Jean Ahoua (-)Jean Ahoua (-)
  • Yanga SC ilianza kwa kusuasua eneo la ufungaji ilipojipata balaa lake lilikuwa zito kwa kushusha dozi kubwa kwa wapinzani wao ndani ya uwanja.
  • Simba SC deni lake kwa sasa ni mabao 8 ikiwa ni tofauti yao dhidi ya Yanga SC zote zikiwa zimecheza mechi ambazo zinalingina idadi.
  • Kariakoo Dabi mzunguko wa kwanza Simba SC ilipoteza ndani ya dakika 90 kwa kushuhudia ubao ukisoma Simba SC 0-1 Yanga SC.

Yanga SC vs Simba SC deni lao hawa watani ni kubwa kwenye eneo la ushambuliaji kutokana na kasi waliyonayo Yanga SC inayoongoza ligi na eneo la ushambuliaji inaongoza katika kasi ya kufunga mabao mengi kwa msimu wa 2024/25 ambao una ushindani mkubwa kila idara.

Miloud Hamdi
Miloud Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika, Yanga SC kwenye idara ya ushambuliaji ni namba moja kwenye kufunga mabao mengi kati ya timu 16. Kigezo hiki kinaongeza hali ya ushindani kwenye vita ya ubingwa huku Simba SC ikiwa ni namba mbili kwenye msimamo na timu iliyofunga mabao mengi.

Soma na hii:Yanga SC vs Simba SC inayodhamiriwa Juni 15 2025 Dabi ya Kariakoo mechi ipo, au haipo?

Mabao ya Yanga SC kwenye ligi

Ni mabao 71 safu ya ushambuliaji ya Yanga SC inayoongozwa na Prince Dube imefunga ndani ya ligi ikiwa ni timu yenye mabao mengi kwa sasa huku ikiwa namba moja kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache uwanjani.

Clement Mzize na Dube
Clement Mzize na Dube washambuliaji wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Baada ya kucheza jumla ya mechi 27 ambazo ni dakika 2,430 safu ya ushambuliaji ya Yanga SC imetupia mabao 71 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 34 kwenye mechi za ushindani ndani ya ligi.

Ikumbukwe kwamba ni timu namba moja ambayo imepata ushindi mkubwa kwenye mechi zake ikipata ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya KMC na iliwatungua mabao 6-1 Ken Gold kwenye mechi za ligi zote zilichezwa Uwanja wa KMC, Complex.

Wakati ikiwa namba moja kwenye ligi na pointi zake 73 kibindoni, watani zao wa jadi Simba wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa namba mbili kwa timu yenye mabao mengi ikiwa imetupia mabao 63 baada ya kucheza mechi 27 na pointi zao ni 72.

Katika dakika 2,430 ilizocheza imekuwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 38 ndani ya uwanja. Mkali wakutupia ndani ya kikosi cha Simba SC ni kiungo mshambuliaji Jean Ahoua mwenye mabao 15 ndani ya ligi.

Mabao ambayo Simba SC anadaiwa na Yanga SC

Deni ambalo Simba SC inalo kwa Yanga SC kwenye eneo la kutupia ni mabao 8 ambayo ni tofauti yao kwa sasa ndani ya ligi. Safu ya ushambuliaji ya Simba SC imekwama kufikia idadi hiyo ya mabao baada ya timu zote kucheza mechi sawa.

Jean C- Ahoua
Jean C- Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC. Source: Simba SC.

 Hivyo kwenye vita ya kuwania ubingwa ikiwa watalingana pointi kuna nafasi kubwa Yanga SC kutwaa taji kwa kigezo cha tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Ushindi mkubwa kwa Simba SC

Mchezo wa kwanza ambao Simba ilipata ushindi mkubwa ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar walipopata ushindi wa mabao 5-2 llikuwa Uwanja wa Kaitaba ikiandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kupata ushindi mkubwa ndani ya msimu wa 2024/25.

Machi 14 2025, Simba ilipata ushindi mkubwa wa pili baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 6-0 Dodoma Jiji, kwenye mchezo huu nyota Jean Ahoua alikosa nafasi mbili za wazi na Kibu Dennis alifungua akaunti yake ya mabao ndani ya ligi.

Kibu kwenye mchezo huu alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo ikiwa ni tuzo yake ya kwanza ndani ya msimu wa 2024/25 na alibainisha kuwa kwake ni furaha kuona timu inashinda na yeye anatwaa tuzo ya mchezaji bora.

Wakali kwenye kufunga hawa hapa

Mkali wa kufunga ndani ya Yanga SC ni Clement Mzize  yupo ndani ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi akiwa kafunga jumla ya mabao 13 msimu wa 2024/25.

Ikumbukwe kwamba Aprili 21 2025 dhidi ya Fountain Gate Mzize alifunga mabao mawili na alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo baada ya dakika 90 wakati wakisepa na pointi tatu mazima uwanjani kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.

Prince Dube wa Yanga SC naye katupia mabao 13 kibindoni sawa na Mzize wakiwa ni miongoni mwa nyota wenye mabao mengi ndani ya kikosi hicho kinachoongoza ligi. Kwa upande wa Simba SC ni Jean Ahoua ambaye ni kinara kwenye chati ya ufungaji. Kiungo huyu mshambuliaji chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids katupia mabao 15.

Soma na hii: Clement Mzize anafuata kuondoka Yanga SC baada ya Aziz Ki

Waliohusika kwenye mabao mengi

DUBEEEEEEEEEEEEE ️
Prince Dube na Mzize nyota wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Prince Dube nyota wa Yanga SC anaingia kwenye orodha ya wakali kwa mastaa waliohusika kwenye mabao mengi akiwa nayo 21 ambapo kafunga mabao 13 na katoa pasi 8. Ni miongoni mwa washambuliaji wenye hat trick ndani ya ligi alifunga kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa.

Kiungo Ahoua wa Simba SC yeye kahusika kwenye jumla ya mabao 23, amefunga jumla ya mabao 15 na kutengeneza pasi 8 za mabao. Anaingia kwenye orodha ya mastaa waliohusika kwenye mabao mengi. Kiungo huyu kafunga mabao 14 kwa mguu wa kulia na bao moja amefunga kwa pigo la kichwa.

Share this: