- Barcelona Vs Inter Milan 30/4/2025 itashuhudiwa na mamilioni ya mashabiki duniani ambapo mchezo utaanza kupigwa majira ya saa 4:00 usiku, Uwanja wa Olimpic Lluis Companys.
- Barcelona Vs Inter Milan wana rekodi ya kucheza mechi 5, ambapo Barcelona wameshinda mechi 2, Inter wameshinda mechi 1, na michezo 2 imeisha kwa sare.
- Timu zote mbili zinakumbana na changamoto ya majeraha ambapo pamoja na mastaa wengine Barcelona itaendelea kumkosa mshambuliaji wao kiongozi, Robert Lewandowski huku iInter tatizo lao kubwa, Marcus Thuram.
Barcelona Vs Inter Milan 30/4/2025 ni mchezo mkubwa wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao unatarajiwa kufuatiliwa na mamilioni ya mashabiki leo usiku.
Katika mchezo huu wa mkondo wa kwanza, Barcelona wanatarajia kuwa wenyeji katika dimba la Olimpic Lluis Companys, ambapo mchezo unatarajia kuanza majira ya saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
UBINGWA WA COPA DEL REY WAIPA JEURI BARCA

Barcelona inaingia katika mchezo huu wakiwa katika fomu nzuri, mara baada ya kufanikiwa kuwafunga mahasimu wao Real Madrid 3-0 na kufanikiwa kuibuka mabingwa wa Kombe la Mfalme siku ya Jumamosi.
Bao la mlinzi wa kimataifa wa Ufaransa, Jules Kounde katika muda wa nyongeza lilimpa kocha, Hansi Flick taji lake la pili katika msimu wake wa kwanza.
Barcelona pia wako mbele kwenye mbio za kusaka ubingwa wa La Liga na ndoto yao ya Ligi ya Mabingwa ikiwa bado hai, hivyo kuwaweka kwenye nafasi kubwa ya kutwaa mataji manne msimu huu.
BARCELONA Vs INTER MILAN 30/4/2025 NI MCHEZO MGUMU, LAKINI BARCELONA WANA NAFASI KUBWA
Barcelona wanapaswa kuishinda Inter katika mechi mbili za nusu fainali ili kutimiza ndoto yao ya kubeba ubingwa wa Ulaya, jambo ambalo halitakuwa rahisi.
Safu ya ushambuliaji ya Barcelona ambayo imeonekana kuwa tishio msimu huu, haitakuwa na kazi nyepesi kuvunja safu ya ulinzi ya kocha, Simone Inzaghi.
Hata hivyo, matokeo ya hivi karibuni ya Inter yataipa Barcelona matumaini. Nerazzurri wamepoteza mechi zao tatu zilizopita katika mashindano yote bila kufunga bao.
Inter wanatarajiwa kucheza kwa tahadhari watakapowasili kwenye Uwanja wa Estadi Olimpic Lluis Companys leo kwenye mchezo Barcelona Vs Inter Milan 30/4/2025 katika mpango wao wa kutoka Catalonia wakiwa na matokeo ya kuvutia kuelekea mchezo wa marudiano wiki ijayo San Siro.
BARCELONA Vs INTER MILAN 30/4/2025 DONDOO MUHIMU ZA MCHEZO

Uwanja: Estadi Olimpic Lluis Companys
Tarehe: Jumatano, Aprili 30
Muda wa Kuanza: 4:00 USIKU
Mchezo: Barcelona Vs Inter Milan 30/4/2025
Refarii: Clement Turpin (Ufaransa)
VAR: Jerome Brisard (Ufaransa)
REKODI YA MECHI TANO ZILIZOPITA KATI YA BARCELONA Vs INTER

Wamecheza mechi 5
Barcelona: ushindi 2, Inter: ushindi 1, Sare: 2
BARCELONA KUENDELEA KUMKOSA LEWANDOWSKI
Barcelona kwenye mchezo wa leo Barcelona Vs Inter Milan 30/4/2025 itaendelea kumkosa mshambuliaji wao kiongozi, Robert Lewandowski ambaye bado anauguza jeraha la msuli wa paja na huenda akakosa pia mchezo wa mkondo wa pili.
Lewandowski anaungana na Marc Bernal na Marc Casado katika chumba cha matibabu. Alejandro Balde yuko karibu kurudi uwanjani lakini Barcelona watachukua tahadhari kutokana na aina ya jeraha lake.
Gerard Martin ataendelea kucheza katika nafasi hiyo iwapo Balde hatatumika. Kulikuwa na wasiwasi kuhusu Frenkie de Jong, Pedri na Ferran Torres baada ya wote watatu kutolewa wakati wa fainali ya Jumapili, lakini wote watakuwa tayari kuivaa Inter.
Marc-Andre ter Stegen alirejea kwenye kikosi kwa mara ya kwanza tangu Septemba wakati Barcelona walipoifunga Madrid, jambo linalomaanisha kuwa sasa atachuana na Wojciech Szczesny kuwania nafasi ya kuanza langoni.
KIKOSI CHA BARCELONA KINACHOTARAJIWA Vs INTER
Szczesny; Kounde, Cubarsi, Martinez, Martin; De Jong, Pedri; Yamal, Olmo, Raphinha; Torres.
Mfumo unaotarajiwa kutumika (4-2-3-1)
INTER KUMKOSA THURAM
Marcus Thuram ndiye tatizo kubwa la majeraha kwa Inter baada ya kukosa mechi tatu zilizopita jambo ambalo limewaathiri sana na kuna nafasi kubwa ya kukosa mchezo wa leo.
Piotr Zielinski na Denzel Dumfries walirejea uwanjani mwishoni mwa wiki lakini Benjamin Pavard alipata jeraha kwenye mechi dhidi ya Roma.
Mfaransa huyo, ambaye alifunga dhidi ya Bayern Munich kwenye robo fainali, alidumu uwanjani kwa dakika 15 tu kabla ya kuumia kifundo cha mguu na kuna uwezekano mkubwa hatacheza leo.
Kiungo chipukizi mshambuliaji, Valentin Carboni bado ni majeruhi wa muda mrefu.
KIKOSI CHA INTER KINACHOTARAJIWA Vs BARCELONA

Sommer; Bisseck, Acerbi, Bastoni; Dumfries, Mkhitaryan, Calhanoglu, Barella, Dimarco; Martinez, Thuram.
Mfumo tarajiwa (3-5-2)
UTABIRI WA MATOKEO YA BARCELONA VS INTER
Inter ni timu ngumu kufungwa wala kuruhusu mabao mengi, lakini wanakuja katika mechi ya Barcelona Vs Inter Milan 30/4/2025 wakiwa katika hali mbaya. Hawajashinda mechi yoyote kati ya nne zilizopita na hawajafunga bao katika mechi tatu mfululizo hali inayowapa hofu kuelekea mechi hii.
Barcelona, kwa upande mwingine, wako kwenye hali nzuri baada ya kutwaa kombe na kushinda mechi 12 kati ya 14 walizocheza karibuni. Ingawa watachukua tahadhari dhidi ya mashambulizi ya kushtukiza ya Inter hasa kutoka kwa Lautaro Martinez
Hivyo huenda mechi ikaisha kwa matokeo ya Barcelona 2-1 Inter

