ya karibu muongo mmoja madarakani.
wako tayari kuanza safari yao dhidi ya vigogo wa Morocco, Wydad AC, katika Kundi G.
Man City vs Wydad AC: Vikosi vinavyotarajiwa, habari za Vikosi

Viungo washambuliaji Rayan Cherki, Tijjani Reijnders na beki wa kushoto Rayan Ait-Nouri walijiunga na City katika dirisha la uhamisho kabla ya mashindano na wameshiriki kikamilifu kwenye kambi ya mazoezi ya Guardiola. Huenda wote wakaanza dhidi ya Wydad.
Kwa kuwa Rodri amerejea na yuko fiti baada ya upasuaji wa goti (ACL) mwezi Septemba uliopita, Guardiola ana chaguzi nyingi katikati ya uwanja. Hata hivyo, Mateo Kovacic hatakuwepo baada ya kufanyiwa upasuaji wa kisigino (Achilles).
Jack Grealish na Kyle Walker hawako kwenye kikosi, jambo linaloashiria mwisho wa safari yao ndani ya klabu hiyo. James McAtee pia anatarajiwa kuondoka, na amechagua kujiunga na kikosi cha England cha chini ya miaka 21 badala ya kusafiri na klabu.
Kikosi cha Man City kinachotarajiwakuanza
Katika mfumo wa 4-2-3-1, kikosi cha City kinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo; Ederson (GK) Nunes, Dias, Gvardiol, Ait-Nouri, Rodri, Reijnders, Foden, Cherki, Marmoush na Haaland. Ikumbukwe majeruhi: Kovacic (kisigino), na hakuna waliosimamishwa.
Kikosi kamili cha Man City:
Makipa: Marcus Bettinelli, Stefan Ortega, Ederson
Mabeki: Ruben Dias, John Stones, Nathan Ake, Rayan Ait-Nouri, Vitor Reis, Josko Gvardiol, Manuel Akanji, Matheus Nunes, Abdukodir Khusanov, Rico Lewis
Viungo: Tijjani Reijnders, Nico Gonzalez, Rodri, Ilkay Gundogan, Bernardo Silva, Nico O’Reilly
Washambuliaji: Omar Marmoush, Erling Haaland, Jeremy Doku, Savinho, Rayan Cherki, Claudio Echeverri, Phil Foden, Oscar Bobb
Kikosi cha Wydad AC

Nordin Amrabat, winga mkongwe wa zamani wa Watford, ni uso unaofahamika kwa mashabiki wa City akiwa upande wa Wydad AC. Sasa akiwa na miaka 38, Amrabat amejiunga na kikosi cha Mohamed Amine Benhachem baada ya mkataba wa muda mfupi na Hull City kuisha.
Mohamed Rayhi, kijana wa zamani wa PSV, alikuwa mfungaji bora wa Wydad msimu uliopita akiwa na mabao 11. Kikosi cha Wydad AC kinachotarajiwa kuanza huku wakitumia mfumo wa 4-2-3-1, ni kama ifuatavyo: El Motie (GK) — Moufi, Meijers, Harkass, Boucheta, Malsa, Moubarik —Amrabat, Arthur, Rayhi, Obeng.
Kikosi kamili cha Wydad AC:
Makipa: Omar Aqzdaou, El Mehdi Benabid, Youssef El Motie
Mabeki: Abdelmounaim Boutouil, Ayoub Boucheta, Guilherme Ferreira, Jamal Harkass, Bart Meijers, Fahd Moufi, Mohamed Moufid
Viungo: Arthur, Stephane Aziz Ki, Ismail Benktib, Yassine Bennani, Rayane Mahtou, Mickael Malsa, El Mehdi El Moubarik, Ismail Moutarajji, Pedrinho, Oussama Zemraoui
Washambuliaji: Omar Alsomah, Nordin Amrabat, Zakaria Fathi, Hamza Hannouri, Thembinkosi Lorch, Cassius Mailula, Selemani Mwalimu, Samuel Obeng, Mohamed Rayhi
Hitimisho: Utabiri wa matokeo Man City vs. Wydad AC

Mwisho wa msimu uliopita, Guardiola alirejesha uthabiti kwenye timu ya City ambayo hapo awali ilikuwa dhaifu. Walipoteza mechi moja tu baada ya mapumziko ya kimataifa ya Machi, ingawa mechi hiyo ilikuwa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Crystal Palace.
Kwa kuongezewa vipaji vipya vya ushambuliaji na nyota kama Erling Haaland na Phil Foden waliopata muda wa kupumzika, huenda City wakarejea na ule mtindo wao wa kucheza kwa kujiamini na inatarajiwa huenda matokeo yakawa kama ifuatavyo.

