Fadlu DavidsFadlu Davids
  • Simba SC kwenye mechi nne za ligi zilizopita ndani ya dakika 360 ilishinda zote, safu ya ushambuliaji ilifunga mabao 10.
  • Singida Black Stars mchezo wa mzunguko wa kwanza wakiwa Uwanja wa Liti walipoteza pointi tatu jumlajumla mbele ya Simba SC.
  • Jean Ahoua mkali wa kucheka na nyavu kwenye kazi na Jonathan Sowah unaweza sema ni vita ya JJ ndani ya uwanja.

Simba SC vs Singida Black Stars mchezo wa Ligi Kuu Bara Mei 28 2025 unasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki kutokana na upinzani uliopo. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex saa 10:00 jioni.

Jean C- Ahoua
Jean Ahoua kinara wa utupiaji akiwa na mabao 15. Source: Simba SC.

Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids inapambania kutwaa ubingwa wa ligi huku Singida Black Stars inapambania kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo. Mchezo uliopita Simba SC ulikuwa ni wa fainali Kombe la Shirikisho Afrika, ilipishana na kombe kwa ubao kusoma Simba SC 1-1 RS Berkane.

Soma zaidi hapa: Simba SC 1-1 RS Berkane ya Morocco yatwaa ubingwa wa CAF Mei 25 2025

Msimamo wa Ligi Kuu Bara Simba SC vs Singida Black Stars

Simba SC kwenye msimamo wa ligi ni namba mbili baada ya kucheza mechi 26. Ushindi ni kwenye mechi 22, sare tatu na ilipoteza mchezo mmoja ilikuwa Simba SC 0-1 Yanga SC.

Rupia
Rupia nyota wa Singida Black Stars. Source: Singida Black Stars.

Inapambania nafasi ya kwanza ambayo ipo mikononi mwa watani zao wa jadi Yanga SC. Yanga SC ni mabingwa watetezi ni vinara wakiwa na pointi 73.

Simba SC imekusanya jumla ya pointi 69 kibindoni. Tofauti ya pointi nne ambazo zimewatenganisha na vinara wa ligi Yanga SC.

Safu ya ushambuliaji ya Simba SC imefunga jumla ya mabao 62. Ni timu namba mbili ambayo imefunga mabao mengi ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika.

Singida Black Stars kwenye msimamo ipo nafasi ya nne. Hawa wanapambania nafasi ya tatu dhidi ya matajiri wa Dar, Azam FC ambayo ipo nafasi ya tatu.

Singida Black Stars kibindoni ina pointi 53 baada ya mechi 27, Azam FC nafasi ya tatu na pointi 57 baada ya mechi 28 kushuka uwanjani msimu wa 2024/25.

Tofauti ya pointi nne kwa wababe hawa wawili ambao kila mmoja amekuwa katika ubora kwenye eneo lake. Safu ya ushambuliaji ya Singida Black Stars imefunga jumla ya mabao 40. Ile ya ulinzi imeruhusu mabao 21.

Ushindi kwa Singida Black Stars ni kwenye mechi 16, sare 5 na kupoteza mechi 6. Kwa Azam FC wao wamepata ushindi kwenye mechi 17, sare 6 wakipoteza mechi 5 pekee.

Mzunguko wa kwanza matokeo yao

Wababe hawa wawili walipokutana mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Liti ulisoma Singida Black Stars 0-1 Simba SC.

Ngoma kimataifa
Ngoma kimataifa

Bao la ushindi lilifungwa na Fabrince Ngoma ambaye alitumia pasi ya kiungo mshambuliaji Jean Ahoua. Nyota hawa wote wawili walianza kikosi cha kwanza dhidi ya RS Berkane.

Maneno ya makocha kuelekea mchezo

Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba SC amesema kuwa wanatambua uimara wa wapinzani wao Singida Black Stars ila watapambana kupata matokeo.

“Timu ya Singida Black Stars ni timu imara tunalitambua hilo hivyo tutaigia kwa tahadhari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja.”

 David Ouma Kocha Mkuu wa Singida Black Stars ameweka wazi kuwa wanakwenda kukutana na timu ambayo imecheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika jambo linalowapa maandalizi mazuri kimataifa.

“Tunawapa hongera Simba SC kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, tunaamini kucheza nao itatupa kipimo namna ambavyo tunapaswa kuwa kimataifa, tupo tayari.”

Mechi nne zilizopita kwa Simba SC walianza na Mashujaa

Mei 2 Simba SC ilicheza mchezo wa ligi matokeo ilikuwa Simba SC 2-1 Mashujaa FC, mabao yote yalifungwa na Leonel Ateba kwa penati na bao la Mashujaa FC lilifungwa na Jaffary Kibaya aliyemfunga Moussa Camara dakika ya 6.

Mei 5 mbele ya JKT Tanzania

 Mei 5 2025, ubao wa Uwanja wa Isamuhyo ilikuwa JKT Tanzania 0-1 Simba SC. Bao la ushindi kwenye mchezo lilifungwa na Fabrince Ngoma dakika ya 45 akiwa ndani ya 18 kwa pasi ya Steven Mukwala.

Mei 8 2025 walimalizana na Pamba Jiji

Mei 8 2025 Simba SC 5-1 Pamba Jiji unaingia kwenye orodha ya ushindi mkubwa katika mechi za viporo. Kiungo mshambuliaji Jean Ahoua alifunga mabao matatu ikiwa ni hat trick yake ya kwanza ndani ya ligi.

 Alifungua ukurasa wa mabao kwa kufunga dakika ya 15 kwa mkwaju wa penati, dakika ya 36 kwa pigo la faulo, dakika ya 47 kwa pigo la kichwa. Anafikisha mabao 15 akiwa kinara wa utupiaji ndani ya ligi.

Mei 11 2025 dhidi ya KMC

Mei 11 2025 kwenye mchezo wa nne ambao unakamilisha dakika 360 za viporo vya Simba SC baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma KMC 1-2 Simba SC. Pointi tatu zikawa mali ya Simba SC.

Rashid Chambo wa KMC FC alianza kumpa tabu kipa wa Simba SC, Moussa Camara dakika ya 8 akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kulia uliopeleka maumivu kwa kipa huyo.

Mukwala vs KMC
Mukwala mshambuliaji wa Simba SC kwenye mchezo dhidi ya KMC. Source: Simba SC.

 Mabao ya Simba SC yalifungwa na Steven Mukwala huku kiungo Yusuph Kagoma wa Simba SC akiokoa hatari iliyokuwa inakwenda langoni dakika ya 78.

Soma na hii: KMC 1-2 Simba SC mchezo wa nne kupata ushindi dakika 360

Kinara wa utupiaji ndani ya Singida Black Stars ni Mghana, Jonathan Sowah ambaye kafunga mabao 11.

Share this: