- Ligi kuu inafuatiliwa na Watanzania kwa ukaribu sana haswa mabao ndani ya 18.
- Timu zilizo tupa mabao zaidi ya 15 ni kama Simba SC, Yanga SC, and Azam FC.
- Simba SC imetupia mabao manne pekee nje ya 18 msimu wa 2024/25.
- Timu bora zilizofunga ndani ya boksi la 18 Ligi kuu ya NBC Tanzania 2024/2025
Kuna timu ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ukiwapa nafasi ndani ya 18 lazima utaokota kunyavu na uyashibe magoli. Wachezaji hatari kama Feisal Salum wa Azam FC, na Jean Ahoua wa Simba SC ni mojawapo ya wachezaji walioinua timu zao kufika kwa kilele mwa orodha ya timu kubwa. Je, timu bora ndani ya boksi la 18 Ligi kuu ya NBC Tanzania 2024/2025 ni zipi?

Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi hii ni namba moja kwenye eneo na watani zao wa jadi Simba SC wanafuata.
Ni timu bora zilizofunga ndani ya boksi la 18 Ligi kuu ya NBC Tanzania 2024/2025?
Kwa mujibu wa takwimu za Bodi ya Ligi Tanzania, hapa tunakutelea orodha ya timu ambazo zina balaa kubwa ndani ya 18 namna hii:-
Simba SC- mabao 48
Simba SC ni namba mbili kwa timu iliyofunga mabao mengi ikiwa ndani ya 18 ambayo ni 48. Ukiweka kando kuwa namba mbili kwenye kufunga mabao mengi ikiwa ndani ya 18 ni namba mbili kwenye msimamo.

Mechi 22 imeshuka uwanjani ikikusanya jumla ya mabao 52 ni mabao manne pekee Simba imefunga ikiwa nje ya 18. Kinara wakutupia kutoka ndani ya kikosi cha Simba SC ni Jean Ahoua mwenye mabao 12.
Katika dakika 1,980 ilizocheza imekuwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 38 ndani ya uwanja. Ni dakika 41 Simba SC ina wastani wakuwa na hatari kwenye kufunga mabao ikiwa ndani ya 18 katika mabao 48 ambayo imetupia.
Azam FC mabao- 38
Matajiri wa Dar, Azam FC ni namba tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 54 baada ya mechi 27. Safu ya ushambuliaji imetupia mabao 43 ikiwa ni timu namba tatu yenye mabao mengi ndani ya ligi.
Azam FC wachezaji wametupia mabao matano wakiwa nje ya 18 ikiwa ni timu namba tatu kwa kutupia mabao mengi ndani ya 18.
Toto Fei nyota wa Azam FC kinara wa utengenezaji pasi za mwisho akiwa nazo 13. Source: Azam FC.
Ina wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 56 baada ya kucheza dakika 2,430 kwenye mechi za ushindani ndani ya ligi. Ipo wazi kwamba wamefungashiwa virago kwenye Muungano Cup 2025.
Singida Black Stars – 37
Hawa wanatumia Uwanja wa Liti kwenye mechi za nyumbani ni namba nne kwenye msimamo ikiwa timu namba nne kufunga mabao mengi ikiwa ndani ya 18 ambayo ni 37.
Baada ya kucheza mechi 27 ambazo ni dakika 2,430 safu ya ushambuliaji ya Singida Black Stars inayoongozwa na Jonathan Sowah mwenye mabao 11 ni mabao 40 imetupia. Hivyo ni mabao matatu pekee Singida Black Stars imetupia ikiwa nje ya 18. Wastani wake kwenye kucheka na nyavu ndani ya uwanja ni kila baada ya dakika 60.
Tabora United – 23
Tabora United ipo ndani ya tano bora kwenye msimamo ni timu inayoshikilia rekodi kuifunga mabao mengu Yanga SC ndani ya dakika 90 msimu wa 2024/25 kwenye mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 1-3 Tabora United.
Safu yake ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 27, ni mabao manne ilitupia ikiwa nje ya 18, Baada ya kucheza mechi 27 ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 90 kwenye dakika 2,430 ilizoshuka uwanjani.
Dodoma Jiji – 23
Kwenye msimamo wa ligi ni namba sita ikiwa kwenye orodha ya timu ambazo zimefunga mabao mengi ndani ya 18. Ni mechi 27 ilishuka uwanjani na safu ya ushambuliaji ikitupia mabao 37. Mabao 14 wachezaji walitupia wakiwa nje ya 18.
Namungo – 22
kosi cha Yanga SC ni Clement Mzize ambaye katupia jumla ya mabao 13 msimu wa 2024/25 akiwa kwenye mbio za kuwania kiatu cha ufungaji bora.
Mechi 22 imeshuka uwanjani ikikusanya jumla ya mabao 52 ni mabao manne pekee Simba imefunga ikiwa nje ya 18. Kinara wakutupia kutoka ndani ya kikosi cha Simba SC ni Jean Ahoua mwenye mabao 12.
Katika dakika 1,980 ilizocheza imekuwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 38 ndani ya uwanja. Ni dakika 41 Simba SC ina wastani wakuwa na hatari kwenye kufunga mabao ikiwa ndani ya 18 katika mabao 48 ambayo imetupia.
Ikiwa nafasi ya 9 kwenye msimamo baada ya kucheza jumla ya mechi 27, safu ya uhambuliaji imetupia mabao 23, pointi zake ni 31 kibindoni msimu wa 2024/25. Ni bao moja limefungwa ndani ya Namungo kwa mchezaji kuwa nje ya 18 mpaka sasa kwenye mabao yao 23.

