Athletic Vs Man UnitedAthletic Vs Man United

  • Athletic Club Vs Man United 1/5/2025, ni mchezo wa kukata na shoka wa hatua ya Nusu Fainali ya kombe la Europa.
  • Mara ya mwisho Athletic Club kuvaana na Man United ilikuwa Machi 15, mwaka 2012 ambapo Athletic Club walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
  • Kwenye mashindano ya Ligi Kuu mpaka sasa Man United wapo kwenye nafasi ya 14 katika msimamo, huku Athletic wao wakiwa nafasi ya nne

Athletic Club Vs Man United 1/5/2025, ni mwendelezo wa michezo ya usiku wa Ulaya ambao unatarajiwa kufuatiliwa na mamilioni ya mashabiki kote dunia, katika hatua ya Nusu Fainali ya kombe la Europa.

Man United ambao walionekana kuwa kwenye hatari ya kutolewa kwenye robo fainali mikononi mwa timu ya Ufaransa, Lyon, mapema mwezi huu wamesafiri hadi Basque, Uhispania kwa ajili ya mchezo huo.

Mashetani hao wekundu walikuwa na dakika sita tu, za kupindua meza dhidi ya Lyon na kushinda kwa kishindo mchezo huo kwa ushindi wa mabao 5-4, mchezo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, hivyo kujikatia tiketi ya kucheza nusu fainali.

Athletic Club Vs Man United 1/5/2025: fomu yao kwenye ligi

The talking is over and now it's time to bring it #MUFC #ManUtd #EuropaLeague
Mastaa wa Man United

Man United wamekuwa na msimu mbaya katika ligi ya ndani, ambapo mpaka kufuikia wikiendi iliyopita walikuwa nafasi ya 14 katika msimamo baada ya matokeo ya sare dhidi ya Bournemouth,.

Kocha wa kikosi cha Man United, Reuben Amorin ameweka wazi kuwa kwa sasa nguvu zao zote wanazielekeza katika mashindano ya Europa.

Hata hivyo, itawabidi wajitahidi sana kuwa bora dhidi ya Athletic Club, ambao wanaonekana kupewa nafasi kubwa ya kufuzu hatua ya fainali ya mashindano haya.

Waliwatoa Rangers kwa urahisi ili kufuzu kwa hatua hii, na walikuwa timu bora katika hatua ya makundi. Katika ligi ya ndani, kikosi cha Ernesto Valverde kipo nafasi ya nne kwenye La Liga na kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Dondoo muhimu kuhusu mechi Athletic Club Vs Man United 1/5/2025

Hali ya majeraha

Athletic Club huenda wakamkosa Mfungaji bora, Oihan Sancet huenda akakosa mechi hii baada ya kuumia msuli wa paja katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Las Palmas Jumatano iliyopita.

Licha ya changamoto hiyo lakini habari njema kwao ni kuwa staa wa kikosi hiko, Nico Williams aliyekuwa na tatizo dogo la majeraha huenda akawa sehemu ya kikosi cha leo.

Rekodi zao

Mechi ya mwisho kwa Athletic Club kuvaana na Man United ilikuwa Machi 15, mwaka 2012 ambapo Athletic Club walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na ilikuwa katika mashindano haya ya Europa.

Maandalizi ya mchezo

Athletic wamepata muda wa kutosha kujiandaa baada ya ushindi huo, na huenda wakamrejesha, Unai Gomez ili kuziba pengo la Sancet. Williams, aliyekuwa akitokea benchi Jumapili, ataanza upande wa kushoto wa Athletic. Ndugu yake, Inaki huenda akaanza benchi.

Kikosi cha Athetic Club kinachotarajiwa leo

Kikosisi cha Athletic
Kikosisi cha Athletic

Kikosi kinachotarajiwa cha Athletic Club Vs Man Utd 1/5/2025 ni kama ifuatavyo; Simon; De Marcos, Vivian, Yeray, Lekue; Ruiz, Jauregizar; Berenguer, Nunez, N. Williams; Sannadi.

Mfumo tarajiwa Athletic Club (4-2-3-1).

Kuhusu maandalizi ya Man United

Athletic Club Vs Man United 1/5/2025
Amad and Mathias De Light

Man Utd hawana majeraha mapya kutoka katika mchezo wa sare ya Jumapili dhidi ya Bournemouth, lakini wanakosa wachezaji kadhaa muhimu kwa mechi ya kwanza nchini Hispania.

Diogo Dalot yupo nje kwa sababu ya jeraha la mguu, huku Lisandro Martinez, Joshua Zirkzee, na Ayden Heaven pia wakiwa majeruhi. Matthijs de Ligt na Amad huenda wakarejea leo huku, Toby Collyer, na Altay Bayindir nao hawatarajiwi kucheza kutokana na matatizo ya kiafya.

Luke Shaw alianza mechi yake ya kwanza msimu huu wikendi iliyopita lakini huenda asianze tena, huku Rasmus Hojlund akitarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Bournemouth.

Kikosi kinachotarajiwa cha Man Utd dhidi ya Athletic Club:

Kikosi cha Man United
Kikosi cha Man United

Onana; Lindelof, Maguire, Yoro; Mazraoui, Ugarte, Casemiro, Dorgu; Fernandes, Garnacho; Hojlund.

Mfumo unaotarajiwa Man Utd (3-4-2-1).

Utabiri wa Matokeo: Athletic Club vs Man Utd

Baadhi ya mechi bora za Man Utd chini ya Amorim zimekuja katika mashindano haya, lakini hakuna shaka kuwa safari ya kwenda San Mames ni ngumu zaidi kwao hadi sasa.

Ili United wapate matokeo mazuri, itawalazimu kuhimili shinikizo la mashabiki wa Basque, lakini hatujaona uimara wa kutosha kutoka kwa United, hasa katika kumiliki mpira, kuashiria kuwa wanaweza kufanikisha hilo.

Kumekuwa na dalili nzuri hivi karibuni, hasa katika ulinzi kwenye Ligi Kuu, lakini mechi hii inaonekana kuwa ngumu kwa wageni ingawa Athletic huenda wasiwashinde United kwa idadi kubwa ya mabao, wana nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi na kwenda nao Old Trafford.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.