Khalid AuchoKhalid Aucho
  • Kiungo mwili jumba chaguo la kwanza la kocha akiwa kakomba dakika 1,555 uwanjani karudi katika majukumu yake.
  • Mtambo mwingine wa mabao unaofunga na kutengeneza pasi za mabao ukihusika kwenye mabao 18 nao warudi.
  • Kituo kinachofuata kwa Yanga SC ni Namungo mchezo wa ligi mzunguko wa pili, Uwanja wa KMC Complex.

Kiungo wa kazikazi kwenye eneo la ukabaji akiwa ndani ya uwanja katika kutimiza majukumu yake Khalid Aucho amerejea katika uwanja wa mazoezi tayari kwa mechi zijazo za ushindani. Kurejea kwa wachezaji wa Yanga SC uwanjani kunarejesha shangwe kwa benchi la ufundi kuwa na uchaguzi zaidi kikosi cha kwanza.

Mzize- Dube- Aucho
Clement Mzize, Khalid Aucho na Pacome kwenye moja ya mchezo wa ushindani. Source: Yanga SC.

Kurejea kwa Aucho ambaye ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi kunaongeza nguvu kwa timu hiyo kuelekea kwenye mechi za mwisho kukamilisha msimu wa 2024/25.

 Aucho ni kiungo mkabaji amerejea uwanja wa mazoezi baada ya kuwa nje kwa muda alipopata maumivu mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Ilikuwa ni Aprili 7 2025 Aucho aliumia alikwama kukomba dakika 90 aligotea dakika ya 45 ambapo nafasi yake ilichukuliwa na kiungo Mudathir Yahya.

Aprili 8 2025 Aucho alifanyiwa vipimo na taarifa iliyotolewa na Yanga SC ilieleza kuwa atakuwa nje kwa muda akipatiwa matibabu.

Rekodi za Aucho

Aucho Hsp
Aucho akifanyiwa vipimo Aprili 8 2025. Source: Yanga SC.

Mpaka anapata maumivu Aucho alikuwa amecheza jumla ya mechi 20 ndani ya ligi akikomba dakika 1,555 alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.

Kahusika kwenye mabao mawili ndani ya Yanga SC kati ya mabao 68 yaliyofungwa na timu hiyo inayoongoza ligi ikiwa na pointi 70 kibindoni baada ya kucheza jumla ya mechi 26.

Mchezo wake wa mwisho

Aucho v Fei
Khalid Aucho kwenye mchezo wake wa ushindani dhidi ya Azam FC. Source: Yanga SC.

Kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union huo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 3-0 Coastal Union.

Alikosekana kwenye mechi zilizofuata kutokana na kuendelea kupewa matibabu ilikuwa mchezo dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na mchezo dhidi ya Fountain Gate uliochezwa Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa.

Katika Dar Dabi Aprili 10 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 1-2 Yanga mabao ya Pacome na Prince Dube kwa Yanga na Lusajo kwa Azam FC.

Mchezo wa pili ilikuwa dhidi ya Fountain Gate Aprili 21 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Fountain Gate 0-4 Yanga pointi sita ndani ya dakika 180 ambazo alikosekana zote ilikuwa ni mali ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.

Ameanza mazoezi na wachezaji wenzake ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo ujao wa ligi dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kuchezwa Mei 13 2025 Uwanja wa KMC Complex.

Mshambuliaji Musonda arejea

Musonda
Kennedy Musonda mshambuliaji wa Yanga SC naye amerejea kwenye ubora wake.Source: Yanga SC.

Mbali na Aucho ambaye alipata maumivu kwenye mchezo wa ligi Bongo, mshambuliaji Kennedy Musonda huyu alipata maumivu kwenye Muungano Cup 2025.

Hali yake naye inazidi kutengamaa kwa ajili ya mechi zijazo jambo linaloongeza tabasamu kwa benchi la ufundi la timu hiyo kuwa na chaguo la nani ataanza kwenye mechi zijazo.

Pacome kazini

Pacome z
Pacome kiungo mshambuliaji wa Yanga SC mwenye mabao 9 ndani ya ligi 2024/25. Source: Yanga SC.

Kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua huyu alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Azam FC tayari amerejea kwenye uwanja wa mazoezi ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo ujao wa ligi dhidi ya Namungo.

Pacome ni mkali kwenye kutengeneza pasi za mwisho za mabao na anajua kuwapa tabu makipa kwa kuwatungua akiwa kafunga mabao 9 na pasi 9 za mabao akihusika kwenye mabao 18 kati ya 68 yaliyofungwa na timu hiyo.

Daktari wa Yanga huyu hapa

Kwa mujibu wa daktari wa Yanga Moses Etutu ameweka wazi kuwa hali ya wachezaji wa Yanga SC ambao walikuwa wakipewa matibabu zinazidi kuimarika.

“Musonda alipata maumivu kwenye Muungano Cup 2025 kwa sasa anaendelea vizuri na tunaamini kwamba atarejea uwanjani kwa ajili ya mechi zetu ambazo zinafuata ikiwa atakuwa fiti zaidi na benchi la ufundi likiamua kumtumia.

“Pacome yeye naye anaendelea vizuri kwa sasa saw ana Khalid Aucho hivyo kwa kuwa mchezo ujao utakuwa baada ya siku saba itakuwa maamuzi ya benchi la ufundi kuona kama itawatumia au la ila ambacho tunapambania kwa sasa kuona wanarejea kwenye ubora.”

Ratiba Bongo Mei hii hapa

KMC vs Simba SC, Mei 11 2025, Uwanja wa KMC Complex.

Mei 12 2025

Tanzania Prisons vs Coastal Union, Uwanja wa Sokoine.

Kagera Sugar vs Mashujaa FC, Uwanja wa Kaitaba.

Hizi hapa kupigwa Mei 13 2025

JKT Tanzania vs Fountain Gate, Uwanja wa Isamuhyo.

KenGold FC vs Pamba Jiji, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Yanga SC vs Namungo, Uwanja wa KMC Complex.

Azam FC vs Dodoma Jiji, Uwanja wa Azam Complex

Mei 14 2025

Tabora United vs KMC, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Kigogo cha kufungia Mei

Simba SC vs Singida Black Stars, Uwanja wa KMC Complex.

Share this: