PSG Vs ArsenalPSG Vs Arsenal
  • PSG Vs Arsenal UEFA CL ni zaidi ya nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, bali ni mchezo gumzo ambao unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mamilioni ya mashabiki wa duniani.
  • Mchezo huu utapigwa kwenye dimba la Parc des Princes, Paris saa 4:00 Usiku (kwa saa za Afrika Mashariki) na kusimamiwa na mwamuzi rai awa Ujerumani, Felix Zwayer.
  • Arsenal anahitaji ushindi wa tofauti ya mabao mawili ili kufuzu fainali, huku PSG akihitaje sare tu, kufuatia matokeo ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa ushindi wa bao 1-0 kwa PSG

PSG Vs Arsenal UEFA CL ni zaidi ya nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, bali ni mchezo gumzo ambao unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mamilioni ya mashabiki wa duniani kote kujua nani atafuzu fainali?

Mchezo huu wa mkondo wa pili umekuwa gumzo kubwa hasa kutokana na ubora wa soka safi na ufundi ambao unatandazwa na kuonyeshwa na timu zote mbili msimu huu.

Arsenal wanauendea mchezo wa leo wakiwa ndiyo wageni baada ya kusafiri kilomita nyingi kutoka nchini England mpaka jijini Paris katika dimba la Parc des Princes.

SOMA HII PIA: UEFA CL NIGHTS ARE BACK; ARSENAL Vs PSG PLACE YOUR BET WITH SPORTPESA NOW

Arsenal kwenye mtihani mzito

PSG Vs Arsenal UEFA CL
PSG wakishangilia bao lao Vs Arsenal

Vijana wa kocha, Mikel Arteta wataingia katika mchezo huo wakiwa nyuma kwa bao 1-0 kutokana na matokeo ya mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa jijini London, England wiki iliyopita.

Kutokana na matokeo hayo ya mkondo wa kwanza, Arsenal wanahitaji kufunga angalau mabao mawili au zaidi ili kufuzu kwa fainali yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu mwaka 2006.

Ni bao pekee la mapema la staa wa kimataifa wa Ufaransa, Ousmane Dembélé katika mechi ya kwanza ndilo linawaweka PSG mbele kabla ya mechi ya marudiano leo huko Paris.

SOMA HII PIA: Inter Milan Vs FC Barcelona ‘live’: Vikosi, uchambuzi, utabiri

Arsenal kupindua meza baada ya vipigo vitatu mfululizo?

Ni wazi kuwa Arsenal wanahitaji kuboresha kiwango chao leo ili kuta matokeo hasa baada ya kuwashuhudia wakipoteza kwa Bournemouth nyumbani mwishoni mwa wiki, ikiwa ni kipigo cha tatu mfululizo.

Sare yoyote PSG wanakwenda fainali

Huku Arsenal wakiwa na kazi kubwa ya kutafuta angalau mabao mawili ili kutinga fainali, PSG wao wanajua kuwa kuepuka kipigo na matokeo yoyote ya sare yatawapa nafasi ya kufuzu fainali ya kwanza tangu 2020.

PSG wamepoteza mara tatu tu, nyumbani msimu huu, ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya Liverpool katika hatua ya 16 bora n ani wazi Arsenal wanahitaji kuonyesha ubora wao ili kufuzu kwa fainali.

Dondoo muhimu za PSG Vs Arsenal UEFA CL

------------------------------------------------n
Kikosi cha Arsenal

Ratiba ya Mechi: Jumatano, Mei 7

Mahali: Parc des Princes, Paris

Muda wa Mechi: Saa 4:00 Usiku (kwa saa za Afrika Mashariki).

Mwamuzi: Felix Zwayer (Ujerumani)

VAR: Bastian Dankert (Ujerumani)

Rekodi zao walipokutana H2H

PSG Vs Arsenal katika michezo yao mitano iliyopita;

PSG: ushindi x 1

Arsenal: ushindi x 2

Sare: 2

Mwenendo wao katika michezo michezo mitano iliyopita ya mashindano yote;

PSG                                                      Arsenal

PSG 2–1 Strasbourg                          Arsenal 1–2 Bournemouth

PSG 1–3 Nice                                     Arsenal 0–1 PSG

PSG 2–1 Le Havre                              Arsenal 2–2 Crystal Palace

PSG 1–0 Liverpool                             Arsenal 2–1 Ipswich

PSG 2–1 Lyon                                     Arsenal 1–2 Real Madrid

Nini kinaendelea ndani ya kambi za timu zote mbili?

PSG:

Licha ya awali kuwepo hofu juu ya uwezekano wa kupata huduma ya kiungo, Ousmane Dembélé ambaye alilazimika kutolewa kipindi cha pili kwa hofu ya jeraha za nyama za paja, kiungo huyo atakuwepo.

Dembele ameonekana akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza na tayari kocha wa PSG, Luis Enrique amethibitisha kuwa mchezaji huyo atakuwa sehemu ya kikosi leo Jumatano.

Ndani ya kikosi cha PSG, staa pekee ambaye anatarajiwa kukosa mchezo wa le oni Mlinzi wa kimataifa wa Ufaransa, Presnel Kimpembe ambaye bado anaendelea kuuguza majeraha.

Arsenal:

Pigo zito kwa Arsenal ni kuwa kwenye hatari ya kukosa huduma ya baadhi ya mastaa wao, Martin Ødegaard, Mikel Merino, Oleksandr Zinchenko, Takehiro Tomiyasu, na Kieran Tierney ambao wote wameelezwa kuwa huenda hawatakuwa kwenye kikosi kutokana na majeraha.

Staa mwingine anayetarajiwa kukosa mchezo huu ni mlinzi, Ben White, hivyo Jurrien Timber anatarajiwa kuendelea kucheza beki wa kulia.

PSG Vs Arsenal UEFA CL vikosi tarajiwa

------------------------------------------------n
Kikosi cha PSG

Kikosi cha PSG ambao wanatumia mfumo wa 4-3-3 kinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo:

Donnarumma, Hakimi, Marquinhos, Pacho, Mendes; Neves, Vitinha, Ruiz; Doué, Dembélé, Kvaratskhelia.

Arsenal

Kikosi cha Arsenal ambao wanatumia mfumo wa 4-3-3 kinatarajiwa kuwa na:

Raya, White, Saliba, Kiwior, Lewis-Skelly; Ødegaard, Partey, Rice; Saka, Merino, Martinelli.

Utabiri wa Matokeo ya mchezo wa leo

PSG walikuwa bora zaidi katika mechi ya kwanza na wanahitaji kuepuka kipigo ili kufuzu kwa fainali, huku Arsenal nao wakihitaji kuboresha kiwango chao ili kufuzu kwa fainali.

Tunatarajia mchezo mgumu lakini PSG anapewa nafasi ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.