UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa mpango mkubwa ni kuvuna pointi tatu mbele ya Tabora United mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kwa dakika 90 zakuvuja jasho ndani ya uwanja.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Tabora United ni muhimu kupata ushindi kwa kuwa walipoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza hivyo utakuwa ni mchezo wa kisasi huku Tabora United wakibainisha kuwa haitakuwa rahisi.

Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ni mabingwa watetezi wa ligi walitwaa msimu wa 2023/24 chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambaye alikutana na mkono wa Thank You.
Kamwe amesema kuwa kila kitu kipo tayari kuelekea kwenye mchezo huo na maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa kilichobaki ni mashabiki kujitokeza kwa wigi uwanjani kuishangilia timu hiyo.
“Mashabiki hii ni timu yenu ni muda kujitokeza kwa wingi kuwashangilia wachezaji wetu wakiwa wanasaka pointi tatu muhimu, huu mchezo una maana kubwa ukizingatia kwamba mchezo wa mzunguko wa kwanza tulipoteza.”
Ni muda wako kukunja mkwanja zaidi ya mamilioni kutoka SportPesa kupitia mechi mbalimbali za kitaifa na kimataifa.
HUYU HAPA KOCHA YANGA
Miloud Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema watapambana kufanya kazi kubwa mbele ya Tabora United ili wapate pointi tatu muhimu katika mchezo ujao unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.
Machi 2025 Yanga ilifunga kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Songea United mchezo wa CRDB Federation Cup ilikuwa ni Machi 29 ambapo mabao yalifungwa na Duke Abuya dakika ya 22 na Jonathan Ikanga Lombo dakika ya 54.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex nyota wa Yanga Pacome Zouzoua alichaguliwa kuwa mchezaji bora na kupewa zawadi ya laki tano na mdhamini benki ya CRDB.
Miloud amesema wachezaji wanajituma kwenye kutafuta ushindi jambo ambalo linawapa nguvu kushinda na kila mchezo wanautazama kwa umuhimu ndani ya uwanja.
“Kila mchezo ambao tunacheza kwetu tunauchukulia kwa umuhimu ambacho tunahitaji ni kupata pointi tatu, mashabiki wazidi kuwa nasi kwani tunatambua mchezo ujao utakuwa ni wa ligi na ushindani ni mkubwa.”
TABORA UNITED SIO KINYONGE
Tabora United wametamba kuwa hawapo tayari kuona wanapoteza pointi tatu wakiwa nyumbani kutokana na maandalizi mazuri na ubora wa kikosi chao kwenye mechi za ushindani ndani ya uwanja.
Kwenye msimamo Tabora United ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 37 baada ya mechi 23, ushindi ni kwenye mechi 10 katika hizo moja ilivuna pointi tatu mazima ugenini dhidi ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi.
Ilipoteza mechi 6 ikiambulia sare kwenye mechi 7 ndani ya msimu wa 2024/25 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 27 ukuta umeruhusu mabao 28.
Christina Mwagala, Ofisa Habari wa Tabora United ameweka wazi kuwa wanatambua wapinzani wao wanahitaji kulipa kisasi cha kupoteza mchezo uliopita hilo wasahau kwa kuwa wapo imara na wanhitaji pointi tatu.
“Tutakuwa nyumbani kwenye mchezo wetu ujao kikubwa tunahitaji pointi tatu kwa kuwa kazi yetu ni kuleta ushindani, tulipata ushindi mzunguko wa kwanza na sasa tunahitaji alama nyingine mbele yao, mashabiki wawe pamoja nasi kwani hili linawezekana.
“Ikiwa utakuwa unacheza na Tabora United lazima uogope kwa kuwa ni timu kubwa na imara kama ilivyo Al Ahly uwanjani nasi tunatambua tupo vizuri kwa ajili ya kusaka ushindi hakuna suala la hofu hapa kila kitu kipo kamili.”

Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90, Novemba 7 2024 ubao ulisoma Yanga 1-3 Tabora United, bao la kufutia machozi kwa Yanga lilifungwa na Clement Mzize.
Kocha aliyekuwa benchi kwenye mchezo huo kwa sasa hayupo kwani timu ipo chini ya Genesis Mang’ombe huyu ni kocha anatarajiwa kukaa benchi Aprili 2 2025 baada ya kuchukua mikoba ya Anicet Kiazmak aliyekuwa benchi kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza.

